Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Sunday, July 31, 2016

Kufukuzwa kazi kwa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Azimina Mbilinyi. LISSU aandika haya

By Tundu Lissu
Kufukuzwa kazi kwa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Azimina Mbilinyi (pichani) ni dirisha lingine la kuangalia the inner workings za Tanzania ya Magufuli.

Azimina Mbilinyi alikuwa Mkurugenzi mtiifu wa maCCM wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana. Aliwasaidia kwa mambo mengi wakati wa kampeni, ikiwemo kuwapa pesa na mafuta kwa ajili ya kampeni zao. Kilichomshinda ni kuwashindisha uchaguzi wa wabunge wa majimbo yote mawili ya Wilaya ya Kilombero, yaani Kilombero na Mlimba.

Nguvu ya CHADEMA katika Bonde la Kilombero ilikuwa kubwa sana na kungekuwa na maafa makubwa kama angelazimisha kunyang'anya ushindi wa CHADEMA. Baadae maCCM walifungua kesi za uchaguzi kupinga matokeo ya Kilombero na Mlimba. Kama Msimamizi wa Uchaguzi, Azimina Mbilinyi alishtakiwa pia. Kwa sababu hiyo, alilazimika kuja Ifakara kutoa ushahidi kuhusu tuhuma dhidi yake na dhidi ya wagombea wa CHADEMA aliowatangaza washindi.

Mimi nilikuwa wakili wa Ambrose Juakali na nilishuhudia ushahidi wa Mama Mbilinyi na pia nilimhoji kwa kirefu sana. Ushahidi wake haukuacha chembe yoyote ya shaka kwamba kesi ile ilikuwa ni ya vihoja vya kuokoteza tu. Ushahidi huo ulikuwa msumari wa mwisho kwenye jeneza la kesi hiyo.
Jana Jaji Rugazia ameifutilia mbali kesi hiyo na leo Azimina Mbilinyi amefukuzwa kazi kwa 'utendaji usioridhisha.

'Ikumbukwe kwamba kabla ya kupelekwa Bagamoyo mama huyu alikuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma alikopelekwa akitokea Kilombero. Amekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri tangu mwaka 2012. Ana shahada ya MBA in Corporate Management na Advanced Diploma in Public Administration. Kwa kumfukuza kazi mama huyu, Magufuli anatuma ujumbe kwa Wakurugenzi wengine wote aliowateua majuzi: tumieni kila hila kuhakikisha CCM inashinda uchaguzi hata kama wapiga kura hawataki. Ikitokea kuna kesi inayotuhusu mahakamani, toeni ushahidi wa uongo ikibidi ilimradi wagombea wa CCM washinde. Msipofanya hivyo Magufuli atawatumbueni majipu na kuwadhalilisha hadharani.

Endapo watamsikiliza na kufanya anavyotaka Magufuli, wasimamizi hawa wa Uchaguzi watasababisha maafa makubwa katika nchi yetu. Wakurugenzi wengi wameanza kutambua kwamba utiifu kwa maCCM hauna guarantee yoyote kwamba hautatumbuliwa jipu.

Na Magufuli anajua hilo. Ndio maana kati ya wateule wa ukurugenzi, wapo maCCM wengi waliokuwa wagombea wa Uchaguzi kwa niaba ya CCM. Licha ya Katiba kukataza, zaidi ya wateule 60 wapya ni maCCM na waligombea uchaguzi wa mwaka jana katika hatua mbali as awali. Watu hawa wanatakiwa uteuzi wao uhojiwe na utahojiwa mahakamani. Itakuwa suicidal kuruhusu Wakurugenzi wa aina wasimamie uchaguzi ujao."
TUNDU LISSU.

No comments:

Post a Comment