Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Sunday, July 3, 2016

AISEE ZITTO NI KAMA SHAABAN ROBERT

Kutokana na kile kinachodaiwa uhuru wa kuzungumza sasa ushakani Zitto ameamua kufuata nyayo za Shaaban Robert mwana fasihi nguli wa kiswahili. unatumia lugha ya picha kuwasema watawala. umesoma kitabu cha Kusadikika au Kufikirika vya Shaaban Robert? Zitto kupitia ukurasa wake wa facebook ameandika hivi, unadhani hapa anawazungumzia akina nani? 

'Jamhuri moja ya KUFIKIRIKA ina wanajeshi wake nchi jirani, magharibi. Huko nchi jirani kuna nchi jirani nyengine inasaidia waasi ambao Jamhuri ya KUFIKIRIKA imeenda kupambana nao kwa ombi la Umoja wa Mataifa. Amiri Jeshi Mkuu mpya wa KUFIKIRIKA ana mahusiano ya karibu sana na Amiri Jeshi Mkuu wa Nchi ambayo inasaidia waasi wanaopigana na Askari wa KUFIKIRIKA.
Ari ya Wapiganaji itakuwa chini sana na kitakachofuata ni urafiki wa wakubwa kutamalaki na maslahi ya nchi kuwekwa pembeni. Madhara yake hayaelezeki...'

No comments:

Post a Comment