Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Sunday, January 12, 2014

MBUNGE WA MOSHI VIJIJINI, MH. CYRIL CHAMI BAADA YA KU AWAITA WENZAKE WANAOSHABIKIA MGOGORO WA CHADEMA SAWA NA MALAYA, LEO ADAI KUWA KINACHOENDELEA NDANI YA CCM NI BALAA KULIKO HILI LINALOENDELEA NDANI YA CHADEMA, UNAJUA NI NINI KINACHOENDELEA CCM? SOMA HAPA

Mbunge wa Moshi Vijijini Mh. Cyril Chami, ambaye pia aliwahi kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara katika serikali hii ya awamu ya nne kuwafananisha wanachama wenzake wa CCM wanaoshabikia mgogoro uliopo ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo [CHADEMA] sawa na Malaya kupitia ukurasa wake wa facebook siku ya ijumaa, leo akiendelea na kuuangazia mgogoro ndani ya cha hicho na kile kinachoendelea ndani ndani ya chama chake CCM, post zote hizi hapa chini:
Cyril ChamiCyril Chami
.... Hii tabia ya wana CCM wenzangu kushangilia wazi wazi mgogoro tata unaoendelea kati ya Mhe. Zitto Kabwe na CHADEMA sijaupenda na wala hauna maana ktk maendeleo ya demokrasia nchini. Maana ya kuwa kwenye mfumo wa vyama vingi ni pamoja na kutokuwa mwanachama wa vyama vingi... Wanachama wa CCM wanaoshabikia suala hili nawaita (Kwa jina baya) kuwa ni sawa na Malaya wa kisiasa.
                                           Nawaomba radhi kwa kutumia maneno makali kwa leo.

Leo ameandika tena hivi:
 
 
 
 
 
.....................Kinachoendelea ndani ya chama changu (CCM) Juu ya Urais 2015 ni hatari kubwa kuliko kinachoendelea CHADEMA na MheZitto Kabwe. Wana CCM tuwe makini.

No comments:

Post a Comment