Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Sunday, July 3, 2016

KAMATI YA HARUSI YATOA ZAWADI YA MADAWATI

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Jordan Lugimbana ameipongeza kamati iliyosimamia harusi ya bwana Richard na bibi Miriam kwa uamuzi aliouita wa kimiujiza wa kuchangia madawati 21 ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano inayolenga watoto wa shule zote nchini wasome katika mazingira bora.
Mheshimiwa Lugimbana alitoa pongezi hizo siku ya Ijumaa tarehe 2 Juni, 2016 wakati akipokea madawati hayo ofisini kwake Dodoma kutoka kwa wawakilishi wa kamati hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati bwana Philbert Rwakilomba.
"Niwapongeze sana kwa uamuzi huu amabao naweza kusema ni wa ki muujiza, pamoja na sherehe ya harusi mkaona kwamba sehemu ya pesa mhifadhi kwa ajili ya mchango kwa jamii, hongereni sana,"alisema Mhe. Lugimbana.
Alisema dhana ya Mhe.Rais John Pombe Magufuli ya kutaka watanzania wabadilike na kila mmoja atimize wajibu wake kuchangia nguvu, utaalamu ama fedha katika kuinua hali ya jamii na kuacha kufanya vitu kwa mazoea imeanza kufanya kazi. Aliipongeza kamati hiyo kwa kuwa ya kwanza kumuunga mkono Rais kwa kitendo chao cha kuchangia madawati kupitia harusi ya Richard na Miriam, jambo ambalo halijawahi kutokea.
Alisema dhana ya Mhe.Rais John Pombe Magufuli ya kutaka watanzania wabadilike na kila mmoja atimize wajibu wake kuchangia nguvu, utaalamu ama fedha katika kuinua hali ya jamii na kuacha kufanya vitu kwa mazoea imeanza kufanya kazi. Aliipongeza kamati hiyo kwa kuwa ya kwanza kumuunga mkono Rais kwa kitendo chao cha kuchangia madawati kupitia harusi ya Richard na Miriam, jambo ambalo halijawahi kutokea.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati iliyosimamia harusi hiyo ndugu Philbert Rwakilomba alisema kuwa waliamua kuchangia madawati hayo 21 yenye thamani ya shilingi milioni moja na laki sita ili kutoa mchango wao kwa jamii baada ya kuona bado kuna tatizo kubwa la wanafunzi kukaa chini hasa katika Mkoa wa Dodoma.
"Tunatambua jitihada zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kuhakikisha wanafunzi wote wanakaa kwenye madawati, lakini changamoto bado ni kubwa hivyo tumeona tuunge mkono jitihada hizi za Serikali kwa kutenga fedha amabazo pengine zingetumika katika kunywa na kula katika sherehe wakati watoto wa watanzania wenzetu wanateseka kwa kukaa chini madarasani," alisema Rwakilomba.
Aidha Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Harusi alitoa wazo kwa halmashauri nchini kuanzisha Sheria ndogo itayozifanya sherehe zote zitakazofanyika katika kumbi mbalimbali kutoa asilimia kidogo kuchangia mambo ya msingi katika jamii kama elimu, afya na mengineyo.
Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Chang'ombe 'B' bibi Asha Mafita aliyekabidhiwa madawati hayo kwa ajili ya shule yake, aliishukuru sana kamati hiyo kwa moyo wao wa upendo na kuwataka wadau wengine kuiga mfano wao.
"Kitendo kilichofanywa na kamati hii ni cha kupongezwa sana, tunashukuru kwa kuwa wamepunguza tatizo lililokuwa linatukabili. Shule yetu ina wanafunzi 595 na ina madawati 42 na upungufu wa madawati ni 192. Madawati haya 21 yaliyotolewa ni nusu ya yale tuliyokuwa nayo hivyo tunawashukuru sana, lakini bado tuna upungufu, tunaomba wadau wengine pia watuunge mkono," alisema Mwalimu Mkuu.
Bwana Richard Masesa ambaye ni mfanyakazi wa Ofisi ya Rais Tamisemi alifunga ndoa na bi Miriam Emmanuel siku ya Jumapili tarehe 29 Mei, 2016 na sherehe kufanyika katika ukumbi wa kilimani mjini Dodoma
Chanzo: TAMISEMI 

No comments:

Post a Comment