Adai hajazuia shuhulizi za kisiasa
Aonya watakaoandamana septemba 1 kukiona
Safari ya Makao Makuu Dodoma, nyumba za serikali Dar kupigwa mnada
Na. Furaha Venance: Manyoni-Singida
Katika muendelezo wa kuhakikisha
utawala wake unakuwa wa
Hapa Kazi Tu,
rais, Dkt. John Pombe Magufuli amewaonya wanasiasa wanaohamasisha maandamo nchi
nzima.
Amemtaka Mwenyekiti taifa wa Chadema ambaye pia ni mbunge wa Hai kama
anataka kuandamanisha watu akawaandamishe watu wa jimboni kwake.
“Na wapo wengine ambao wanapenda maandamano tu. Na saa nyingine wengine
watasema wamezibwa kuzungumza, wakati walipoziba midomo tuliwaruhusu,
walipozungumza juzi kuwa watafanya maandamano tumewaangalia. Nchi ni mbili tu,
ambazo baada ya uchaguzi watu wanaendelea kufanya kampeni, ni nchi ya Tanzania
na Kenya, wakimaliza uchaguzi leo kesho wanaanza kampeni, kampeni zitaisha lini?”
…ninafahamu katika maeneo hapa tuna wabunge, wabunge wanaruhusiwa
kufanya mikutano yao, kwenye maeneo yao, bila kuwa na wasiwasi..kwa hiyo kama
uko mbunge wa chadema, uko kwenye jimbo lako la Hai, zunguka hai mpaka uchoke,
fanya mikutano katika kila kijiji, kila kata..siyo uliache jimbo lako la Hai
uende Shinyanga ukaanze kuwaambia waandamane wakati Hai hawataki kuandamana. Kawaandamanishe
wa Hai hata usiku na mchana wawe wanaandamana. Wanazunguka ili wakati
tutakapokuwa tunavuna wawe wanaandama.”
Sijazuia shughuli za siasa,ila watakaoandama kukiona cha mtema kuni
Rais amewataka wanasiasa waache
wabunge katika majimbo yao wafanye kazi, watekeleze yale waliyoyaahidi
kuyafanya.
“Ni lazima muelewe sijazuia shughuli
za siasa za watu waliochaguliwa, lakini sitaki nchi hii iwe nchi ya vurugu. Watakaoleta
vurugu mimi nitawashughulikia kikamilifu bila huruma. Na wasije wakanijaribu,
mimi ni watofauti sana na kama wapo watu wanaowatumia wakawaeleze vizuri, mimi
sijaribiwi na wala sitajaribiwa…tunataka nchi hii enede mbele…na mimi sitaki
mtu yoyote anicheleweshe. Nataka hao wanaotetea maandamano watangulie wao alafu
wataona cha mtema kuni. Na mimi nataka watangulie wao hiyo tarehe waliyoipanga.”
Alisema rais Magufuli kwa sauti kali na ya kujiamini kuashiria kwamba hatanii
na hayuko tayari kuona maandamano hayo.
Ikumbukwe Chadema imetangaza kuwa
kuanzia Septemba mosi mwaka huu itakuwa ni siku ya maandamano na mikutano ya
hadhara nchi nzima kupitia kinachoitwa Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania
(UKUTA). Iliyotangazwa na mwenyeketi wa chama hichO taifa, Freeman Mbowe.
Aviponda vyama vya upinzani
Katika hatua nyingine alitumia
mkutano huo kuviponda vyama vya upinzani na kuvifananisha na nyoka aliyejifia
huku akitingisha mkia.
“Lakini najua saa zingine unajua ukikutana na nyoka ukimpiga ukamua,
mkia lazima atingishe, unaweza kufikiri ni mzima kumbe nyoka ameshakufa, vyam
vyenyewe vimechoka…wananchi wameshaona.” Wakati huo huo Rais ameahidi
hatawabugua wananchi kwa itikadi za vyama vya siasa atawatumikia wananchi wote
bila ya upendeleo.
Akerwa na kodi kandamizi kwa wananchi
Rais alionekana kukerwa na kodi
wanazotozwa wananchi na halmshauri zao na kuzitaka halmashauri husika kukaa na
kuziangalia namna ya kuziondoa kodi hizo, “Katika
kipindi changu ninapenda kodi lakini si kodi za kwa watu wanyonge, si kodi kwa
watu masikini. Kodi ambazo zinazowanyanyasa wananchi tuzitoe.” Alisema.
Ashikilia msimamo wa makao makuu kuhamia Dodoma,
Nyumba za serikali Dar es salaam kupigwa mnada
Watakaoshindwa kuhamia Dodoma kukiona
Rais magufuli ameshikilia msimamo
wake wa kuhamia Dodoma. Awashangaa wanaokosoa msimamo huo wakidai kuwa
Dodoma miondo mbinu haijakamilika. Katika
kuwatoa hofu wananchi Rais amesema miundo mbinu ya imekalika zikiwemo barabara
zinazounganisha Dodoma na mikoa mingine, uwanja wa ndege wa kisasa umekamilika
na reli ya kisasa itaanza kujengwa mwaka huu.
Katika kuhakikisha hakuna
kiongozi wa serikali yake anabaki Dar es salaam, atapiga mnada nyumba zote za
serikali zilizo jijini humo na kiongozi atakayebaki huko baada ya yeye kuhamia
Dodoma ajue hana kazi.
“Na nataka niwaeleze mara baada ya kuhamia mimi pale yale majengo yote
yaliyo Dar es salaam nitayapiga mnada…fedha zile ninazileta Dodoma kwa ajili ya
kujenga majengo ya serikali. Na nikishahamia huku yeye bado yuko kuleatabaki
kule hana kazi na mshara hamna…ni nchi gani hii ambayo mnatoa maamuzi ya miaka
50 hamtaki kutekeleza, Baba wa taifa alizungumza mpaka ametangulia mbele ya haki
sisi hatutekelezi, si mimi. Mimi watahama, watahama na wasiohama wajiandae
kuacha kazi…” Alisema.
Amani ya nchi
Amedai kuwa amani ya Tanzania wapo
wanaoionea wivu. Alizitolea mfano nchi za Libya, Iraq, Siria na Somalia ambazo
zilikuwa nchi za amani lakini baada ya kuchonganishwa na kuanza kupigana wao
kwa wao sasa nchi hizo hazina amani tena.
Kuhusu demokrasia alisema demokrasia
ya Tanzania inatosha, isimamiwe,ilindwe ili watu waishi kwa amani na kuleta mabadiko
katika nchi yao. Aidha liwataka Watanzania kusimama imara kudumisha amani. “Mabeberu wanaimezea mate rasilimali za
Tanzania. Naomba msimame imara, Amani hii tulinde na tutafika kwa ajili ya Tanzania
mpya.” Alisema Rais Magufuli.
Rais Magufuli alitumia
mkutano huo kuwaleza wananchi kuwa mpaka sasa zaidi ya watumishi hewa 12,500
wamebainika na kuondolewa ambao walikuwa wakilipwa mabilioni ya pesa.
Amewataka
vijana kujituma kwa kufanya kazi ili wajiletee maendeleo “Nawaomba vijana wajue vya bure vimekwisha. Kila
mmoja afanye kazi, dhamira yetu ni maisha mazuri kwa Watanzania.” Alisema Magufuli
huku akishangiliwa na wananchi wengi waliofurika katika viwanja vya shule ya
msingi Tambukareli wilayani hapa.
Wabunge waomba
Mbunge wa Manyoni Mashariki,
Daniel Mtuka aomba gari la zima moto, maji na utatuzi wa migogoro ya ardhi
wakati mbunge wa Manyoni Magharibi Yahaya Masale aliomba wilaya mpya ya Itigi.
Wananchi walitarajia majipu kutumbuliwa
Katika hali isiyokuwa ya kawaida
wananchi wengi walitegemea katika mkutano huu majipu yatatumbuliwa. Mara baada
ya mkutano mwandishi alitembelea vikundi mbalimbali vilivyokusanyika na
kujadiliana yaliyojili katika mkutano huo. Wengi walidhani kwamba rais
angetumia mkutano huo
kutumbua majipu. Inagwa katika mijadala hiyo wengine waliona
kuwa hakukuwa na haja ya rais kutumbua majipu wakati karibia viongozi wote wa
wilaya kuanzia Mkuu wa Wilaya, Wakurugenzi hadi Madas ni wageni hivyo wanaona majipu
tayari yalishatumbuliwa.
Kusikiliza sauti bofya
HAPA