Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Wednesday, January 2, 2013

SAJUKI TULIKUPENDA SANA ILA MUNGU AMEKUPENDA ZAIDI

BREAKING NEWS: Taarifa zimetufikia kwamba msanii wa filamu Sajuki (Juma Kilowoko) amefariki dunia alfajiri leo katika hospitali ya Taifa Muhimbili.
Sajuki enzi za uhai wake
 
Msanii wa filamu [Bongo movie]  Sajuki amefariki dunia leo asubuhi  katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
 
Taarifa zinasema kuwa Sajuki alilazwa hapo kwa wiki mbili akiwa anasubiri kupata urahisi wa kusafiri kurudi India baada ya kuanza kusumbuliwa na tatizo la kukosa pumzi na upungufu wa damu, huku jitahada za kutafuta ndege itakayotoa huduma ya gesi ili iweze kumsafirisha hadi India kwenye matibabu ambayo alipangiwa kurudi tena december 2012.
                                         Sajuki akiwa na mke wake wakati wa uhai wake
 
Baada ya taarifa za kifo cha sajuki kusambaa viongozi na wadau mbalimbali wametoa salamu zao kuhusiana na kifo hicho katika mitandao mbalimbali ya kijamii, miongoni mwao akiwemo Mh. Freeman Mbowe [mwenyekiti taifa -Chadema] Mh. Zitto Kabwe [Naibu katibu Bara-Chadema] Shy-Rose Bhanji na Masanja Mkandamizaji
 
Freeman Mbowe katika ukurasa wake wa facebook anasema

"Tunaishi katika nyakati ngumu. Katika sehemu zote za ulimwengu, tunasikia habari nyingi kuhusu misiba na misukosuko ya kijamii hata hivyo hali hakika awezae kuizoea kamwe. Baada ya kuamka asubuhi majira ya saa 12 asubuhi na kuangalia simu yangu ya mkononi nilikuta kuna missed call kama kumi na tano missed call saba zikitoka kwa rafiki yangu wa karibu na ni mdau wa bongo movies kama nilivyo ... mimi niliona itakua ni busara kama nikimpigia na kumuuliza ni yapi yaliyo jili mwanzo wa mwaka 2013.baada ya kumpigia akanipa taarifa unaowahusu watanzania kwa ujumla hasa wapenzi wa bongo movies, kiukweli ni engo kubwa sana. Pole kwa wanafamilia wa marehemu, mke wa marehemu na wote walioguswa na msiba wa ndugu yetu Sajuki hakika hatuwezi pingana na mipango yake Muumba wetu, bali hatuna budi kumuombea makazi mema uko alikotangulia mpendwa wetu. Amina"

 
Sajuki akiwa uwanja wa ndege wa Mwalimu JK Nyerere kwa safari ya kuelekea
India baada ya hali ya afya yake kuwa mbaya


Zitto Kabwe katika ukurasa wake wa Facebook anasema;
"Hali ya Afya ya Sajuki ndiyo ilinisukuma sana kuanza kusaidia wasanii nchini kupata kipato stahili na kazi Yao. Kifo chake kimeniondolea Mtu niliyemtazama kama kishawishi Cha Mimi kupigania haki za Watanzania walio kwenye entertainment industry. Sajuki left an indelible mark in my politics. Pumzika Kwa Amani Juma."

 
 Sajuki akiwa hospitalini huko India kwa matibabu
 
Shy-Rose Bhanji
"Its completely heartbreaking that Wastara has to mourn her beloved Sajuki`s death after being through a lot together: GOD GIVE HER STRENGTH!

Mara ya kwanza kumfahamu Sajuki ilikuwa kupitia post moja kwenye FB iliyobeba picha mbili za Sajuki; kabla na baada ya kusumbuliwa na na maradhi. Niliguswa sana na nilihamasika kuacha ujumbe wangu kumuombea Mungu amsaidie apone haraka.

Siku chache baadae niliskia kwenye Clouds FM kipindi cha Leo Tena, Dina Marios akihamasisha wadau kuchangia kwa hali na mali ili Sajuki aweze kwenda kutibiwa India. Nilihamasika na mimi nilichangia kusaidia azma hiyo.
...

Nilikwenda mbali zaidi (shukrani kwa wadau wengine pia ) kujitolea kuigiza kwenye filamu ambayo ilikuwa imelenga kupata fedha za kusaidia matibabu ya Sajuki. Mhusika Mkuu wa idea hii akiwa Ruge Mutahaba.

Pole sana Wastara, Mungu akupe nguvu katika kipindi hiki...wengi tumeumia na kifo cha Sajuki, lakini Wastara na familia ndio mnayajua zaidi maumivu ya kuondokewa na kipenzi wenu. PUMZIKA KWA AMANI SAJUKI."
 
Sajuki na mke wake mara baada ya kurejea kutoka India kwa matibabu

SALAMA JABIR
"juzi tu j3 nilikua nae katika kipindi cha mkasi leo hatupo nae siamini. Kweli mungu hakosei.... #R.i.p Sajuki Juma Mungu Akulaze mahala pema peponi"
Masanja Mkandamizaji
"I have some bad news. Ndugu yetu SAJUKI amefariki dunia leo alfajiri katika hospitali ya Muhimbili. Bwana ametoa na Bwana ametwaa. Jina lake na lihimidiwe! Tulimpenda, tulijitahidi kufanya kile tulichoweza lakini Mungu amempenda zaidi na amemuita kwake kupumzika.! Thanks kwa support yenu kubwa sana wakati tunatafuta msaada wa matibabu yake. Mungu awabariki sana!"
Taarifa zaidi tutawaletea kadili tutakvyozipata 
NAMI NAPENDA KUWAPA POLE FAMILIA YA SAJUKI NA WAPENZI WAKE WOTE WA KAZI ZAKE
 
SAJUKI TULIKUPENDA SANA! ILA MUNGU AMEKUPENDA ZAIDI- PUMZIKA KWA AMANI SAJUKI
     AMEN

No comments:

Post a Comment