Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Sunday, January 12, 2014

WAKATI STEVEN WASIRA AKIITABIRIA KIFO CHADEMA, MWANAE MWINGINE AJIUNGA CHADEMA

MAGAMBO Wassira ambaye ni mtoto wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mahusiano na Utaratibu, Steven Wassira, amejiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
 
 
Akizungumza na Tanzania Daima jana, Magambo alisema hawezi kumfuata baba yake kujiunga na CCM, kwani hayo ni maono yake mwenyewe.
 
 
Magambo ambaye pia ni mgombea wa udiwani katika Kata ya Nyasura, wilayani Bunda, alisema anamuheshimu Wassira kwani ni baba yake mkubwa, lakini hawezi kumfuata kiitikadi.
 
 
Alisema haki pekee inapatikana kwa CHADEMA na kueleza kuwa akishinda amejipanga kuhakikisha uchaguzi mkuu wa mwakani Jimbo la Bunda linapata mbunge wa CHADEMA.
“Mambo ya kifamilia ni ya kifamilia, baba Wassira yeye ameona awe CCM, lakini mtazamo wangu na wake ni tofauti, mimi naona CCM hainitendei haki.
 
 
“Suluhisho la Watanzania ni CHADEMA pekee na ukombozi wa kweli utapatikana kupitia chama hicho kwani si kandamizi,” alisema Magambo.
Uchaguzi mdogo wa madiwani unatarajiwa kufanyika Februari 9 katika kata 27 nchini

Via: Tanzania Daima

No comments:

Post a Comment