Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Sunday, December 23, 2012

UKOSEFU WA MVUA ZA KUTOSHA WASABABISHA NJAA WILAYANI MANYONI


Wilaya ya Manyoni inakabiliwa na njaa kutokana na ukosefu wa mvua kwa muda wa miaka mitatu [3] hayo yamezungumzwa na wananchi wa Manyoni jimbo la Manyoni Magharibi wakati wa mkutano wa Mwenyekiti mpya wa CCM Mkoa wa Singida ndugu Mgana Msindai.


 Naye Mbunge wa jimbo hilo Mh. Paul Lwanji, alisema kuwa mwaka jana wilaya hiyo haikuvuna chakula cha kutosha kutokana na hali ya hewa ya Manyoni na uhaba wa mvua.


Akijibu malalamiko hayo ya wananchi, mwenyekiti huyo, alisema kuwa, Serikali ya Chama Cha Mapinduzi [CCM] imeliona hilo na hivyo imeanza kuleta chakula cha msaada katika wilaya hiyo ambacho kitauzwa kwa bei nafuu tofauti na bei ya juu inayouzwa na wafanyabiashara walanguzi.

Chanzo cha habari: ITV

No comments:

Post a Comment