Kituo cha tiba asilia cha Foreplan kinachomilikiwa na Tabibu Juma Mwaka Juma (pichani) kimefungiwa na serikali kwa kukiuka masharti ya kibali alichopewa kwa kujitangaza kuwa anatoa tiba za kisasa badala ya matibabu ya asilia.
Akizungumza na Waandishi wa habari leo jijini Dar es salaamHayo yalisemwa jana na Mwenyekiti Wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala Dkt. Edmund Kayombo wakati akizungumza na waandishi wa habari jiji Dar es salaam. Amesema kuwa kituo hiko kimefutiwa usajili na hakiruhusiwi kutoa huduma za tiba asilia na Tiba mbadala kwa jamii kwa kutokidhi masharti ya usajili na kufanya kazi kinyume cha usajili wake.
Vituo vingine vilivyokumbwa na panga hilo ni pamoja na Tabibu Abdallah Mandai wa Mandai Herval Clinic na kituo cha Fadhaget Sanitarium Clinic kinachomilikiwa na tabibu Fadhil Kabujanja. Vituo vingine vilivyofungiwa kwa miezi sita kila kimoja ni tabibu Simon Rusigwa wa kituo cha Sigwa Herbal Clinic na Tabibu John Lupimo wa kituo cha Lupimo Sanitarium Clinic.
No comments:
Post a Comment