Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Friday, December 9, 2016

DARASA KATIKA WIMBO WAKE NI KAMA ANAWACHANA DIAMOND NA KIBA

                           Darasa                                                          Alikiba                                           Diamond

Na. Furaha Venance

1.  Darasa anaanza kuwaponda wasanii ambao wanakomaa katika game lakini mambo yamekuwa magumu kwao. Anawaambia:

Rudi utotoni,
Usipotembea utabebwa mgongoni.

Hapa anawazungumzia wasanii ambao walipata kiki kwa kubebwa na media (kumbuka anayebebwa ni Mtoto). Hivyo anawataka warudi enzi hizo za kubebwa au wawatafute watu wa kuwabeba.

2.      Diamond ni msanii ambaye anajisifu sana kuwa yeye ndiye msanii anayelipwa zaidi kuliko msanii yoyote Bongo, ndiye msanii mwenye nyumba Sauz, ndiye msanii pekee anayelipa kodi zaidi ya mil/ 30 TRA. Mashakibiki wa muziki wanamuonma kama ni msanii mwenye sifa sana na ni kama ameota mapembe kutokana na misifa yake. Darasa anamwambia:

 Wanaoota mapembe waongezee mkia.

3.      Kiba na Diamond wanajisifu kuwa wao ni wakali hadi kufikia kujifananisha na wanyama, Diamond anajiita Mnyama, Simba huku mashabiki wa Kiba wakimwita mfalme huyo Tembo. Darasa anawambia:
Blah blah sitaki kusikia,
siyo Simba, siyo Chui,
siyo mamba, haaha ”

Akiwa na maana kwake hakuna cha samba, chui wala mamba wote hao anawameza ndiyo maana anamalizia na kibwagizo “Haaaaa!” (kumeza).

4.      Diamond ni msanii anayesifika kwa mashauzi, kujigamba n.k. yemwenyewe anajiita mswahili wa uswahilini hasa. Darasa anamwambia:

Pumzi yangu inatosha kujigamba,
Na sina maneno ya kwenye kanga

Hapa anamaana kuwa kazi (pumzi) zake zinatosha kujigamba wala hana maneno ya kwenye kanga (maneno ya uswahili).

5.      Diamond ni msanii anayemiliki wasanii kadha wa kadha. Miongoni mwao kuna Richmavoko, Raymond, Harmonize na Queen Darlin. Kati ya wasanii hawa Harmonize ameonekana kuzua kizaazaa. Wapo wanamuona hatafika mbali, kutokana na kukosa ubunifu wake na kumuiga zaidi Diamond katika muziki hadi maisha yake binafsi. Sasa hapa ni kama Darasa anamuonya Diamond:

Kuzaa unawe kuzaa kizaazaa,
Sinzia na fegi uchome kibanda. 

Akiwa na maana Diamond ni kama amemzaa Harmonize lake badala yake amezua kizaa, akiendelea kumkumbatia (sinzia na fegi) anaweza ua WCB (choma kibanda).

6.     Wapo wanasema kuwa WCB chini ya Diamond hawafanyi muziki zaidi ya kufanya usanii usanii tu. Miongoni wa wasanii wanaosema hivi ni Ommy Dimpoz na Team Kiba. Darasa ni kama anaungana nao na kumwambia Diamond:

Maisha na muziki,
acha maneno weka muziki.

7.  Kwa sasa bila ubishi Diamond ndiye msanii aliyejuu. Huku Kiba akikimbizana kuhakikisha anamshusha msanii huyo. Sasa kaja Ommy Dimpoz naye anataka kuchuana, kukimbizana na Diamond ambaye anaonekana amewaacha, sasa Darasa anawambia wasanii hawa:

Unataka kukimbia na hauna break,
what do you expect?

Hapa ni sawa na kuwaambia wanataka kushindana wakati hawana mbinu za ushindani. Muziki ni kuwekeza mkwanja, ubunifu na kipaji ili ufike unapotaka.

8.     Diamond ni msanii anayesemwa kuwa anajifanya mjuaji sana, mademu anawajua yeye, muziki anajua yeye, maisha anayajua yeye yaani kila kitu anajua yeye. Sasa kuhusu madem, Darasa anamwambia:

Watch yourself, usije ukaji-comfuse…
Vitu vingine havitakagi ujuaji,
utajikuta unatandikia watu jamvi.”

Hapa ni kama anamwambia kungonoka na madem wa kila aina haitaki ujuaji asijejikuta anaaga dunia kwa ngoma. Si unajua tena mtu akifariki kinachofuata ni kutandika majamvi msibani! (pia inaweza kuwa kuwapa watu maneno ya kusema na kukukalia kitako kukusema).

9.  Kuna hili linasemwa na teamkiba hasa Ommy Dimpoz kuwa wapo wasanii wanaonunua views youtube ili ionekana nyimbo zao zinabamba. Hapa ni kama alikuwa analengwa Diamond na timu yake. Lakini hili ni kama watu hawajalielewa kwa maana kwamba Ommy hajaeleweka. Sasa Darasa anawaona watu wasioelewa hili ni kama machizi vile. Anamwambia Ommy na teamkiba, “Kumuelewesha chizi utajipa kazi.” Anaendelea kuwaambia wasanii kupata views nyingi wafunge mkanda, wakaze kamba, kwa maana ya kutoa ngoma kali. Au wafuate nyao za kununua views waone kama hawajachana msamba (kupotea kwenye game) kama asemavyo:

 Funga mkanda na kaza kamba,
Ama ufuate nyayo uchane msamba.

10.  Mwisho anazigeukia media na watu wanaotaka kuipoteza Hip Hip na wasanii wake. Anawambia:
Wanataka tupotee kwenye map,
tunapeleka game to the top top…
We don’t stop.

Huu ni mtazamo tu...inaweza kuwa si kweli
Mwl. Venance
0715 335558 (whatsapp) 
follow me instagram @fullraha17

No comments:

Post a Comment