Mhariri.
Kwanza kabisa
napenda kuwapongeza kwa kanzi yenu nzuri mnayoifanya kuwahabarisha Watanzania
kupitia gazeti hili la Mwananchi, lakini pia ningependa kuwashukuru na
kuwapongeza kwa nzuri ya kutuelimisha na makala za miaka 50 ya uhuru katika
matoleo mbalimbali ya gazeti hili kusema kweli makala hizo zimetujuza mengi sana
. Basi baada ya kutoa pongezi hizo naomba nijikite katika mada yangu
iliyonisukuma leo hii nami kujitokeza katika gazeti hili.
Ndugu zangu kwa
muda mrefu tumeona wadau mbalimbali hususani serikali ikijisifu kwa jitihada
kubwa iliyofanya ya kuongeza shule za sekondari, lakini imekuwa ikadai kuwa
changamoto iliyopo mbele yao ni upungufu wa walimu katika shule hizo, na hii
imesababisha watu wengi kudhani kuwa katika nchi hii watu waliosomea taaluma ya
ualimu ni wachache na hii inachagizwa zaidi na hatua ya serikali kutangaza hatua
ya kukabiliana na changamoto hiyo ni kuongeza udahili katika vyuo mbalimbali
katika taaluma ya Ualimu na hata kutoa udhamini wa asilimia mia
moja kwa wanafunzi wanaosomea ualimu hususani wa Sayansi.
Yote
haya yanafanywa kwa lengo la kupunguza uhaba wa walimu au kuliondoa kabisa hili
tatizo. Lakini mtakubaliana nami kuwa bila ya kuwa na mikakati ya maana hatua
zote hizo zitakuwa ni kupotoza muda tu! Na tatizo litaendelea hata baada ya
miaka 50 mingine ya uhuru, mathalani, tafiti mbalimbali ambazo zimefanywa na
wataalamu na hili linaweza pia kuthibitishwa hata na Maafisa Elimu Sekondari wa
Wilaya hapa nchini. Kwanza kati ya wahitimu walimu hususani wa Shahada ni
asilimia hamsini tu wanaoripoti vituo vya kazi walivyopangiwa licha ya kupewa
mikopo ya silimia mia moja au themanini, wengi wao wanaenda katika ajira
nyingine kama vile, polisi, jeshi la wananchi [JWTZ], jeshi la magereza,
uhamiaji, wengine katika taasisi binafsi n.k wengine utawakuta hata benki
wakifanya kazi lakini ni walimu na wanaokimbilia katika siasa
tusiwasahau!
Na wale
wanaoripoti katika maeneo yao ya kazi wanaripoti kama kutegeshea tu huku
wakiendelea kutafuta kazi sehemu mbalimbali wamefanya vituo vyao vya kazi kama
sehemu ya kujiegesha tu!
Sasa nini kama
taifa tunatakiwa kufanya! Ni serikali kuacha kufikiria kushawishi au kuongeza
wanafunzi kusomea taaluma ya ualimu na hata kuwadhamini kwa asilimia mia au
themanini kwa madai kuwa ualimu ni kipaupembele bila kuboresha maslahi ya walimu
hususani mshahara, tukifanya hivyo wanafunzi wenyewe watashawishika kusomea
taaluma hii bila hata kuwapa nafauu ya mikopo vyuoni ama vipi. Maana haina maana
kusema ualimu ni kipaumbele ukampa mwanafunzi nafuu ya mkopo kwa asilimia zote
hizo [100%] bila kujenga mazingira ya mwanafunzi huyo anapohitimu kwenda
kufundisha na si kufikiria kazi nyingine zenye maslahi zaidi, hapo itakuwa ni
sawa tu na kupoteza pesa tu na muda! Maana hakuna sheria inayombana huyo
mwanafunzi kwamba akimaliza lazima akafundishe angalau hata kwa miaka
fulani.
Ushauri wangu
kwa serikali, waangalie namna ya kuboresha maslahi ya walimu, ebu fikiria tu,
nesi mwenye cheti [Certificate] mshahara wake anamzidi mwalimu mwenye stashahada
ya ualimu we unadhani kwanini watu wasikimbilie huko! Au kazi zinazofanana na hizo!
Lakini pia kama inashindwa kuboresha hayo maslahi kwa kiwango kinacholingana na
taaluma nyingine kama sheria, uhasibu, madaktari n.k basi wawe wanaingia
mikataba maalumu na wanafunzi inaoamua kuwafadhiri kwa asilimia miamoja kwa kozi
wanazosema ni kipaumbele kama ualimu, kuwa wataenda kufanya kazi kwa taaluma
walizosomea au watakazopangiwa na serikali kwa muda maalumu, hapa inaweza kuwa
miaka miwili mitatu au itakayoonekana inafaa. Najua ushauri utakuwa mchungu kwa
wanafunzi wanaosomea taaluma fulani kwa ajili ya kupata nafuu ya mikopo utakuwa
mbaya kwao, wanisamehe maana NCHI YANGU KWANZA. Kinyume cha hapo tatizo la
ualimu utakuwa wimbo wa milele katika taifa letu.
No comments:
Post a Comment