Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Friday, July 29, 2016

MAANDAMANO YA CHADEMA NCHI NZIMA HATI HATI, MAGUFULI ACHIMBA MKWARA MZITO


Adai hajazuia shuhulizi za kisiasa
Aonya watakaoandamana septemba 1 kukiona
Safari ya Makao Makuu Dodoma, nyumba za serikali Dar kupigwa mnada

Na. Furaha Venance: Manyoni-Singida
Katika muendelezo wa kuhakikisha utawala wake unakuwa wa Hapa Kazi Tu, rais, Dkt. John Pombe Magufuli amewaonya wanasiasa wanaohamasisha maandamo nchi nzima.

Amemtaka Mwenyekiti taifa wa Chadema ambaye pia ni mbunge wa Hai kama anataka kuandamanisha watu akawaandamishe watu wa jimboni kwake.

Na wapo wengine ambao wanapenda maandamano tu. Na saa nyingine wengine watasema wamezibwa kuzungumza, wakati walipoziba midomo tuliwaruhusu, walipozungumza juzi kuwa watafanya maandamano tumewaangalia. Nchi ni mbili tu, ambazo baada ya uchaguzi watu wanaendelea kufanya kampeni, ni nchi ya Tanzania na Kenya, wakimaliza uchaguzi leo kesho wanaanza kampeni, kampeni zitaisha lini?”

ninafahamu katika maeneo hapa tuna wabunge, wabunge wanaruhusiwa kufanya mikutano yao, kwenye maeneo yao, bila kuwa na wasiwasi..kwa hiyo kama uko mbunge wa chadema, uko kwenye jimbo lako la Hai, zunguka hai mpaka uchoke, fanya mikutano katika kila kijiji, kila kata..siyo uliache jimbo lako la Hai uende Shinyanga ukaanze kuwaambia waandamane wakati Hai hawataki kuandamana. Kawaandamanishe wa Hai hata usiku na mchana wawe wanaandamana. Wanazunguka ili wakati tutakapokuwa tunavuna wawe wanaandama.”

Sijazuia shughuli za siasa,ila watakaoandama kukiona cha mtema kuni
Rais amewataka wanasiasa waache wabunge katika majimbo yao wafanye kazi, watekeleze yale waliyoyaahidi kuyafanya.

Ni lazima muelewe sijazuia shughuli za siasa za watu waliochaguliwa, lakini sitaki nchi hii iwe nchi ya vurugu. Watakaoleta vurugu mimi nitawashughulikia kikamilifu bila huruma. Na wasije wakanijaribu, mimi ni watofauti sana na kama wapo watu wanaowatumia wakawaeleze vizuri, mimi sijaribiwi na wala sitajaribiwa…tunataka nchi hii enede mbele…na mimi sitaki mtu yoyote anicheleweshe. Nataka hao wanaotetea maandamano watangulie wao alafu wataona cha mtema kuni. Na mimi nataka watangulie wao hiyo tarehe waliyoipanga.” Alisema rais Magufuli kwa sauti kali na ya kujiamini kuashiria kwamba hatanii na hayuko tayari kuona maandamano hayo.

Ikumbukwe Chadema imetangaza kuwa kuanzia Septemba mosi mwaka huu itakuwa ni siku ya maandamano na mikutano ya hadhara nchi nzima kupitia kinachoitwa Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (UKUTA). Iliyotangazwa na mwenyeketi wa chama hichO taifa, Freeman Mbowe.

Aviponda vyama vya upinzani

Katika hatua nyingine alitumia mkutano huo kuviponda vyama vya upinzani na kuvifananisha na nyoka aliyejifia huku akitingisha mkia.

Lakini najua saa zingine unajua ukikutana na nyoka ukimpiga ukamua, mkia lazima atingishe, unaweza kufikiri ni mzima kumbe nyoka ameshakufa, vyam vyenyewe vimechoka…wananchi wameshaona.” Wakati huo huo Rais ameahidi hatawabugua wananchi kwa itikadi za vyama vya siasa atawatumikia wananchi wote bila ya upendeleo.

Akerwa na kodi kandamizi kwa wananchi

Rais alionekana kukerwa na kodi wanazotozwa wananchi na halmshauri zao na kuzitaka halmashauri husika kukaa na kuziangalia namna ya kuziondoa kodi hizo, “Katika kipindi changu ninapenda kodi lakini si kodi za kwa watu wanyonge, si kodi kwa watu masikini. Kodi ambazo zinazowanyanyasa wananchi tuzitoe.” Alisema.

Ashikilia msimamo wa makao makuu kuhamia Dodoma,
Nyumba za serikali Dar es salaam kupigwa mnada
Watakaoshindwa kuhamia Dodoma kukiona

Rais magufuli ameshikilia msimamo wake wa kuhamia Dodoma. Awashangaa wanaokosoa msimamo huo wakidai kuwa Dodoma  miondo mbinu haijakamilika. Katika kuwatoa hofu wananchi Rais amesema miundo mbinu ya imekalika zikiwemo barabara zinazounganisha Dodoma na mikoa mingine, uwanja wa ndege wa kisasa umekamilika na reli ya kisasa itaanza kujengwa mwaka huu.

Katika kuhakikisha hakuna kiongozi wa serikali yake anabaki Dar es salaam, atapiga mnada nyumba zote za serikali zilizo jijini humo na kiongozi atakayebaki huko baada ya yeye kuhamia Dodoma ajue hana kazi.

Na nataka niwaeleze mara baada ya kuhamia mimi pale yale majengo yote yaliyo Dar es salaam nitayapiga mnada…fedha zile ninazileta Dodoma kwa ajili ya kujenga majengo ya serikali. Na nikishahamia huku yeye bado yuko kuleatabaki kule hana kazi na mshara hamna…ni nchi gani hii ambayo mnatoa maamuzi ya miaka 50 hamtaki kutekeleza, Baba wa taifa alizungumza mpaka ametangulia mbele ya haki sisi hatutekelezi, si mimi. Mimi watahama, watahama na wasiohama wajiandae kuacha kazi…” Alisema.

Amani ya nchi
Amedai kuwa amani ya Tanzania wapo wanaoionea wivu. Alizitolea mfano nchi za Libya, Iraq, Siria na Somalia ambazo zilikuwa nchi za amani lakini baada ya kuchonganishwa na kuanza kupigana wao kwa wao sasa nchi hizo hazina amani tena.

Kuhusu demokrasia alisema demokrasia ya Tanzania inatosha, isimamiwe,ilindwe ili watu waishi kwa amani na kuleta mabadiko katika nchi yao. Aidha liwataka Watanzania kusimama imara kudumisha amani. “Mabeberu wanaimezea mate rasilimali za Tanzania. Naomba msimame imara, Amani hii tulinde na tutafika kwa ajili ya Tanzania mpya.” Alisema Rais Magufuli.

Rais Magufuli alitumia mkutano huo kuwaleza wananchi kuwa mpaka sasa zaidi ya watumishi hewa 12,500 wamebainika na kuondolewa ambao walikuwa wakilipwa mabilioni ya pesa.

Amewataka vijana kujituma kwa kufanya kazi ili wajiletee maendeleo “Nawaomba vijana wajue vya bure vimekwisha. Kila mmoja afanye kazi, dhamira yetu ni maisha mazuri kwa Watanzania.” Alisema Magufuli huku akishangiliwa na wananchi wengi waliofurika katika viwanja vya shule ya msingi Tambukareli wilayani hapa.

Wabunge waomba

Mbunge wa Manyoni Mashariki, Daniel Mtuka aomba gari la zima moto, maji na utatuzi wa migogoro ya ardhi wakati mbunge wa Manyoni Magharibi Yahaya Masale aliomba wilaya mpya ya Itigi.

Wananchi walitarajia majipu kutumbuliwa

Katika hali isiyokuwa ya kawaida wananchi wengi walitegemea katika mkutano huu majipu yatatumbuliwa. Mara baada ya mkutano mwandishi alitembelea vikundi mbalimbali vilivyokusanyika na kujadiliana yaliyojili katika mkutano huo. Wengi walidhani kwamba rais angetumia mkutano huo kutumbua majipu. Inagwa katika mijadala hiyo wengine waliona kuwa hakukuwa na haja ya rais kutumbua majipu wakati karibia viongozi wote wa wilaya kuanzia Mkuu wa Wilaya, Wakurugenzi hadi Madas ni wageni hivyo wanaona  majipu tayari yalishatumbuliwa.

Kusikiliza sauti bofya HAPA




No comments:

Post a Comment