Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Thursday, December 27, 2012

TAARIFA YA JESHI [JWTZ] KWA VYOMBO VYA HABARI


'Mwanajeshi aliyepiga picha na lema tutamfukuza kazi ndani ya saa 24' by Nape Nnauye 

source:wapo radio

 Jeshi la Ulinzila Wananchi wa Tanzania limeshitushwa na kusikitishwa kuona taarifa ya mtualiyejitambulisha kuwa askari wa JWTZ wa Kambi ya Monduli, Arusha, iliyochapishwakatika gazeti la Mwanandhi la Desemba 24, 2012 akiwa amevaa sare za JWTZ.
 

 Baada ya kuonahabari hii JWTZ linafanya uchunguzi wa kina ili kutambua kama mtu huyo ni askariwa kweli au la. Kimsingi, JWTZ linafanyauchunguzi wa kumtambua mtu huyo kama kweli ni askari wake kwa sababu zifuatazo;kwanza Jina la mtu huyo halijaandikwa, pili kikosi halisi cha mtu huyohakijaandikwa kwani eneo la Monduli lina vikosi vingi na hakuna kikosikiitwacho Monduli. Lakini pia inatia shaka kuwa mavazi yale siyo yaleyanayotumika kwa wanajeshi wa JWTZ hivi sasa, kuna tofauti kati ya jampa(jacket) na suruali kama ilivyooneshwa katika picha hiyo. Aidha, jampa la sarehiyo pia lina tofauti katika sehemu za mikono, jambo ambalo linatia shaka kamani sare halisi ya JWTZ.
 

 Ilikuwa ra...hisikumtambua mtu huyo kwa kuangalia uso, lakini mtu huyo anayedaiwa kuwa ni askarialifunika paji la uso ili asitambulike. Pamoja na hali hiyo ilivyojitokeza,JWTZ linashughulika kumtambua mtu huyo kwa kutumia mbinu mbalimbali. JWTZlitakapobaini ukweli huo, hatua za kinidhamu zitachukuliwa kutokana na Kanuni zaMajeshi ya Ulinzi kwani, Sheria nambari nne (4) ya mabadiriko ya nane (8)katika Katiba ya Nchi ya mwaka 1992 ibara ya 147(3), mwanajeshi yeyote hatakiwikujihusisha katika masuala ya kisiasa.

 

 Kamailivyoelezwa hapo juu, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limesikitishwakuchapishwa kwa picha hiyo kwani hakunatija wala faida kwa wananchi wa Tanzania zaidi ya kuwatia hofu kuwa Vyombo vyaUlinzi navyo vinashabikia mambo ya siasa, wakati Katiba ya nchi imekataza jambohilo. JWTZ linawaomba wananchi waliangalie jambo hili kwa makini, kwa usalamawa nchi yetu.

Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
MakaoMakuu ya Jeshi, Upanga


No comments:

Post a Comment