[Lionel Messi ]
Mshambulizi wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina Lionel
Messi ameshinda tuzo ya Ballon d'Or kwa mwaka wa nne mfululizo.
Messi, 25, alifunga jumla ya magoli 91 mwaka wa 2012 na aliwashinda wachezaji
wengine Andres Iniesta wa Barcelona na Christiano Ronaldo wa Real Madrid.
Licha ya kufunga idadi hiyo ya magoli, timu yake ya Barcelona haikunyakuwa
kombe la ligi kuu ya Uhispania ay kombe la klabu bingwa barani Ulaya mwaka
uliopita.
Abby Wambach, alishinda tuzo kwa upande wa kina dada naye Vicente del Bosque,
akituzwa kuwa kocha bora.
Timu bora ya kwana ilijumuisha wachezaji wanaoshiriki katika ligi ya
Uhispania pekee.
Messi alitangazwa mshindi wa tuzo hiyo ya the Ballon d'Or, tuzo ambayo
hukabithiwa mchezaji bora wa mwaka katika sherehe iliyofanyika mjini Zurich
Messi alikuwa miongoni mwa wachezaji watatu walioteuliwa na jopo la wandishi
wa habari na makocha wa timu za taifa, manaodha wa timu hiyo wakiwa ni pamoja na
Iniesta na Ronaldo.
Mesi sasa ni mchezaji wa kwanza kuwahi kushinda tuzo hiyo ya Ballons d'Or,
kwa miaka minne mfululizo, rekodi anayoshikilia na aliyekuwa mchezaji wa
Ufaransa na rais wa UEFA kwa sasa Michel Platini.
Kikosi cha wachezaji bora wa mwaka 2012
•Iker Casillas (Real Madrid)
•Dani Alves (Barcelona)
•Gerard Pique (Barcelona)
•Sergio Ramos (Real Madrid)
•Marcelo (Real Madrid)
•Andres Iniesta (Barcelona)
•Xabi Alonso (Real Madrid)
•Xavi (Barcelona)
•Cristiano Ronaldo (Real Madrid)
•Radamel Falcao (Atletico Madrid)
•Lionel Messi (Barcelona)
•Dani Alves (Barcelona)
•Gerard Pique (Barcelona)
•Sergio Ramos (Real Madrid)
•Marcelo (Real Madrid)
•Andres Iniesta (Barcelona)
•Xabi Alonso (Real Madrid)
•Xavi (Barcelona)
•Cristiano Ronaldo (Real Madrid)
•Radamel Falcao (Atletico Madrid)
•Lionel Messi (Barcelona)
Habari kwa hisani ya http://www.bbc.co.uk/swahili/michezo/2013/01/130107_ronaldo.shtml?
No comments:
Post a Comment