Kitendo cha Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania [JWTZ] kupiga picha akiwa na makada wa CHADEMA huku akiwa amevaa sare za jeshi hilo [kombati] na akionesha alama ya vidole viwili inayotumia na Chama hicho amezua gumzo katika mitandao ya kijamii na hata miongoni mwa wananchi ambao wameiona picha hiyo katika gazeti la Mwananchi la leo.
Wapo wanaoona kitendo cha wabunge hao kupiga picha na askari huyo huku wakijua kuwa ni kukiuka sheria za nchi ambazo wabunge hao wanazihamu zinazokataza askari yoyote wa majeshi ya Tanzania kuwa mwanachama au kushabikia chama chochote cha siasa ni kitendo kisichofanaa na kinachotakiwa kukemewa na watu wote bila kujali itikadi za vyama vyao. lakini wapo wanaoona kitendo cha askari huyo kujitokeza hadharani na kuonesha mapenzi yake kwa chama chake ni kitendo cha kishujaa na kuonesha kuwa hata askari nao wamechoshwa na chama cha mapinduzi [ccm] kinachotawala kwa sasa.
Nisikuchoshe kwa maelezo mengi angalia picha hizo chini ambazo zimeonekana kutawala na kuibua gumzo katika mitandao mbalimbali ya kijamii na wewe unaweza weka maoni yako baada ya kuangalia picha hizi.
Godbless Lema akihutubia mkutano wa hadhara huko Mererani
Askari wa JWTZ akiwa mguu pande kumsikiliza Lema na makada wengine wa CHADEMA
Hapa Lema akiwa katika picha na Askari huyo huku akiwa amenyoosha alama ya vema alama inayotumiwa na chama hicho
Kamanda wa JWTZ akiendelea kusikiliza na kufuatilia mkutano
Pia unaweza bofya hapa ~ http://j.mp/Tje9o9
Pia unaweza bofya hapa ~ http://j.mp/Tje9o9
No comments:
Post a Comment