Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Friday, June 28, 2013

MSANII ROMA: HUU NDIO MSOTO NILIOPITIA KABLA YA KUTOKA KIMUZIKI

 
1.MWAKA 2006 nikiwa tanga nilitoroka shule asubuhi nikamfukuzia Mtangazaji wa Clouds Fm ya jiji Dar es Salaam, Hamis Mandi 'B-12' aliyekuja Tanga nadhani kwenye show ya Park Lane!! am not sure, nikamkuta ameshapanda basi na anataka kuondoka ikanibidi nikadandia basi na mimi na kuanza kumtafuta miongoni mwa abiria, kipindi hiyo hata simjui kwa sura nikasema atakayekuwa brazameni tu humu ndani ndio yeye, huku basi linaenda niligonganishana naye macho akasmile nami nikasmile, nikamfata ikamkabidhi cd ikiwa na nyimbo zangu 2 nilizirekodi kwa marehemu Mr. Ebbo zamani sana Motika Record!!! MUNGU AMREHEMU!! "Braza ngoma zangu hizi samahani naomba kanipigie zipo poa sana na Tanga zimekubalika mno samahani sana kanipigie", akawa ananisisitiza poa zimefika kama kali zitapigwa, we shuka uwahi shule maana basi linazidi kwenda, nikashukia
majani mapana kule kutokea standi!!!
 

Hazikupigwa zile ngoma na msoto ukaendelea kama kawa!! nadhani hazikuwa na kiwango bora au mimi sikuwa mkali!!!! 
 
2. MWAKA 2007 nilirecord nyimbo yangu ya kwanza SALUTE kwa producer Abbuy wa Tanga, studio za GOMBA RECORD, sasa wakati naipeleka Dar kwenye vituo vya redio nikakutana tena na B-12, akaniunganisha kwa Dj Nelly ambae alikuwa mjengoni kipindi hicho kama mmoja wa watu waliokuwa wanafanya kitengo cha muziki pale Clouds Fm.
 
 
Basi nikafika mjengoni kitega uchumi pale mchana mapema nimeambiwa nifike saa kumi mimi nimefika saa tisa, adabu za kale mbele hapo, kufika nje nikamwambia mlinzi nataka kumuona B-12 nina ahadi naye, daah nilipewa mkwara, nikaambiwa nikamngoje chini. Sijakaa sawa mara bwana Matonya naona anapita pale na anaingia ndani bila bugudha kwa mlinzi, kidogo tena nikamuona A.Y naye akapita bila kuulizwa lolote, daaah moyoni nikawa natukana kimoyomoyo. Baadae B-12 akatoka akanipeleka hadi kwa Dj Nelly, ilikuwa kama oyaa Dj Nelly msikilize huyo mdogo wangu...dah jamaa akawa kama hasikii vile apo nimesimama na kacd kangu pembeni nashangaa tu kumbe huyu ndiyo Gadner na huyu ndiyo P.J okey hapo Jahazi ndiyo linataka kuanza.
 
Dj Nelly akaanza kusema 'oya sema shida yako?' nikajibu aaah braza mimi naitwa Ro....akanikatisha haraka na kuniambia nina dakika 2 tu za kuongea naye, kisha akachukua CD akaiweka kwenye machine vile inaanza tu akaisimamisha hakuicheza tena, na hapo yani kaisikiliza nyimbo ndani ya sekunde 15 au 20 akaitoa CD na kunijibu hamna kitu Production mbovu na huwezi kuchana!!! kisha akamgeukia Gadna na kuendelea na hadithia zao, mimi nikamuuliza sasa braza nishauri nifanyaje? Oyaa dogo tuna maongezi hapa huoni!!? hatuwezi kupiga nyimbo kama hiyo akanijibu kwa ukali...dah nikakosa pozi nikaanza kusepa, huku moyoni najisemea, aah wewe Gadna si ni Mtanga mwenzangu wewe hata hutii neno kaka?.
 
Nikamfata B-12 wangu maana ndiyo alikuwa kimbilio langu mjini hapa, naye hakuwa na jinsi wal anamna ya kufanya maana hawezi kupiga nyimbo kama kitengo cha muziki hakujaruhusu, akanishauri nikairudie nyimbo ile kwa Dunga...kipindi hiyo Dunga alikuwa ndiyo gumzo.
 
 
Hivyo nikatoka pale nikaipeleka ngoma ile ile East Africa Radio nikaiandikisha na nikasepa hapo nauli inaelekea kuliwa, babaako nikalirudisha kunani Tanga moja. Aaah! East Africa Radio bana wakanipigia simu na kusema nyimbo yako tunaitambulisha leo na wana segment inaitwa ipotezewe au iendelee kuwepo kitu kama hicho... basi nikiwa Tanga nikatega sikio kwenye satelite kusikiza baadae wakaipiga na ikapata kura 338 zikisema iendelee kuwepo na kura 34 zikisema ipotezewe nakumbuka hadi leo hiyo!!! basi nyimbo yangu ikapita na ikawa inapigwa pigwa east East Africa Radio.
 
Wakati huo huo samahani kabla sijaenda Tanga, nikiwa Dar nilikutana na Jaffarai alikuwa ni rafiki wa karibu wa braza yangu, braza akanitambulisha "Huyu mdogo wangu anaitwa Ebra au ROMA anarap na kaleta nyimbo yake"... hapo natamani jamaa aseme tuisikize... (si unajua zile ukiwa unajiamini na nyimbo ni nzuri) basi tukamshawishi aisikize, basi tukaenda kwenye gari na akaiweka. Uwiiiiiiii! Jafarai akaanza "Aaah mbona anachana kama mwana FA? aaah! hana style yake huyu babu, tafuta style yako mzee, game gumu mzee, njoo kivyako man", sasa nikawa najiuliza nachana vipi kama Mwana FA? mh! nikaona ananikata tu nikamchana braza tuondoke bwana naona navurugwa tu. Tukaaga tukaondoka kinyonge!! 
 
3. MWAKA 2008 nimeshajichanga nipo safi ndiyonakuja Dar rasmi sasa kurekodi TANZANIA haponimeshaongea na Nahreal, na pia nakuja kuirudia ile ngoma iliyokataliwa radio nakuja kuirudia kwa Dunga. Ndipo hapo tukiwa na braza mitaa ya mikocheni nadhani. Ndio tunakutana na Fid Q, Jafarrai na Mussa Hussein wa uswazi yule, tukafika na kaka hadi pale tukasalimia pale ila si unajua kisanii mara nyingi ukimsalimia mtu ni kama anakuwa anakukataa hivi anaitikia short short ndivyo ilivyokuwa.
 
 
Sasa kaka akaanza kuongea na Jafarai mambo yao tu aaah! katikati ndiyo  wakachomekea kaka akamwambia Jaffarai "Aah! tunaenda 41 Record kwa Dunga nampeleka mdogo wangu huyu si unamkubuka"?? Jafarai akajibu aaah! huyu si yule wa kipindi kileee? hapo ujue mwaka umeshapita hapo, kaka akamjibu ndiyo huyu sasa amekuja kuirudia ile ngoma huku kwa Dunga!! Jafarai akasema aaah amebadilika? au bado anachana vile vile? dogo badilika aisee! game gumu sana dogo kwa style ile unapoteza hela tu huwezi kutoka, sasa akaanza kunivuruga tena ila moyoni nikawa nasema " Mbona Fid Q haununui huu ugomvi? yani kwanini haulizi lolote daah! hapo Fid Q kajikausha hata hatusikilizi yani yeye busy wanaongea na Mussa tu, mimi nikawa natamani kaka aseme kitu tu.
 
Hatimaye Fid Q akaingilia "Oya kwani vipi babu? mbona kama unamnyea sana jamaa"? akamuuliza Jafarai? Jafarai akajibu "Aah! huyu dogo alikuja huku kama mwaka umepita hivi, akaniletea nyimbo yake, ila ni ya kiwaki!! sasa kaenda kujipanga na sasa karudi rasmi... Fid akasema niaje babu? unaimba au unarap? nikamwambia narap!! akasema ok 1,2,3 twendee... mamamammama ndiyo nilichokisubiri kwa muda mrefu hiki. Nikaanza kuchana nyimbo ile iliyokataliwa radioni na iliyopingwa na Jafarai... sasa kadri ninavyozidi kuchana naona jinsi bwana Kubanda anavyozidi kunogewa, namimi naongeza misifa hapo nachana tuu kwa hisia. Ikawa poa sana kwake na akakubali hadi kuamka kwenye kiti na kunipongeza kuwa am good, lakini moyoni nikawa nataka nimchanie TANZANIA maana ndiyo nimekuja kuirekodi na ndiyo nina mzuka nayo na ndiyo naiona ni nyimbo kali, yani zile za (kama kadata nahii tu je Tanzania nikichana itakuwaje)?
sasa nikamwambia ngoja nikuchanie nyingine... akakataa akasema aaah! mimi sitaki nyingine, nichanie hii hii iliyokataliwa. Sasa nikapita nayo tena. Sasa ujuee na nyimbo hiyo ninayochana hapa ndiyo baadhi ya mashairi yake yamepita tena kwenye MATHEMATICS na MECHI ZA UGENINI... niliyarudia kwa vile sikutaka yapotee bure vitu kama "Ndoto zangu kitambo zilikuwa nije kuwa padre, zikayeyuka nilipopuliziwa moshi wa weed etc. Basi Fid Q alikubali sana na hapo ndipo akasema una IQ sana bab...ndio chanzo cha ule mstari wa kusema
 

"Nawazidi kwa IQ shahidi Fareed Kubanda"! ambapo tazama sasa nimeuimba kwenye ngoma ya 4 toka niambiwe hivyo na yeye. Basi alikubali sana na akasema ni bora nikarudie kwa Macko Chali na akawa anampigia simu sema Marco hakupatikana akaniachia namba yake, sasa Jafarai na yeye alipoona Fid Q anakubali akawa na yeye anasema aah! dogo sasa amebadilika sasa hahaha! moyoni nikawa na furaha sana unajua inavyokuwa unakubaliwa na watu kama hawa kwa kipindi hicho u konw it!! nikaondoka na kaka tukawaacha majamaa, nikaendelea na hasso za kurekodi kwa Dunga na Nahreal!!! 
 
HIZO NI BAADHI ZA MICHONGO ILIYOHAPPEN KABLA HAIJATOKA WALA KUREKODIWA NGOMA YA KWANZA YANGU ILIYONITAMBULISHA "tanzania" 4. BASI YAPO MENGI SANA YANAJAA KITABU NADHANI NA MENGI NI YA KUSISIMUA. NATAMANI NIPATE INTERVIEW TENA YA TV HARAFU NIHADITHIE KWA SAA MOJA NA ZAIDI YOTE HAYA. SEMA YOTE HAYA UTAYAPATA KWENYE 
 
"DOCUMENTARY YA ROMA 2030" KUANZIA NAZALIWA HADI HAPA NILIPO SASA. (UZURI NI KUWA KUNA BAADHI YALIREKODIWA SO ITAKUWA IPO REAL SANA). TUENDELEE KUNGOJA!!! NAJUA MNAENJOY NIKIFUNGUKA HIVI YAPO MENGI KAMA;

1. Mimi kukutana na kala na kugonganisha
mawazo ya wimbo wa Tanzania na wa kwake wa
wimbo wa Taifa. 
2.Nakaaya kunizingua kwenye kumshirikisha katika ngoma yangu ya Tanzania, ila badae alinitafuta na kuniomba kolabo baada ya kutoka Mathematics.
 
 3. Wasanii wakubwa kunikatalia kwenye kolabo zangu kama Mr.President na Tanzania, ndiyo maana nasimama bila kumshirikisha mtu kiivyo.
 4. Nikki wa Pili alisababisha nikarekodi mechi za ugenini though yeye hajui hili. 
 
5. Nilivyoingia kwa Duke M. LAB na kurekodi Mr. President lakini haikutoka, na mimi nikahamia Tongwe na kuanza kurekodi upya hadi leo nipo Tongwe.
 6. Nilihit sana na Tanzania lakini Jay MO aliwahi kuniambia hanifahamu... ila siku zikaenda akaja akanifahamu na tukafanya naye MVUA NA JUA REMIX kwa majani. 
 
7. Kwanini wadau wengi wakati natoka na Tanzania hadi Mr. President walinambia THAT IS HIP HOP!!! safi kaza mwana harafu leo inatoka hit kama Mathematics wanasema sifanyi hip hop!! napayuka!! naropoka!! napiga makelele!! sina stye!! na mengi tu hadi kusema tuzo sikustahili.... duuuh! HATARI AISEE! 
8... NYIMBO YANGU YA TANZANIA ILIVYOKATALIWA NA RADIO STATIONS NYINGI, ADAM MCHOMVU ALIKUWA MBISHI SANA THANKS GOD AKAIPITISHA NA RADIO ZA MIKOANI ZIKASSUPORT MNO!! .
.9.......10..... Nawapenda sana watu wangu kuna vita kubwa sana dhidi yetu basi katika sala zenu msinisahau kuniombea niwe na afya njema na maisha yenye heri na baraka na marefu mimi na familia yangu na Tongwe wote na ndugu jama na marafiki wote!!!.
 
 
Chanzo : hi255.blogspot.

No comments:

Post a Comment