Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Saturday, January 11, 2014

HUU NDO WASIFU WA ARIEL SHARON

Ariel Sharon alikuwa mtu asiyejali,mwenye aina ya ukaidi,asiyejali nani anayempenda wala anayemchukia iwe ni Waisrael au Waarabu.

Malengo ya kwanza ya mwanajeshi huyu mstaafu na veterani wa siasa ilikuwa ni kuhakikisha kwanza usalama wa Israel kwa vile alivyoamini.
Sharon hakujali chochote kwa wale wasioamini.
Ndio maana alihakikisha ardhi kubwa na haki ya kisiasa inasalia kwa Waisrael na kutoa nafasi ndogo kwa Wapelestina.
Bwana Sharon alizaliwa nchini Palestina mwaka 1928,ilipokuwa chini ya utawala wa Kiingereza.
Akiwa kijana mdogo alijiunga na kitengo cha jeshi la chini kwa chini la Wayahudi la Haganah na kupigana katika vita vya Israel na Waarabu mwaka 1948-49 baada ya kuundwa kwa taifa la Wayahudi.
Kwenye miaka ya 1950 aliongoza oparesheni kali ya kijeshi dhidi ya kituo cha jeshi la Misri kilichopo kwenye ukanda wa Gaza,katika tukio moja la mwaka 1955 wanajeshi wa misri 38 waliuwawa.
Bwana Sharon alipanda kicheo kutoka brigedia hadi jenerali na kamanda wa kikosi cha jeshi kwenye vita vya siku sita vya mwezi Juni mwaka 1967 ambapo Israel iliuteka ukanda wa Mashariki wa mji wa Jerusalem,Ukindo wa Magharibi na ukanda wa Gaza.

Uny'ang'anyi huo wa nguvu uliofanywa na jeshi la Wayahudi ilizidisha chuki ya Wapalestina kwa mtu ambaye alikuwa adui yao mkubwa.

Alichaguliwa kwa mara ya kwanza kwenye bunge la Israel lijulikanalo kama Knesset mwaka 1973,lakini akajiuzulu mwaka mmoja baadaye ili kutumikia nafasi kama mshauri wa usalama wa aliyekuwa waziri mkuu wa tano wa taifa la Israel bwana Yitzhak Rabin.
Alichaguliwa tena kwenye bunge la Israel mwaka 1977.
Bwana Sharon alikuwa kinara wa uvamizi wa Israel nchini Lebanon mwaka 1982.
Akiwa kama waziri wa ulinzi na bila kumueleza Waziri Mkuu Menachem Begin alituma vikosi vya jeshi la Israel kwenda mjini Beirut,uvamizi ambao ulimaliza na kufukuza chama cha ukombozi cha Palestina kilichokuwa kikiongozwa na Yasser Arafat cha Palestine Liberation Organisation (PLO) kutoka nchini Lebanon.
Uvamizi huo ulisimamisha mashambulizi yaliyokuwa yakifanywa na PLO kupitia nchini Lebanon kuipiga Israel na pia ilisababisha uteswaji mkubwa wa mamia ya Wapelestina kutoka kwa wapiganaji wakristo kutoka Lebaanon chini ya amri ya wanajeshi wa kiyahudi kwenye kambi ya wakimbizi.
Bwana Sharon aliondolewa madarakani mwaka 1983 na mahakama ya Israel ya uchunguzi ya uvamizi wa mwaka 1982 nchini Lebanon, ambapo ilimkuta na makosa kutohusika moja kwa moja na mauaji.
Kwa wanasiasa wengi na wale waliokuwa na mtazamo kama wake huo ndio ulikuwa mwisho wake wa kisiasa.
Lakini kwa bwana Sharon alisalia kiongozi maarufu wa Wayahudi wenye mrengo wa kulia na kuwa imani kwamba muda ungalipo na nafasi nyingine itajitokeza tu.
Ariel Sharon malengo yake ambayo maadui zake waliyaita ya hatari na yenye kukandamiza, ilikuwa ni kupigania hali ya usalama wa ulinzi wa Israel, alimini daima kwamba mwisho hilo lingekuwa suluhisho la haki.
Akiwa waziri wa nyumba kwenye miaka ya 1990,alisimamia na kuongoza ujenzi mkubwa majengo ya wayahudi kwenye Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza tangu Israel iyachukue maeneo hayo kwenye vita vya siku sita.
Baada ya Chama chenye mrengo wa kulia cha Benjamini Netanyahu kuchukua madaraka mwaka 1996, Waziri mkuu mpya wa Israel alitia chagizo kumweka jenerali huyo wa zamani wa jeshi kwenye baraza lake la mawaziri.
Wakati alipomchagua kama Waziri wa mambo ya nje mwaka 1998, Bwana Netanyahu alisema Ariel Sharon alikuwa mtu sahihi kwa nafasi hiyo.
Meja Jenerali wa jeshi la Israel, Ariel Sharon(aliyeko kushoto mbele) akiwa ndani ya gari ya kijeshi aina ya Jeep mwezi October mwaka 1973. Picha na Wizara ya Ulinzi ya Israel.

" Hatutakiwi kufikiria yaliyopita" alisema. " ana rekodi katika maisha yake yote ya kutumikia uma na katika miaka 15 iliyopita watu wanatakiwa kujivunia naye."

Bwana Sharon alichaguliwa kuwa kiongozi wa chama wa mrengo wa kulia cha Likud kilichokuja kuwa chama cha Upinzani baada ya anguko kubwa la Netanyahu kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 1999.
Baada ya kushindikana kwa mapatano kwenye mkutano wa amani ya Palestina na Israel ujulikanao kama Camp David mwaka 2001,bwana Sharon alipigania tena kurejea kwenye ofisi za uma akimpinga waziri mkuu wa wakati huo Ehud Barak,huku akimtuhumu kwa kuwa tayari kuiuza Jerusalem kwaajili ya mapatano ya amani.

" Barak hana haki ya kukata tamaa juu ya Jerusalem,ambayo watu walipokea kama urithi," Bwana Sharon alisema kwenye mojawapo ya vikao vya bunge.

Ziara yake yenye utata mwaka 2000 kwenye msikiti wa Al Aqsa mashariki mwa Jerusalem, eneo ambalo pia ni eneo takatifu kwa Wayahudi,ilikuwa ni kutonesha kidonda kwa mara ya pili kwa kuamsha vuguvugu la Wapelestina.
Wasioamini wanasema bwana Sharon alijuwa fika kuwa ziara yake hiyo ingeleta vurugu na alifanya hivyo kwa makusudi ili kuwaonyesha Wayahudi kuwa kiongozi kama yeye ndiye atakayeweza kumudu hali hiyo.
Lakini kwa mara nyingine tena, bwana Sharon hakuwahi kusikia wala hakujali wasioamini walimweleza nini.
Katika nyakati fulani kwenye mikutano ya kampeni za uchaguzi mkuu aliwahi kusema anajiandaa kufanya mazungumzo na kuingia makubaliano ya amani na Waarabu lakini sio chini ya vitisho.
Licha ya yote alikuwa tayari kufanya lolote ili kuondoa hali ya uonevu utakao ondoa "haki ya Wayahudi kuishi kwa amani kwenye ardhi yao"
Ariel Sharon malengo yake ambayo maadui zake waliyaita ya hatari na yenye kukandamiza, ilikuwa ni kupigania hali ya usalama wa ulinzi wa Israel, alimini daima kwamba mwisho hilo lingekuwa suluhisho la haki.
 
Via BBC Swahili

No comments:

Post a Comment