Baada ya habari za kuvuliwa uanachama kwa wanachama wa Chadema na Baraza la Vijana Chadema [BAVICHA] mmoja wa wanachama hao Habib Mchange amejitokeza na kutoa taarifa kuhusiana na taarifa za kufukuzwa kwake uanacha na hii ndo taarifa yake
HABARI, kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikipigiwa simu na kutumiwa MESEJI kuulizwa juu ya habari za kuvuliwa kwangu uanachama wa BAVICHA na CHADEMA.
jimboni kwangu KIBAHA wamefikia hatua ya kuzusha kuwa NIMEHAMIA CCM na sasa kuna vikundi mbali mbali vya wananchi wanajadili kwa mitazamo tofauti tofauti.
naomba niwaambie leo hapa,
SIJAFUKUZWA CHAMA, mimi ni MWANACHAMA HALALI WA CHADEMA. na wala sijawahi kuitwa wala kuhojiwa na mamlaka yoyote ya chama iliyopewa haki na katiba ya chama kuweza kumvua mwanachama uanachama.
...
kikubwa kuelewa taarifa hizi zinazosambazwa kwa kasi ya ajabu ni za kipotoshaji zenye lengo la kunichafua kisiasa.
hakuna tangazo lolote so far lililotolewa na CHAMA mpaka sasa linalosema nimefukuzwa uanachama.
ni kweli jana nilialikwa kwenye kikao cha kamati tendaji ya BAVICHA, lakini sijaandikiwa kwenye barua yangu ya mwaliko kuwa nimekwenda kuhojiwa ili nifukuzwe chama.
yawezekana waliokuwa kwenye hicho kikao wanasambaza habari hizo, lakini ukweli ni kwamba.
BAVICHA hawajawahi kupewa mamlaka na katiba ya chama chetu kuweza kumfukuza mwanachama uanachama.
cha kuzingatia tu kujua ni kuwa mamlaka pekee za chama zenye kuweza kunivua uanachama ni TAWI LANGU ama KAMATI KUU YA CHAMA.
na ili vyombo hivyo viwili vinivue uanachama ni lazima taratibu za kisheria zilizowekwa kwenye jatiba ya chama chetu zifuatwe. taratibu hizo ni pamoja na kuandaa mashtaka, kunipatia hati ya mashtaka kwa maandishi katika kipindi kisichopungua wiki mbili na kuyajibu kisha kuitwa kwenye kikao cha mahojiano.
nasisitiza BAVICHA hawajawahi kunipatia hati yoyote ya mashitaka na sijawahi kuhojiwa. hizi tuhuma zinazowekwa humu mitandaoni tena kwa lugha za kejeli ni za kuzipuuza.
BAVICHA wangeweza kuwa na uwezo wa kunivua uanachama wa BAVICHA na sio uanachama wa CHADEMA, bahati mbaya sana mpaka leo hii hakuna hata mtu mmoja ambaye ni mwanachama wa BAVICHA wote waliokuwepo humo ni sehemu tu ya wanajumuhiya ya wanachadema wenye rika la umri unaolingana.
kwa hiyo taarifa zozote za kuwa mimi nimevuliwa uanachma na BAVICHA chini ya ndugu HECHE ni za kipotoshaji na hazipo.
Mimi ni MWANACHADEMA halali na nitaendelea kukitumikia changu mpaka hapo itakapokuwa vinginevyo.
sijawahi kuwa na KADI YA UANACHAMA WA BAVICHA hivyo siwezi vuliwa uanachama wangu wa chama kwa kuzingatia umri wangu.
nimeshaandaa malalamiko kwa viongozi wangu wakuu wa chama juu ya upotoshwaji huu unaofanywa na kwa makusudi na baadhi ya viongozi wa BAVICHA katika kile wanachokiita kujihami na uchaguzi ujao wa chama.

No comments:
Post a Comment