Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Saturday, August 31, 2013


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA


PRESIDENT’S OFFICE
PUBLIC SERVICE RECRUITMENT SECRETARIAT
Ref. Na EA.7/96/01/E/14 21ST AUGUST, 2013

VACANCIES ANNOUNCEMENT

Public Service Recruitment Secretariat (PSRS) On behalf of the Kibaha Education Centre (KEC), invites qualified Tanzanians to fill 36 vacant posts in the above public institutions.


NB: GENERAL CONDITIONS

i. All applicants must be Citizens of Tanzania.
ii. Applicants must attach an up-to-date current Curriculum Vitae (CV) having reliable contact postal address, e-mail address and telephone numbers.
iii. Applicants should apply on the strength of the information given in this advertisement.

iv. The title of the position and institution applied for should be written in the subject of the application letter and marked on the envelope; short of which will make the application invalid.


v. Applicants must attach their detailed relevant certified copies of Academic certificates:

- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma transcripts.
- Form IV and Form VI National Examination Certificates.
- Computer Certificate
- Professional certificates from respective boards
- One recent passport size picture and birth certificate.
vi. FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS ARE STRICTLY NOT ACCEPTED
vii. Testimonials, Partial transcripts and results slips will not be accepted.
viii. Presentation of forged academic certificates and other information in the CV will necessitate to legal action


ix. Applicants for senior positions currently employed in the public service should

route their application letters through their respective employers.

x. Applicants for entry levels currently employed in the Public Service should not apply, they have to adhere to Government Circular Na. CAC. 45/257/01/D/140 dated 30th November, 2010.


xi. Applicants who have/were retired from the Public Service for whatever reason should not apply.
xii. Applicants should indicate three reputable referees with their reliable contacts.

xiii. Certificates from foreign examination bodies for ordinary or advanced level education should be certified by The National Examination Council of Tanzania (NECTA)
xiv. Certificates from foreign Universities should be verified by The Tanzania Commission for Universities (TCU)
xv. Dead line for application is 4th September, 2013 at 3:30 p.m


xvi. Applicants with special needs/case (disability) are supposed to indicate
xvii. Women are highly encouraged to apply
xviii. Only short listed candidates will be informed on a date for interview
xix. Application letters should be written in Swahili or English

APPLICATION LETTERS SHOULD BE POSTED TO THE FOLLOWING ADDRESS. HAND DELIVERY IS NOT ACCEPTABLE:
Secretary OR Katibu
Public Service Recruitment Sekretarieti ya Ajira katika Secretariat, Utumishi wa Umma
P. O. Box 63100 S. L. P 63100,
DAR ES SALAAM. DAR ES SALAAM
 
 

FAHAMU HISTORIA YA WAIRAQW NA ASILI YA JINA MBULU

Wairaqw ni moja ya makabila matatu tu Tanzania ambalo ni jamii ya Wakushi au Wahamitiki wenye asili yao kwenye nchi za Ethiopia tofauti na wengi wanavyoamini kuwa asili yao ni mesopotamia yaani Iraq ya sasa(mengine ni Wambugu waliopo Tanga na Wagorowa au wafyomi waliopo Babati). Utafiti wa kiathropolojia na hata vinasaba (DNA) uliofanyika unathibitisha kuna uhusiano mkubwa kati ya Wairaqw na hao wakushi wa Ethipia na Eritrea, kuanzia muundo na matamshi ya lugha, miili (body structure), mavazi na hata shughuli za kila siku ikiwemo hata michezo kwani Wairaqw kama walivyo waethipia wanasifika kwa riadha na wamefanana katika kila hali
 

 
Kutokana na sababu ambazo hazifahamiki japo inaaminika kuwa ni kwa sababu ya vita au njaa ya mara kwa mara inayoikumba eneo hilo la pembe ya Afrika, kundi moja la watu lilihama kuelekea kusini kufuata bonde la ufa kwa miaka mingi sana. Walipofika kaskazini kwa Tanzania ya sasa, wakagawanyika makundi mawili ambapo kundi moja dogo lilielekea mashariki na kundi lingine likaendelea na safari yao wakifuata bonde la ufa kuelekea kusini. Kundi hilo dogo lilifika mpaka milima ya usambara Tanga na kukaa huko mpaka leo ambao ndio wanaofahamika kama Wambugu.

 
Inasemekana kundi kubwa liliendelea kusonga mpaka kusini mwa Tanzania hadi Iringa wakaishi huko kwa miongo mingi sana kabla ya kuamua kurudi kaskazini baada ya kuona eneo hilo haliwatoshi baada ya kustawi sana hapo. Katika thesis yake ya PHD, Dr. Jackson Makwetta ambaye ni Mhehe aliandika kuwa jina la wahehe limetokana na kabila moja dogo ambalo liliishi zamani karibu na wahehe ambalo kwa sasa lipo wilayani Mbulu mkoani Arusha (sasa Manyara) ambalo wao kila wakimwona mtu asiye wa kabila lao walimwita Hee! Hee! 

 
Lakini pia, masimulizi ya wazee wa kiiraqw yanaanzia kwenye sehemu inayoitwa Gusir Ma/angwatay, nchi inayoelezwa kuwa ni ya baridi sana iliyopo kusini, ambapo hawakumbuki wala hakuna masimulizi yanayoeleza kabla ya kufika hapo walitoka wapi lakini wanajua baada ya kuondoka hapo wakafika sehemu inayoitwa Gusir Tiwalay yaani sehemu tuliyopigwa. Hapa ndipo historia ya Wairaqw ilipoandikwa upya na kuchukua sura nyingine kabisa, eneo hili inasemekana ni kati ya Babati, Hanang na Kondoa.
 
Wakiwa hapa, wairaqw walistawi sana wakiwa na ng`ombe na mazao ya kutosha, wakashamiri katika michezo na mafunzo ya kivita lakini hawakuwa na watu wa kupigana nao. Masimulizi yanaeleza kuwa katika kipindi hiki mchezo wa kupigana kwa fimbo yaani Ilgendi ulishamiri sana ambako kulikuwa na hadi mashindano ya kutafuta bingwa wa mchezo huo. Vijana wakajawa na kiburi na kuona wao ni wao, wakamshinikiza kiongozi wao aliyeitwa Haymu Tippe awaletee watu wa kucheza nao (kupigana nao) na kumteka mtoto pekee wa Haymu na kumtishia kuwa kama hatawaleta watu wa kupigana nao watamuua huyo mtoto. Japo Haymu Tippe aliwaasa hasa baada ya ramli yake kuonesha madhara makubwa yatakayotokana na vita hivyo lakini vijana hao waliushikilia msimamo wao, walidai vita.
 
Haymu akaenda akawafuata wadatoga lakini kabla hawajafika, Haymu alitoroka na baadhi tu ya watu wa ukoo wake (Tippe) na ukoo wa Duwe na Naman (wengine wanadai ni Masaay) ambao ndio waliomsikiliza. Waliobaki nyuma na kusubiri vita walimalizwa wote na hakubaki hata mtu moja. Katika kukimbia huko, Haymu alikuwa na mpwa wake (mtoto wa dada yake) aliyeitwa Gortoo ambapo katika kukimbia kuelekea ukingo wa bonde la ufa kwa kaskazini waligawanyika huku Gortoo akiwangoza kundi dogo kuelekea mlima Kwaraa uliopo Babati na Haymu Tippe na kundi lingine wakielekea mlima Hanang (/Anang) lakini wakaamua kukimbilia kwenye kingo za bonde la ufa eneo la Madunga na kisha kufuata kingo hizo kuelekea Kaskazini Mashariki hadi milima ya Tlahhara na Nou hadi Irqwar Daaw sehemu inayoitwa Mama Isara.
 
Gortoo na kundi lake wakakaa huko Kwaraa na maeneo ya Babati na ndio wakawa kabila la Gorowa au Wafyomi ambao kwa sehemu kubwa wamefanana na wairaqw isipokuwa baadhi ya matamshi ya maneno kutokana labda na mabadiliko ya mazingira lakini wanasikilizana.
 
Wairaqw waliishi hapo Mama Isara kwa miaka mingi sana na kuanza kuongezeka kutoka hizo koo tatu tu, wakaanza kupokea watu kutoka koo mbalimbali (assimilation) na kuunda koo mpya, mfano ukoo wa Bayo uliundwa na Wanyiramba waliofikia kwa mtu anayeitwa Bayo na kisha kuitwa Manda do Bayo! Aidha ukoo mkubwa kuliko wote wa Wairaqw ambao ni Sulle asili yao ni Wadatoga na utafiti unaonesha kuwa wadatoga wote wanaopakana na Wairaqw wanazungumza Kiiraqw na zaidi ya nusu ya hao wadatoga wanajitmbulisha kama Wairaqw tena wengi wa hao wazazi wote wawili wakiwa wadatoga.
 
Baada ya kukaa Mama Isara kwa miaka mingi na baada ya sera ya serikali ya kikoloni ya Kiingereza kuamua kufyeka maeneo kuondokana na mbung`o waliokuwa wanasababisha tauni, Wairaqw walianza kutoka huko milimani na kujaza maeneo ya Karatu, Mbulu, Babati, Hanang na kusonga magharibi hadi Haydom kote huku wakisonga nyuma ya Wadatoga ambao huhamahama kutafuta malisho na ndio maana majina karibu yote ya huku yanaasili ya Kidatoga.
 
Je! jina Wairaqw ni Wambulu! na nini asili ya jina Mbulu? itaendelea kesho? 
 

Thursday, August 29, 2013

MZEE MOYO APINGA MANSOUR KUTIMULIWA CCM

Zanzibar. Wakati Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano Zanzibar, Hassan Nassor Moyo, akisema uamuzi wa CCM kumfukuza uanachama Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki, Mansour Yussuf Himid, siyo sahihi, Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM) Wilaya ya Dimani, Unguja umesema chama hicho kiwatazame vigogo wengine wanaokwenda kinyume cha maadili yake.
                               
Halmashauri Kuu ya CCM ilimvua uanachama Mansour kwa kile kilichoelezwa kukisaliti chama, kwa kushindwa kusimamia malengo ya CCM na kutekeleza masharti ya uanachama, kushindwa kutekeleza wajibu wa mwanachama na kukiuka maadili ya viongozi wa CCM na kuikana ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa 2010-2015 na kuisaliti CCM.
UVCCM ilidai kuwa hatua hiyo isimkumbe peke yake, badala yake iwatizame wabunge, wawakilishi na viongozi wengine wanaokwenda kinyume na sera za chama hicho.

 
Taarifa ya umoja huo kwa vyombo vya habari iliyosainiwa na Katibu wa UVCCM Wilaya ya Dimani, Yussuf Suleiman, inadai umoja huo umepata faraja na imani kuona chama chao kinatetea nidhamu ili kukabiliana na vurugu zilizokuwa zikifanywa na mwakilishi huyo.
 
Pia, inadai umefika wakati wa uongozi wa chama hicho kuchukua hatua za maadili dhidi ya wawakilishi na wabunge ambao mchana ni CCM na usiku hugeuka maadui na wasaliti.

 
Moyo apinga
Mwanasiasa huyo mkongwe alisema jana mjini hapa kwa simu kuwa Mansour ameonewa, kwa sababu hakupewa nafasi ya kujitetea kabla ya kuchukuliwa hatua ya kufukuzwa na Halmashauri Kuu ya Taifa. 
                              
Moyo (pichani kulia) aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa miaka mingi, alisema hata yeye, moyo wake upo kwenye muundo wa Serikali ya Muungano wa Mkataba.

 
Watu waonaotaka Muungano wa Mkataba katika mapendekezo ya Katiba Mpya inayojadiliwa sasa wanataka ziwepo Serikali mbili za Tanganyika na Zanzibar zenye mamlaka kamili, baadaye kuwapo na Muungano wa mkataba baina ya Serikali hizo.
 
“Utashi wangu ulikuwa kwenye mkataba, lakini Kamati ya Katiba haikutupa kwa hiyo sasa kete yangu naitupa kwenye Serikali tatu,” alisema Moyo.

 
Alipoulizwa kuhusu madai kuwa atajivua uanachama wa CCM ikiwa Mansour atafukuzwa, Moyo alisema hakuwahi kusema hivyo bali alieleza ikiwa Mansour anafukuzwa na yeye anaweza kufikwa na hatua kama hiyo, kwani ana fikra sawa na Mansour.
 
“Sijasema nitajivua uanachama, ila nilieleza kuwa nami nitakuwa na hali kama hiyo ya Mansour kwani msimamo wangu si tofauti,” alisema Mzee Moyo.

 
CCM kina msimamo wa kutaka mfumo wa sasa wa Muungano wa Serikali mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar uendelee.

 
Hata hivyo asilimia kubwa ya wananchi wa Zanzibar waliotoa maoni yao kwa Kamati ya Katiba wanataka Muungano wa Mkataba na Serikali mbili za Tanganyika na Zanzibar, zenye mamlaka kamili na Kamati ya Katiba imetoa rasimu yenye kupendekeza Serikali tatu; Shirikisho, Zanzibar na Tanzania Bara.

 
Mansour agoma
“Naomba uniache tafadhali, nasikitika kuwa sitakuwa tayari kuzungumzia suala  hilo kwa sasa,” alisema. 
                              
Jumamosi iliyopita Mansour alizungumza na gazeti na kusema anasubiri uamuzi wa Halmashauri Kuu kujua hatma yake na kuahidi kuwa, angezungumza baada ya uamuzi huo, jambo ambalo ameshindwa kutekeza kwa kuendelea kuwa kimya.
 
Mara ya kwanza, tuhuma za Mansour zilifikishwa katika kikao cha Kamati ya Maadili ya CCM Zanzibar, kilichoketi Agosti 16, mwaka huu Ofisi za CCM Kisiwandui na wajumbe wa kamati hiyo kwa kauli moja walitoka na azimio la kumvua uanachama. Uamuzi wa kumvua uanachama Mansour uliwasilishwa katika kikao hicho chini ya Makamu Mwenyekiti wake, ambaye pia ni Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein. Hatua hiyo inaliacha wazi Jimbo la Kiembesamaki kwa ajili ya uchaguzi wa mwakilishi. 

Chanzo: Mwananchi                              

Sunday, August 25, 2013

SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA, MBUNGE WA NZEGA, Dr. KIGWANGALLA AJITOA MHANGA KUWATAJA WAHUSIKA

Hamisi KigwangallaSakata la madawa ya kulevya limechukua sura mpya, baada ya mbunge wa Nzega Hamisi Kigwangalla kuahidi kuwaanika wote wanaojihusisha na biashara hiyo haramu, akitumia ukurasa wake wa facebook Mh. Kigwangalla ameandika kuwa, kupitia Bunge lijalo, atajitoa mhanga kuwaanika wote, hivyo na kuwataka wananchi wanaowajua wauza  'unga' wampe ushirikiano kwa kumpenyezea majina ya wahusika. kupitia ukurasa wake huo, ameandika hivi:
 
 
 "Kuna watu wengi sana mtaani wanadai wanawajua wauza dawa za kulevya. Mimi najitoa mhanga kuwaanika hadharani kupitia Bunge litakaloanza keshokutwa. Naomba sasa kila mwenye taarifa sahihi kuhusu mtu yeyote anayefahamika kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya anipenyezee ili mimi nimfunge paka Kengele. Tuache siasa na minong'ono isiyo na tija, leteni taarifa tuchukue hatua!"

KAGASHEKI NA MEYA WA BUKOBA Dr. AMANI KUPIGWA STOP KUGOMBEA UBUNGE 2015

Dodoma.
Suala la kutimuliwa kwa madiwani wanane wa CCM katika Manispaa ya Bukoba limeingia sura mpya baada ya Kamati Kuu kuwazuia Meya, Dk Anatory Amani na Mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Khamis Kagasheki kushiriki katika siasa mkoani humo hadi mwaka 2015.

 
Habari zilizopatikana kutoka ndani ya kikao hicho zinaeleza kuwa uamuzi huo umefikiwa baada ya kubainika mgogoro wa viongozi hao, unakiumiza chama katika jimbo hilo.

 
Taarifa zilidai chanzo cha ugomvi kati ya Balozi Kagasheki na Dk Amani, ni kwa kila mmoja kutaka kugombea nafasi ya ubunge Jimbo la Bukoba mjini katika uchaguzi ujao. Na kwa uamuzi huo, Kagasheki na Dk Amani hawatashiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
 
Hata hivyo, akitangaza uamuzi huo jana, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema viongozi hao watakutana na Kamati Kuu leo na baada ya hapo utatangazwa uamuzi  uliofikiwa. 
                              
Mbali na meya na mbunge huyo ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, wengine walioitwa katika kikao hicho cha leo ni Mwenyekiti wa CCM mkoani humo, Costansia Buhinye, katibu wake, Averin Mushi pamoja na mwenyekiti wa chama Wilaya ya Bukoba, Yusuph Ngaiza na katibu wake, Janath Kayanda.

 
Kutokana na uamuzi huo, Kamati Kuu ambayo ilimaliza kikao chake saa 8:30 usiku wa kuamkia jana italazimika kukaa tena leo kuwaelezea uamuzi uliofikia.

 
Kumekuwapo na mgogoro mkubwa katika Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Bukoba, ukimuhusisha Kagasheki na baadhi ya madiwani kwa upande mmoja; na Dk Amani na kundi jingine la madiwani kwa upande mwingine.
 
 
Wakati wa mgogoro huo madiwani wamekuwa wakituhumiana ufisadi, na CCM imekwishawatuma viongozi wake wa juu kuingilia kati mgogoro huo akiwamo mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete, lakini hakuna mafanikio yaliyopatikana.

 
Kufikishwa kwenye Kamati Kuu kwa suala hilo kumekuja baada ya uongozi wa CCM Mkoa wa Kagera kuamua kuwatimua uanachama madiwani hao, hatua ambayo ilikuwa inahatarisha nafasi zao na hivyo kukiingiza chama hicho kwenye uchaguzi mdogo.
 
Habari kutoka ndani ya vikao hivyo zinasema kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa viongozi hao kuwajibishwa kwa kukiuka kanuni, kwa kuwa upo uamuzi wa chama unaokataza viongozi waliochaguliwa katika vyombo vya dola kuwajibishwa kwa staili hiyo.
 
Madiwani waliovuliwa uanachama na kata zao katika mabano ni pamoja na Richard Gaspar (Miembeni ), Murungi Kichwabuta (Viti Maalumu), Alexander Ngalinda ambaye pia ni Naibu Meya (Buhembe) na Yusuf Ngaiza ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya (Kashai).
 
Wengine ni Deusdedit Mutakyahwa (Nyanga), Robert Katunzi (Hamugembe), Samwel Ruhangisa (Kitendaguro) na Dauda Kalumuna (Ijuganyondo).
 
Baada ya kutimuliwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema chama Mkoa wa Kagera hawana uwezo wa kuvua uanachama na kwamba wenye uwezo huo ni ngazi ya taifa.
 
Nape alisema kwa mujibu wa taratibu za CCM, Mkoa wa Kagera walitakiwa kuwasilisha tuhuma hizo ngazi za juu ili zijadiliwe na kuamuliwa na Kamati Kuu (CC).

 
Aliongeza kuwa kwa mujibu wa taratibu, viongozi wa kuchaguliwa na wananchi kama wabunge na madiwani, hawawezi kuvuliwa uanachama na vikao vya chini bali chombo chenye mamlaka hayo ni Kamati Kuu. 

                              
Hata hivyo, siku moja baada ya tamko hilo la Nape, CCM mkoani Kagera kilisisitiza kuwa uamuzi wa kuwafukuza madiwani hao ni halali, kwa kuwa ulifanywa na kikao halali kwa mujibu wa katiba na kanuni za chama hicho.
 
Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Kagera, Costansia Buhiye, alisema kwa mujibu wa katiba na kanuni za chama hicho, hakuna kikao chochote ndani ya chama kinachoweza kukinzana na kikao kingine kwa hivyo, bado madiwani hao wamefutiwa dhamana ya uanachama kama mkoa ulivyoamua.

 
Buhiye alisema kikao cha Halmashauri Kuu ya Mkoa ndicho kikao kikuu chenye uamuzi wa kumwajibisha mwanachama yeyote, iwapo atabainika kwenda kinyume cha taratibu na kanuni za chama, kwa mujibu wa katiba ya CCM.
 
 
Suala la Mansour
Katika hatua nyingine, Kamati Kuu imelipeleka suala la kutimuliwa uanachama kwa Mwakilishi wa Kiembesamaki Zanzibar, Mansour Yusuf Himid kwenye Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ambako litajadiliwa leo na kutolewa uamuzi.
 
Nape alisema mamlaka ya mwisho ya kumteua mwakilishi ni NEC, hivyo lisingeweza kujadiliwa na Kamati Kuu.



Via: Mwananchi

Friday, August 9, 2013

AKINA HENRY KILEWO KULA IDD URAIANI, WATOKA GEREZANI NA Wafichua walivyoteswa wawasingizie ugaidi Mbowe, Slaa

HATIMAYE makada watano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wanaokabiliwa na shtaka la kummwagia tindikali kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), wameachiwa kwa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mfawidhi Wilaya ya Igunga.
 
 
Makada hao ambao wanatetewa na mawakili Prof. Abdallah Safari na Peter Kibatala ni pamoja na Avodius Justinian (Bukoba), Oscar Kaijage (Shinyanga), Rajabu Daniel (Dodoma), Seif Magesa (Mwanza) na Henry Kileo (Dar es Salaam).
 
 
Muda mfupi baada ya kuachiwa, vijana hao walifichua jinsi walivyopata mateso makali kutoka kwa maofisa wa jeshi la polisi wakilazimishwa kuwataja viongozi wa juu wa CHADEMA, Mwenyekiti Freeman Mbowe, Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa, John Mnyika na Tundu Lissu kuwa wanahusika na ugaidi.
 
 
Bila kumung’unya maneno waliwataja vigogo kadhaa wa serikali, CCM na mbunge mmoja wa CHADEMA kuwa ndiyo waratibu wa mikakati hiyo ya kuwabambika CHADEMA kesi za ugaidi.
 
Vijana hao waliowasili mjini Igunga 12:45 jioni juzi na kupandishwa kizimbani katika mahakama hiyo saa 1:20 usiku na kusomewa shtaka lao la kufanya kitendo kilicholenga madhara mwilini.
 
Mapema hati ya mashtaka iliyowasilishwa mahakani hapo na Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Mrakibu Msaidizi, Cosmas Mboya, makada hao walidaiwa kutenda kosa la kummwagia tindikali kada wa CCM, Mussa Tesha, usiku wa Septemba 9, 2011, katika msitu wa Hanihani, Igunga.
 
Mbela ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Ajali Milanzi, ilidaiwa na mwendesha mashtaka kuwa washtakiwa hao kwa pamoja walimmwagia kada huyo tindikali sehemu za uso, puani, mdomoni na kwenye bega la kulia.
 
 
Mwendesha mashtaka alidai kuwa shauri hilo limekwenda wilayani Igunga baada ya Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora, kuwafutia shtaka la ugaidi na kuamuru kwamba warejeshwe Igunga na kushtakiwa kwa kosa la kumwagia tindikali kisha wapatiwe dhamana.
 
 
“Masharti ya dhamana yaliyowekwa na mahakama ni kila mshtakiwa kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini dhamana kwa ahadi ya sh milioni 10 za maandishi kila mmoja.
 
 
Washtakiwa wote walikana shtaka hilo na kutimiza masharti ya dhamana kisha hakimu akaiahirisha kesi Septemba 10 mwaka huu itakapotajwa tena.
 
 
Katika hatua nyingine, vifijo, nderemo, vilio vya furaha na shangwe vilitawala mahakamani hapo baada ya makada hao kuachiwa kwa dhamana.
 
 
Wafuasi wa CHADEMA walifanya maandamano yaliyoongozwa na msururu wa magari, pikipiki na baiskeli wakitembea umbali wa takriban kilomita tano kutoka mjini Igunga kwa lengo la kuwapokea makada hao.
 
Akizungumza kwa kifupi, wakili wao Peter Kibatala, aliendelea kuishukuru Mahakama Kuu Kanda ya Tabora kwa kuonyesha ujasiri wake na kutimiza majukumu yake ya kutoa haki.
 
“Namshukuru Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, Simon Likelerwa, kwa weledi wake wa kutoa uamuzi ulio sahihi kisheria na ulioshiba.
 
“Pia naipongeza mahakama ya Igunga kwa kuwapatia dhamana washtakiwa kwa masharti yanayoendana na uzito wa jambo lenyewe kwani dhamana ni haki ya msingi kwa mshtakiwa yeyote,” alisema.
 
Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Tabora, Kansa Mbaruku, alisema kuwa pamoja na kuridhishwa na hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, pia hiyo ni ishara kuwa haki imezingatiwa kisheria.
 
Awali makada hao walifutiwa mashtaka na mahakama ya wilaya ya Igunga kisha kukamatwa tena na kupelekwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Tabora kusomewa shtaka la ugaidi ambalo hata hivyo lilifutwa na mahakama hiyo.
 
Mikakati ya hujuma 
Wakisimulia kile kilichowapata tangu kukamatwa kwao hadi kufikishwa mahakamani, makada hao walisema kuwa walipata mateso makubwa huku wakilaghaiwa kupewa vyeo serikalini na fedha ili mradi wawahusishe viongozi wa CHADEMA na ugaidi.
 
Evodius Justinian (Bukoba)
Alisema kuwa alikamatwa Bukoba: “Nikakaa rumande siku tatu kabla ya kusafisirishwa hadi Mwanza. Nikiwa huko niliteswa sana ili nikubali kuwa ninajua ule mkanda wa Wilfred Lwakatare uliokuwa kwenye mitandao.
 
“Nilikataa, niliteswa sana nikahojiwa kama nilimmwagia Musa Tesha tindikali nilikataa. Nilisafirishwa kwa ndege kuja Dar es Salaam ambako nilipokelewa na polisi.
 
“Nikiwa uwanja wa ndege niliomba ruhusa kwenda chooni, askari walinifuata huko wakanitesa sana. Nilifanyiwa mahojiano na Advocate Nyombi na afande Pasua. Walinilazimisha nikubali kuwa viongozi wetu huwa wanafanya vitendo vya kigaidi,” alisema.
 
Alisema kuwa akiwa makao makuu ya jeshi la polisi, aliteswa sana kwa maelekezo ya Afande Pasua na Nyombi katika ghorofa ya nane, jengo la makao makuu ya polisi.
 
“Niliambiwa nieleze siri za Dk. Slaa, Mbowe, Mnyika na Lissu na niseme kuwa walihusika na vitendo vya utekaji na utesaji, nilipokataa nilipigwa shoti za umeme ili nikubali kusema.
 
“Walikuwa wametafuta hata waandishi wa habari wakisubiri nikubali ili wanirekodi. Nilitoa maelezo kwa kulazimishwa huku nikiteswa. Nilipata nafuu baada ya wakili wangu, Nyaronyo Kicheere, kuja ndipo nikaeleza nilivyofanyiwa ukatili,” alisema.
 
Alisema kuwa alisafirishwa toka Dar es Salaam hadi Igunga na kwamba kila walipopita alitambulishwa kwa makamanda wa polisi kuwa ni mtu hatari sana.
 
Seif Magesa (Mwanza)
Alisema kuwa alikamatwa Mwanza na mabaunsa wa Meya wa Manispaa ya Ilemela, Henry Matata, aliyefukuzwa CHADEMA, wakiambatana na Adam Chagulani ambaye pia alifukuzwa pamoja na baadhi ya maafisa wa Usalama wa Taifa.
 
“Nilipelekwa ofisi za Usalama wa Taifa. Nilihojiwa nikiulizwa mimi ni nani katika CHADEMA na kwa nini huwa nawasiliana na Mbowe, Dk. Slaa, Lissu au Mnyika,” alisema.
 
Alisema kuwa aliuzwa kama viongozi hao wanahusika na utekaji wa watu mbalimbali unaotokea nchini na alipokataa aliteswa sana kuanzia saa 3 hadi 7 usiku.
 
“Nilipigwa shoti za umeme kwa maelekezo ya afande Pasua. Yeye alikuwa anakuja kuniaga kuwa anaenda kunywa pombe, vijana watafanya kazi yao. Waliniambia kuwa Lwakatare alikuwa amenitaja kuwa mimi nafanya vitendo vya kigaidi. Nilikataa kata kata,” alisema.
 
Aliongeza kuwa Aprili 23, mwaka huu, waliwaleta mama yake mzazi, mama mkwe na mkewe huku wakimdhalilisha mbele yao lakini alikataa kubadili maelezo yake.
 
“Siku moja nikiwa nahojiwa simu ya afande aliyekuwa ananihoji ilikuwa karibu; kiongozi mmoja wa CCM (anamtaja) alipiga simu akisema kama nimekataa kusema lolote nipelekwe Igunga ambako nilipelekwa nikasomewa shtaka la kummwagia tindikali Musa Tesha,” alisema.
 
Oscar Kaijage (Shinyanga)
“Mimi nilikamatwa, nikaambiwa niwasaidie askari kufahamu wizi wa milioni 100 uliokuwa umefanyika kwa njia ya mtandao kwa kuwa mimi ni wakala wa Airtel.
 
“Lakini nilipokubali kwenda na askari kituoni nikawekwa chini ya ulinzi. Ghafla nikapelekwa kwa mkuu wa upelelezi akanielekeza kuwa nikapekuliwe nyumbani kwangu kama kuna silaha ya aina yoyote au chupa zenye majimaji. Nilipekuliwa hawakupata kitu. Ilikuwa yapata saa 5 mchana,” alisema.
 
Aliongeza kuwa ilipofika saa 12 jioni, alipelekwa tena kwenye ofisi ya mkuu wa upelelezi, akakutana na askari alioambiwa wanatoka Dar es Salaam.
 
“Hapo nikamkuta afande ninayemfahamu, anaitwa Pasua kwa kuwa aliwahi kufanya kazi Shinyanga na Simiyu. Walinihoji kwa nini nina namba za viongozi wa CHADEMA. Nikawaabia, ‘mbona hamuulizi za wale wa CCM?’,” alisema.
 
Alisema kuwa alijibiwa kuwa wanajua hana kosa ila wanataka ushirikiano aseme kuwa Mbowe, Slaa, Mnyika na Lissu wanahusika na utekaji unaotokea nchini.
 
“Nilikataa. Afande Pasua nikamwambia anajua kazi yangu na mimi namjua yeye ndipo wakasema sasa kwa kuwa sitoi ushirikiano nitaunganishwa kwenye kesi ya kummwagia Musa Tesha tindikali huko Igunga,” alisema.
 
Aliongeza kuwa alipelekwa Igunga na wakati wanahojiwa na askari wa kutoka makao makuu, walikuwa wanafanya siri hata OCD wa pale alikuwa haruhusiwi kusikia.
 
Rajabu Kihawa (Dodoma)
Alidai kuwa alichukuliwa Dodoma baada ya kupigiwa simu na msichana mmoja aliyedai kuwa na maagizo kutoka kwa kaka yake anayesoma naye Chuo Kikuu cha Dodoma.
 
“Nilikataa lakini alikuwa anapiga simu kila mara, nikaona ngoja nikamsikilize. Nilipofika kabla sijaongea naye nilikamatwa na maafisa sita wa polisi waliojitambulisha, wakaninyang’anya simu zote na kunipeleka polisi.
 
“Walinihoji kama najua mkanda wa Lwakatare, nikasema sijui. wakanihoji kama viongozi wa CHADEMA wanahusika na utekaji unaoendelea nchini, nako nikasema sijui,” alisema.
 
Alisema kuwa baada ya hapo alipelekwa na kufungiwa Chamwino siku mbili bila kupewa chakula kisha askari wakaja wakamuuliza kama amebadili msimamo.
 
Alitolewa akapelekwa hoteli ya Nam, ambapo aliwakuta vijana waliofukuzwa kwenye uongozi wa Bavicha (anawataja) meya mmoja wa Mwanza na diwani aliyefukuzwa CHADEMA na kijana mwingine wa chama hicho mkoa wa Pwani aliyevuliwa uongozi wa Bavicha.
 
“Niliombwa nikubali kupewa sh milioni 30 ili nikubali kurekodiwa nikisema kuwa Mbowe, Dk Slaa, Lissu na Mnyika wanahusika na vitendo vya kigaidi na utekaji.
 
“Nilikataa. Baadaye niliingizwa katika chumba kimoja cha hoteli hiyo nikakuta mbunge mmoja wa CHADEMA kutoka Kanda ya Ziwa (anamtaja) akaniambia, ‘angalia huku’ akinionyesha simu yake kuwa alikuwa akiwasiliana na Rais,” alisema.
 
Kihawa aliongeza kuwa aliahidiwa kupewa cheo kizuri serikalini na fedha ili mradi akubali kuwa viongozi hao wa CHADEMA wanafanya vitendo vya kigaidi.
 
“Nilimuuliza kwa nini alikuwa ananishauri hivi wakati yeye ni mbunge wa chama chetu. Akasema mimi nilishinda ubunge sio kwa sababu nipo CHADEMA, bali ni muhimu hata akiondoka CHADEMA.
 
“Nilikataa kukubali ushauri wao ndio niliambiwa napelekwa Igunga kuunganishwa kwenye kesi ya Musa Tesha,” alisema.
 
Henry Kileo (Dar)
Alisema kuwa alipigiwa simu na maafisa wa polisi makao makuu Juni 17, mwaka huu, wakimwarifu kuwa wanataka kufanya mahojiano naye lakini hawakusema ni kuhusu nini.
 
“Juni 21, mwaka huu, wakili wangu Peter Kibatala na John Mnyika (mbunge wa Ubungo) tulienda polisi makao makuu, nilihojiwa mambo mbalimbali likiwemo tukio la kummwagiwa tindikali Musa Tesha.
 
“Nilicheka sana kwa kuwa kabla ya kuitwa nilipata taarifa za kikao kilichofanyika Dodoma ili kuniunganisha na kesi ya ugaidi. Mahojiano yalifanyika wakati tayari kuna kesi iliyokuwa inaendelea huko Igunga,” alisema.
 
Kileo alisema kuwa baada ya mahojiano hayo na kuandikisha maelezo saa 11.30 jioni, polisi walimnyima dhamana na kumpeleka rumande ya kituo kikuu cha polisi alikolala.
 
“Jumamosi ya Juni 22, familia yangu ilikuja kunitembelea ikakatazwa lakini baadaye wakili wangu aliwasiliana na makao makuu ya polisi ndipo wakaruhusiwa kuniona.
 
“Juni 22, mwaka huu, nilisafirishwa kwa ndege nikapelekwa Igunga kuunganishwa kwenye kesi ya kummwagia tindikali Musa Tesha baada ya kukataa kujibu maswali ya kuwahusisha viongozi wa CHADEMA na vitendo vya utekaji vinavyotokea nchini,” alisema.
 
Habari kwa hisani ya gazeti la Tanzania Daima

Thursday, August 8, 2013

SOMA MEXICO

TANGAZO LA SKOLASHIPU ZILIZOTOLEWA NA SERIKALI YA MEXICO KWA TANZANIA KWA MWAKA 2014
 
Serikali ya Tanzania imepokea mwaliko wa Skolashipu kutoka kwa Serikali ya Mexico kwa mwaka 2014.

Wadau wote, raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wenye sifa wanashauriwa wasome mwongozo na maelekezo kwenye Kiambatisho cha tangazo hili na kuyafanyia kazi.

Maombi yaliyokamilika yakiwa na nyaraka zote zilizoorodheshwa ukurasa wa pili kwenye Kiambatisho isipokuwa kipengele cha “Official nomination”, yawasilishwe Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kabla ya tarehe 20/08/2013 kwa anuani ifuatayo:-

Katibu Mkuu,
Wizara Ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
S. L. P 9121,
DAR ES SALAAM

MAELEKEZO YOTE YAKO HAPA

http://www.moe.go.tz/index.php?option=com_docman&task=doc_download&gid=273&Itemid=385

MADUDU MTIHANI WA DARASA LA SABA

 
 
  Ni wa majaribio katika wilaya 40


  Maswali mengine yakosa majibu

  12 yamtoa jasho Profesa UDSM
 
Madudu zaidi yamebainika katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, baada ya mtihani wa kujipima wa darasa la saba uliofanyika Julai, mwaka huu katika wilaya 40 za Tanzania Bara kuwa na mapungufu makubwa na ya wazi.
 

Aidha, maswali 12 kati ya 50 katika mtihani wa Hisabati hayana majibu, 14 ni magumu ambayo mtoto wa darasa la saba hawezi kuyajibu na mengine matano yamekosewa na hata yafanywe kwa kiasi gani hayawezi kuwa na majibu.
 


Mbunge wa Kuteuliwa (NCCR-Mageuzi), James Mbatia, alibainisha madudu hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake na kuwataka Watanzania kushiriki kupinga anguko la elimu linalotia aibu Taifa.
 

Mbatia alibainisha kuwa katika mtihani huo uliofanywa Julai 8 na 9, mwaka huu, kwa masomo ya Hisabati, Kiswahili na Kiingereza, jina la Wizara limeandikwa ni Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi huku usahihi hakuna neno Stadi.
 

Alisema matokeo hayo yamekuja katika kipindi ambacho serikali iko katika dhana ya matokeo makubwa sasa (big result now), katika sekta ya elimu na mtihani huo umetungwa kwa dhana hiyo.
 
Alisema baada ya kupata mtihani huo, alikusanya baadhi ya walimu wa shule za msingi na sekondari katika moja ya shule jijini Dar es Salaam na kuufanya na zaidi ya nusu walishindwa kupata daraja la tatu yaani C.
 

“Sikuishia hapo, nilimtafuata msomi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) yaani Profesa na kumpa mtihani wa hesabu aliufanya kwa muda wa saa 2:03, lakini na hakupata daraja la kwanza, alishindwa kujibu baadhi ya maswali na mengine kukosa majibu kabisa,” alisema.
 

Kwa mujibu wa Mbatia, Profesa huyo alisema swali namba 33 ni gumu ambalo linafanywa na mwanafunzi wa fani ya uhandisi na linahitaji muda mrefu kupata jibu.
 

“Sikutaka kuridhika na majibu yao, nilijifungia ofisini majira ya asubuhi kwa saa 2:30 na kuufanya mtihani wote nikalinganisha na majibu ya wengine, lakini sikupata alama A…ninachojiuliza hii ndiyo Big Result Now?” alibainisha na kuhoji.
 
 
Alisema kwa muundo wa mtihani huo, ni kuwakatisha tamaa wanafunzi na kuwafanya wazidi kulichukia somo la hisabati na kiwango cha taaluma nchini kuendelea kuporomoka.
 

Katika somo la Kiingereza, kulikuwa na mapungufu makubwa ya kisarufi na majina ikiwamo historia ya Tanzania kwa viongozi wa Taifa kama Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Amani Karume.
 
 
Mbatia alisema jina la Mwalimu Nyerere limekosewa na kuandikwa Julias na Rais wa awamu ya Pili likiandikwa Ally Mwinyi badala ya Ali Hassan Mwinyi, huku wakishindwa kueleza kifo cha Karume na kueleza kama kifo cha kufanana na Mwalimu Nyerere. Itakumbukwa kwamba, Mwalimu Nyerere alifariki dunia baada ya kuugua wakati Karume aliuawa.
 
 
Aidha, alisema katika mtihani wa Kiswahili, kuna mapungufu mengi hususani ya usahihi wa lugha na kuwafanya Watanzania kujiuliza kama mitihani hiyo ilitungwa na wanataaluma walibobea au ni ubabaishaji.
 

Alisema suala hilo linakwenda sambamba na makosa yaliyopo kwenye vitabu vinavyotumiwa na wanafunzi wa shule za msingi hadi sekondari ambavyo vimepitishwa na kupewa cheti cha ithibati.
 
 
“Tumefika mahali pagumu kielimu yaani ni janga la kitaifa,” alisema Mbatia.
 
Alisema kitabu cha uraia cha darasa la nne, kuna mahali kimeandikwa ‘Serikali za mitaa zinaongozwa na viongozi wa vitongoji’ huku cha hesabu kikieleza namba nzima ni moja hadi 99 badala ya moja hadi tisa.
 
 
“Haya yote wanalishwa watoto wa maskini wa nchi hii, hakuna mtoto wa kigogo anayesoma kwenye shule hizi na hawajafanya mitihani hii,” alisema.
 
 
MAPENDEKEZO YA MBATIA
 
Kuundwa kwa tume ya kudumu ya elimu nchini, itakayoshughulika pamoja na mambo mengine, kuhakikisha ubora wa elimu nchini na kudhibiti mambo yote yanayosababisha kutetereka kwa ubora huo (Education quality assurance and control).
 
 
 
Aliongeza kuwa tume hiyo iwe na mamlaka ya kuhakiki utendaji wa taasisi mbalimbali za elimu ambazo hadi sasa zimeonekana kutotimiza vyema majukumu yake.
 

 
“Tume itakapoundwa inaweza vile vile kusaidia kubainisha wazi ni nini falsafa na malengo hasa ya utoaji wa elimu nchini kulingana na wakati tulionao,” alisema.
 
 
Januari 31, mwaka huu, Mbunge huyo aliwasilisha hoja binafsi bungeni kuhusu udhaifu uliopo katika sekta ya elimu nchini.
 
 
 
Alianisha sura hizo ni kuporomoka kwa uwajibikaji, kutokuthamini rasilimali za Taifa, kukithiri kwa ukiukwaji wa haki za binadamu, kumomonyoka kwa uadilifu miongoni mwa watumishi wa umma na kupungua kwa uzalendo.
 
 
Hata hivyo, hoja hiyo haikutiliwa maanani ingawa siku chache baada ya hoja hiyo, Wizara ilifuta Kamati ya Uthibitishaji ya Vifaa vya Elimu (Emac).        
 
 
Aidha, Februari 18, mwaka huu, Wizara hiyo ilitangaza matokeo ya kidato cha nne yaliyonyesha zaidi ya watahiniwa 240,000 walipata daraja sifuri ikiwa ni asilimia 66 na baadaye matokeo hayo yalipangwa upya na watahiniwa 210,000 wakapata daraja la sifuri.
 
 
Kwa mujibu wa matokeo ya ualimu ngazi ya Astashahada na Shahada yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani Tanzania (Necta),  Julai, mwaka huu, watahiniwa 2,606 wa Stashahada wanarudia mtihani na 533 wamefeli.
 
 
Msemaji wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Ntambi Bunyazu, alipotafutwa na NIPASHE, alithibitisha mitihani hiyo kufanyika katika halmashauri 40 nchini na kusema kwamba asingeeleza undani wa makosa yaliyobainika hadi atakapopata ufafanuzi wa kitaalam.
 
 
 
 Chanzo: Nipashe

 


KAULI YA HENRY KILEWO BAADA YA KUFUTIWA MASHTAKA YA UGAIDI

Baada ya Kufutiwa mashtaka ya ugaidi kamanda wa Chadema Henry Kilewo ameandika hivi katika ukurasa wake wa facebook;
 
Kwa watanzania wataka mabadiliko: jela siyo sehemu salama ya kuishi,wala haijawahi kuwa sehemu salama ya kuishi,wala haitakaa iwe sehemu salama ya kuishi pasipo tokea wajasiri na wazalendo kama mimi na wewe kwenda kuishi kwa hiari sehemu ambayo utawala dhaifu wa ccm unadhani ni kitisho cha kuzuia mabadiliko. Watawala wabovu kwenye nchi yetu hutumia jela kama kitisho cha kuzuia ukweli,ukiruhusu kitisho cha kuogopa jela utakuwa mwanamabadiliko kigeugeu na mnafiki machoni mwa umma. Kitisho hiki kamwe sintokiruhusu mimi henry kilewo hata kwa mtutu wa risasi za moto,japokuwa natambua athari za kukaa jela muda mrefu kama ambavyo shujaa wa... dunia nelson mandela anavyopitia kwasasa,
 
hii kwangu mimi ni sadaka tosha kwa taifa langu chama changu, familia yangu pamoja na ndugu jamaa na marafiki zangu. Nionyo na funzo kwa watawala dhaifu kudhani wataweza kuzuia harakati hizi za mabadiliko kwa kuvitumia vyombo vya dola vibaya kama usalama wa taifa, jeshi la polisi, mahakama na hata magereza. Kamwe tusiruhusu kuwa wanyonge wala kukubali kuonewa kwani watatuzuia kwa muda, watatudhalilisha kwa muda na sikuogopa kukaa jela ila moyo wangu unasononeka pale nionapo saa ya ukombozi inachelewa. Ni muda tu, tutashinda.

Wednesday, August 7, 2013

MKENYA ALIYETUHUMIWA KUMTEKA DR. ULIMBOKA AFUTIWA KESI

Jamaa aliyekuwa akidaiwa kumteka na kumtesa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka afutiwa mashtaka, hili ndo sakata ambalo Sugu alimwambia Kamanda Kova arudi studio kuisuka ngoma yake upya maana kitaa haikueleweka, ungana na mwanandishi Happiness Katabazi katika gazeti la Tanzania Daima kuhusiana na sakata hilo anaripoti hivi:
 
MKURUGENZI wa Mashitaka nchini (DPP), Dk. Eliezer Feleshi, amefuta kesi ya kuteka na kujaribu kumuua Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka, iliyokuwa ikimkabili raia wa Kenya, Joshua Mulundi, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.
 
 
Hatua hiyo imeelezwa kuwa ni baada ya DPP kuona hana haja ya kuendelea kumshitaki kwa makosa hayo ambayo yalikuwa hayana dhamana.
 
Hati hiyo ya DPP iliwasilishwa chini ya kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002 kwa niaba yake na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Tumaini Kweka, jana mbele ya Hakimu Mkazi Waliarwande Lema.
 
Kweka aliiambia mahakama kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa lakini upande wa Jamhuri hauna nia tena ya kuendelea kumshitaki Mulundi kwa kesi hiyo.
 
Hakimu Lema alikubaliana na hoja hiyo na akamfutia kesi hiyo Mulundi ambaye yupo gerezani tangu Julai 13, mwaka jana.
 
 
Hata hivyo muda mfupi baada ya Hakimu Lema kumfutia kesi hiyo Mulundi, askari kanzu walimkamata tena na kumfikisha kwa Hakimu Mkazi, Alocye Katemana na kisha Wakili Kweka akaiambia mahakama kuwa upande wa Jamhuri umemfungulia kesi mpya ambayo itakuwa na shitaka moja tu.
 
 
Mbele ya Hakimu Katema, wakili huyo alidai kuwa Julai 3, mwaka jana, Mulundi katika Kituo cha Polisi Oystebay alitoa taarifa za uongo kwa ofisa wa polisi kuwa yeye na wenzake walikodiwa kwenda kumteka na kumjeruhi Dk. Ulimboka, jambo ambalo si kweli.
 
 
Alidai kosa hilo ni kinyume cha kifungu cha 122 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002 na kuongeza kuwa upelelezi wa kesi hiyo mpya umekamilika.
 
 
Wakili Kweka alidai licha ya kosa hilo kuwa na dhamana kwa mujibu wa sheria, lakini upande wa Jamhuri unaomba Mulundi asipewe dhamana kwa ajili ya usalama wake.
 
Hakimu Katemana aliiahirisha kesi hiyo kwa muda na kisha kuutaka upande wa Jamhuri uende ukalete kwa maandishi hati ya kumfungia dhamana mshitakiwa huyo.
 
Hata hivyo mshitakiwa huyo alikanusha shitaka hilo na akaomba apewe dhamana kwani alikuwa na wadhamini. Pia alidai amesota muda mrefu gerezani bila kosa.
 
“Ninajua wanataka kunifungia dhamana makusudi ili waweze kunyamazisha Bunge na umma usiendelee kupiga kelele kuhusu tukio la kupigwa na kuteswa kwa Dk. Ulimboka na kwa taarifa yenu mkinipeleka tena gerezani naenda kuanza mgomo …nimechoka kuonewa,” alidai Mulundi.
 
 
Hata hivyo kesi hiyo iliporudi tena mchana, Wakili Kweka hakuweza kuja na hati ya kuzuia dhamana, hali iliyosababisha Hakimu Katemana kutoa masharti ya dhamana kwa mshitakiwa huyo.
Hata hivyo mshitakiwa huyo jana alishindwa kutimiza masharti hayo na Hakimu Katemana aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 20, mwaka huu.
 
 
Katika kesi hiyo awali, Wakili wa Serikali, Ladslaus Komanya, mbele ya Hakimu Agnes Mchome, alidai kuwa Mulundi Juni 26, mwaka jana, akiwa eneo la Leaders Club alimteka Dk. Ulimboka.
Katika shtaka la pili, Komanya alidai kuwa Juni 26, mwaka huu, akiwa katika eneo la Msitu wa Mabwepande, Tegeta, Dar es Salaam, kinyume cha sheria, mshtakiwa huyo alijaribu kumsababishia kifo Dk. Ulimboka.
 
Chanzo: Tanzania Daima

Monday, August 5, 2013

HENRY KILEWO AFUTIWA MASHTAKA YA UGAIDI, JOYCE KIRIA AUTAMANI UBUNGE

 
Kufuatia mume wake kufutiwa mashtaka ya Ugaidi sasa Joyce Kiria autamani Ubunge kupitia CHADEMA, hivi ndivyo alivyoandika katika ukura wake wa facebook;
 
Mlionishauri kwamba Mume wangu Henry akitoka nimshauri aache siasa, naomba niwaambie kwamba nimem join Mume wangu kwenye Siasa. pipooooooooooz
 
 
Hizi kesi zingine zinatufanya wengine tufanye maamuzi ya kujoin harakati...mke mwenzangu ana skafu na mie kombati... mtajuuuuuuuta kutugusa pabaya
 
"Mungu mkubwa sana mimi siyo mke wa Gaidi.... nipeni jimbo niwarudishie maumivu maana wamenigusa pabaya....."

 
Joyce Kiria ndani ya gwanda