Na. Furaha Venance : Manyoni-Singida
Ufunguzi
wa barabara hiyo ya lami Manyoni – Isuna yenye urefu wa kilometa 54
imezinduliwa leo na rais wa Jamhuru ya Muungano
wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, kabla ya ufunguzi huo, mkuu wa
wilaya ya Manyoni mama Fatuma Tawafiq alikaribisha Mkuu wa mkoa Dr. Paseko.
Kone kuzungumza na wananchi kidogo na kufanya utambulisho wa wageni
walioongozana na msafara wa rais.
Ilipowadia
nafasi ya Mh. John Chiligati mbunge wa Manyoni Mashariki kuzungumza na wananchi,
aliwahakikishia wakazi wa Manyoni kuwa, ujenzi wa barabara ya Manyoni
inayoingia mjini kati yenye urefu wa kilometa 4.5 haijasahaulika amekuwa
akizungumza na waziri wa ujenzi na kumuahidi kuwa barabara hiyo itajengwa hivyo
aliwataka wakazi hao wasiwe na wasiwasi kuhusu barabara hiyo.
Mh Chiligati pia
aligusia tatizo la maji, ambapo alisema kuwa ili kutatua tatizo la maji, kazi
mbili zinatakiwa kufanywa, kwanza ni kujenga tenki lenye uwezo wa kuhifadhi
maji lenye ujazo wa lita milioni moja lililopo halikidhi kwa kuwa lina ujazo wa
lita laki mbili na nusu tu, ujazo ambao ni mdogo ukilinganisha na mahitaji ya
wakazi wa wilaya hiyo, kazi ya pili inayotakiwa kufanywa ni usambazi wa maji
kutoka bwawa la Mbwasa na kuyasambaza katika vijiji vya bonde la ufa ambao
hukabiliwa na tatizo la maji,
Kuhusu
umeme mbunge huyo alisema kuwa inahitajika kutoa umeme mjini na kupeleka
vijijini, aliendelea kufafanua kuwa mradi wa kwanza wa kusambaza umeme wa
vijiji kumi, vijiji saba umeme umefika na kuna vijiji vitatu vilisahaulika
katika mpango huo ambavyo ni, Mbwasa,
Maweni na Sukamahela ambavyo kwa sasa vijiji hivyo vipo kwenye mpango.
Chiligati
alimuomba Mh. Rais kuwezesha wakazi wa Nkoko kupata umeme, katika hili alisema,
“..Mh. Rais wewe ndiye rais wa kwanza
katika nchi hii kufika Nkoko na naomba uwe rais wa kwanza kukipatia kijiji cha
Nkoko umeme..”
Mwisho
Chiligati aliwataka wana Manyoni kuwapuuza wote wanaopita pita wakiwadanganya
wananchi kuwa wanaleta mabadiliko, “..kuna
watu wanazunguka walienda Morogoro, wakaenda na Iringa na hapa watakuja, ndugu
zangu, wakija …ndugu zangu wana Manyoni tushikamane…” Inaelekea hapa
alikuwa anakizungumzia Chama cha Demokrasia na Maendeleo [CHADEMA] ingawa
hakukitaja chama chenyewe,maana ndiyo kumbukumbu zinaonesha wamepita huko na
ile Operesheni yao waliyoibatiza kwa jina la M4C.
Ulipowadia
wasaa wa Waziri wa Ujenzi Mh. John Pombe Magufuli alisema kuwa barabara hiyo ya
Manyoni –Isuna ina urefu wa Kilometa 54 na imetengenezwa kwa pesa za ndani
kiasi cha Tsh. Bilioni 32,
“Ujenzi wa barabara hiyo uliamia hapa
ilipojengwa kutoka Manyoni mjini ili kuepuka bomoa bomoa nyumba za watu lakini
cha ajabu watu wanaifuata hii barabara, napenda niwambie hao wote walioifuata
barabara hii tutawabomolesha, tena ngoja niwaambie kuifuata barabara ni
kutafuta umasikini.” Alisema
Magufuli.
Kuhusu barabara ya Manyoni mjini kati, Mh.
Magaufuli alisema tatizo halipo kwa selikali kujenga barabara hiyo, tatizo lipo
kwa Mkandarasi wa Wilaya aliyedizaini ujenzi wa barabara hiyo alileta
mapendekezo kuwa ujenzi wa kilomita 1.2 ni bilioni 1.2 kwa kiwango cha lami wakati
zipo barabara zimejengwa kwa milioni 250 hadi 300 kwa kilometa na zingine
zimejengwa kwa milioni 680 hadi 800 yeye
bilioni moja tena barabara ya wilaya!
Hivyo Magufuli aliwahakikishia wakazi wa
Manyoni Barabara hiyo itajengwa na Mkandarasi wa Wilaya hatakiwa kuiangalia
wala kuisogelea barabara hiyo itasimamiwa na Mkandarasi wa Mkoa na kuzitaka
Mamlaka husika kumfukuza kazi Mkandarasi huyo au kumshusha cheo akafanye kazi
zingine.
Rais
Jakaya M. Kikwete aliyotoa ahadi ya
kujenga tenki kubwa la maji kupunguza tatizo la maji Manyoni, kuhusu matatizoya
maji vijiji vya bonde la ufa , katika atua nyingine Rais aliwapandisha jukwaani
Mkurugenzi na Mhandisi wa Maji Wilaya kuwataka kueleza kwanini hawajashusha
maji kutoka Mbwasa kwenda vijiji hivyo
Na
kuiagiza Halmashauri kuuingiza mradi huo katika mipango yao kama mradi na yeye
atawasaidia kuwasemea.
Na
kuhusu umeme katika kijijicha Nkoko Mh. Rais aliahidi kuwa kijiji hicho
kitapata umeme, kuhusu ELIMU serikali itajitahidi kutatua tatizo la vitabu
katika shule zake pia aliwaagiza wakuu wa mikoa na wilaya kuhakikisha ndani ya
miaka miwili shule zote za kata zinajengwa maabara za sayansi na kuahidi
kutatua tatizo la walimu katika wilaya hii katika mgao wa walimu mwaka huu.
Vilevile
Mh. Rais aliwataka wananchi kujiepusha na ngono zembe ili kuepuka maambukizi
mapya ya virusi vya ukimwi, kuhusu AFYA alisema kuwa serikali yake imefanikiwa
kujenga vituo vya afya na zahanati ili kupunguza vifo vya akina mama wakati wa
kujifungua, pia wananchi wamepewa vyandarua kujikinga na malaria na kuwataka
wananchi wasitumie vyandarua hivyo kufugia kuku au kuvulia samaki.
Katika
uzinduzi huo viongozi mbalimbali wa kidini kisiasa na serikali walihudhuria,
pamoja na hao viongozi wengine waliohudhuria ni pamoja na Wakuu wa wilaya ya
Iramba na Singida, Mbunge wa Iramba Mwiguli Nchemba, wabunge wa viti maalumu
Diana Chilolo na Martha Mlata, Mwenyekiti mpya wa CCM Mkoa wa Singida Mgana
Msindai, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyarandu, Naibu waziri
wa Ujenzi na wengine wengi.
Chanzo: mimi mwenyewe
No comments:
Post a Comment