Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Sunday, September 29, 2013

MUZIKI WETU UNA MATUKIO MENGI SANA SANA!!!

MUZIKI  WETU  UNA MATUKIO  MENGI SANA  SANA!!!

    Kama miaka 2  iliyopita  hivi kulikuwa  na  show  ya  X -MASS  MWANZA!!  aaaf kesho yake  26th  ilikuwa  MUSOMA!!  ilikuwa  ni  mimi  na belle 9  na band  fulani hii ya wakongo!!!

  Sasa kiufupi tu ile  show ya 25th ya  X -MASS pale  GOLD CREST  MWANZA  ilifeli hivi(obvious haikutangazwa so wakaifelisha wenyewe waandazi)!!
 lakini sisi mtonyo wetu tulikuwa tumeshabeba bfr!! 

    So  kutokana na hali  ile  yule  big boss akatutengenezea  picha  fulani  hivi  asubuhi ya kesho  yake  tulipoamka  tu!!

  Yeye  alitaka  tukafanye  show  ya bure  musoma  kesho yake  kama kulipizia  show  yake  ya  mwanza  iliyofeli.....
TULIPOKATAA    jamaa  akatumia  UTARIME  WAKE/ UBABE  NA  KUJUANA  NA  WADAU WA MWANZA  AKATUITIA  POLICE  ASUBUHI PALE  HOTELINI...anajua  mwenyewe  alivyowapiga  kiswahili  askari  hadi  wakajaa!!

  Wana  tukabebwa  nini..... haoooooo    hadi  kituoni!!! 
 Sasa  kwakuwa  jana  yake  ilikuwa sikukuu, basi  walikuwa wamekamatwa vijana wengi sana  kwa makosa mbali mbali wakiwa mahabusu ya pale......

   Aisee  vile  tunafika  tu  tunaambiwa  aya  vua  mikanda/viatu/ aaaf ingieni  kule  kwa  wenzenu!!!
sasa  mle  ndani  nikipatazama  na mwanangu belle  9  naona  zile  mbavu mule...duuuh!!!  moyoni sasa nawaza  itakuwaje  kule  ndichi!!

 Aaaf sasa  kiukweli  mm sikuwa na wasi wasi kuhusu mimi,   kiukweli!!  coz  najua  kule wanangu  wanaonielewa na muziki wangu  watakuwa wengi tu lazima!!

 Sasa  wasi wasi    nikawa ninao  kwa  bele 9(watamuelewa??!!)!!  aaf tukiwa  tupo  pale  kaunta  tunaandikisha  maelezo  kule  ndani wana  wakaanza  kuongea

  "aisee  rire  si  riroma  riree..." 
 mwingine  anajibu
 "ee riko  na ribere naini asee  itakuwa  wameshazingua" 
 
wakaedelea  kusema  kwa  sauti  
" wana  msijari  karibuni  humu ni kwa kira  mtu  juzi tu  turikuwa  naa ritwente  pasenti  na daz baba, huku  ni kwa  wote"

Daahh apo tunaandikisha  maelezo  tuna hasira  na  police  wote  wamekaza kama hawatujui...na yule boss  sijui  aliwapanga  vipi  hadi  jamaa wakatukazia  vile!! 
 basi  kuna  police  flani  wa kike  mjeuri  huyo  akamtazama  belle 9  kwa  dharau  aaf akauliza wee jina  lako  nani? anamuuliza  belle  kwa  sauti...

basi  nikasikia  voko  moja  imetoka  mle  ndani  mahabusu....

  "issshhh  ritazame  rire  ridemu  ris....(tusi) eti anauriza belle  9   ni  nani, akati  simu yake  rimejaza  majimbo  yake, yani we dada ni  mus.....(tusi)"

 duuuh  tukamalize  wana tukawa  tunaingia  ndani!!  basi  kufika  tu  tunaingia  kuna  mwana  nakumbuka  akamdaka  belle  fasta  na kumkazia  eti  amvulie culture  fulani  hivi  belle alivaa mkononi!
 belle  akamkazia  aaf wakaanza kupandishiana  pale pale  huyu  akitukana  belle  kajibu nayeye...daaah  nikasema  yeeees  mtoto wa moro  ninja kweli!!

 Basi  kuna  wana  mle  ndani wakaanza zile za "oya  kausheni  kausheni  hawa  wana mjue,  haya  ndiyo  majembe, oyaa  mkatoriki eeee  tulia  apo  chini  msijali  apa  amani  tu!!(hao  wana  wawili  waliokuwa  na sauti  mle  ndani  ya kuweza kuwatuliza  woote  aisee sisahau  sura  zao  hadi  leo, maana walituelewa  sana!!)
 basi tukatulia...

   Huku  nyuma sasa report zimewafikia  wana,  maana jana yake  sikukuu so  mwanza kulikuwa na show  kama nne  hivi sehemu tofauti!!
 alikuwa izzo b, linna,tunda, tip top wote... basi  fasta  pale  kituoni  akaja  madee/barnaba na wana kibao  kuja kujua  kinachoendelea....


   Sasa  mle  ndani aisee kwa haraka  haraka  tulikuwa  sio chini  ya 20 aisee na  zaidi  nahisi,  yani tumebanana sana!!  
asa  kuna  muda  nimekaa  nimesizi  nawaza  tuuu   tunafanyaje  hapa...
basi  nasikia  wana wanaambiana 

"apo  riroma  rinatunga  sheria  apo  rikitoka  nheeee utasikia  ritatoa  kama  ireee  dokta  anakunywa  varuuu...aisee ire  ni kariiii"

     aaf  ananiinamia  ananambia  "ivi pare  uriwazaga  nini  jembe"?  
sasa  mm  si  unajua  nina  mastress    yangu naona  kama anazingua  ivi  ananirushia...ila  ili  niende  nao  sawa inabidi nimjibu...hhhahahahhahahah!!

    Jamaa  mwingine  mara  achungulie  nje  anamuona barnaba  kaunta  akiongea  na  maaskari...anamwambia 
   
" wee banaba wee njoo uwatoe  wana apa, watarara  hapa  hawa  ohooo!! aisee  ira  kabanaba  ni kafupi jamani..."
  yaani ikawa  mwana anamix sana  stori  daah!! kucheka nataka  huku nawaza  mengi!! 
 aaaf  unajua  kuna  zile  mnakaa  aaaf mnagonganisha  macho  mimi  na mwanangu belle aaaf  kama mnaongea kwa ishara  ivi....daah!!!

  Kuna mwana nakumbuka  akanitazamaaaaa  aaaf akasema 
 "ira  riroma  rinaonekana  rijembe" 

 aliposema  ivo  belle  kama naye  akamtazama  kwa kumkazia  ivi  uso wa mbuzi...basi  mwana nikamsikia  tena  eti   "iraa  nyinyi  nyote  majembe  tuuu"
 hahahahha belle   alinicheki  aaf aka-smile  ivii!! 

 nakumbuka  vitu wlivokuwa wakisema mle  ndani.....
 "ira  bere  ire  ngoma sijui  masogange iree naikubariiii sana,
  aaaf  jamaa anaanza kuiimba, sasa akiimba  utacheka aisee...

aaaf anaacha kuimba  anasema " ira  we  dayamondi  hakuwezi wewe...kisha  wanaanza  kubishana  wao  kwa  wao" 

    Aisee mle ndani  kuna watu  wana majanga  nyinyi  daaah!!  kuna  wana yani unakuta  sura  nzima  ana alama  za mapanga  tu  humtazami mara  2, aaaf yeye anakukazia  jicho  tu kinoma  noma!!...

   Baadae  kdg  kuna mwarabu/msomali aliletwa na yeye..basi  vile  anaingizwa  tu na lango kufungwa  daah walimnyang'anyia  kama mpira wa kona!! jamaa alipigwa  ngumi/mateke  fasta  akavuliwa shati  wakalizuia  jamaa!!   nikasema yeees,  wana kweli sisi walituelewa  kama hali  zenyewe  ndiyo  hizi!!! 
 karibu mahabusu  hiyo inaitwa!!!

"eti aisee roma nauza frash  we ukitoka nitoe buku mbiri tu hii frash ina kirakitu ndani"........ hahaha sasa  eti flash  inauzwa aaf ina kila kitu sasa badala iwe empty yeye anasema ina kila kitu...

  NWAYS  yalitokea mengi sana  mle  ndani  hadi tunaletewa msosi  mchana, na wana wakatuzunguka wakisema tunawalinda mle  kwa amani.. na  tukaenjoy  nao sana kuwa nao  kwa  muda ule  wa masaa sio chini ya  matano!!

Finally  tulikuja  toka  kwa  masharti...na  kila  kitu  kikawekwa sawa....sasa  baadae  usiku  tumetulia hotel  na belle 9  ndio  tunaanza  kukumbushiana  sasa  story  za kule..cheka  sana...tukagonga  macheers nini....ikabaki  mumbukumbu  tuu!!

Juzi  nilikutana  na  mwana  mmoja  wapo (GEITA  KWENYE  SHOW)ni  mwana mmoja kati ya  wale  tuliokuwa  ndani siku  hiyo!!  TULICHEKA  NA KUENJOY  PAMOJA!!!

(PICHANI  NI  MASAA KADHAA  BAADA  YA  KUWA  HURU)!!

-Nikijaga  kuyaimba  haya kwenye  ngoma  zangu  naambiwa  NAKUSANYA  HABARI  ZA KITAIFA  NA KIMICHEZO...HAHAHHAHAHAHHAHAHH  BONGO BANA!!!


"Wakati  mwingine  tunachukuliana  poa  ila tuna nguvu sana  kwa  mtaa/ tunapendwa  sana/tuna  face  a lot  of  troubles"...bt  we  still  kip t real...ONE!!!Roma ameamua kushare nasi story yake, kupitia ukurasa wake wa facebook, ameandika hivi, "Kama miaka 2 iliyopita hivi kulikuwa na show ya X -MASS MWANZA!! aaaf kesho yake 26th ilikuwa MUSOMA!! ilikuwa ni mimi na belle 9 na band fulani hii ya wakongo!!!

Sasa kiufupi tu ile show ya 25th ya X -MASS pale GOLD CREST MWANZA ilifeli hivi(obvious haikutangazwa so wakaifelisha wenyewe waandazi)!!
lakini sisi mtonyo wetu tulikuwa tumeshabeba bfr!!

So kutokana na hali ile yule big boss akatutengenezea picha fulani hivi asubuhi ya kesho yake tulipoamka tu!!

Yeye alitaka tukafanye show ya bure musoma kesho yake kama kulipizia show yake ya mwanza iliyofeli.....
TULIPOKATAA jamaa akatumia UTARIME WAKE/ UBABE NA KUJUANA NA WADAU WA MWANZA AKATUITIA POLICE ASUBUHI PALE HOTELINI...anajua mwenyewe alivyowapiga kiswahili askari hadi wakajaa!!

Wana tukabebwa nini..... haoooooo hadi kituoni!!!
Sasa kwakuwa jana yake ilikuwa sikukuu, basi walikuwa wamekamatwa vijana wengi sana kwa makosa mbali mbali wakiwa mahabusu ya pale......

Aisee vile tunafika tu tunaambiwa aya vua mikanda/viatu/ aaaf ingieni kule kwa wenzenu!!!
sasa mle ndani nikipatazama na mwanangu belle 9 naona zile mbavu mule...duuuh!!! moyoni sasa nawaza itakuwaje kule ndichi!!

Aaaf sasa kiukweli mm sikuwa na wasi wasi kuhusu mimi, kiukweli!! coz najua kule wanangu wanaonielewa na muziki wangu watakuwa wengi tu lazima!!

Sasa wasi wasi nikawa ninao kwa bele 9(watamuelewa??!!)!! aaf tukiwa tupo pale kaunta tunaandikisha maelezo kule ndani wana wakaanza kuongea

"aisee rire si riroma riree..."
mwingine anajibu
"ee riko na ribere naini asee itakuwa wameshazingua"

wakaedelea kusema kwa sauti
" wana msijari karibuni humu ni kwa kira mtu juzi tu turikuwa naa ritwente pasenti na daz baba, huku ni kwa wote"

Daahh apo tunaandikisha maelezo tuna hasira na police wote wamekaza kama hawatujui...na yule boss sijui aliwapanga vipi hadi jamaa wakatukazia vile!!
basi kuna police flani wa kike mjeuri huyo akamtazama belle 9 kwa dharau aaf akauliza wee jina lako nani? anamuuliza belle kwa sauti...

basi nikasikia voko moja imetoka mle ndani mahabusu....

"issshhh ritazame rire ridemu ris....(tusi) eti anauriza belle 9 ni nani, akati simu yake rimejaza majimbo yake, yani we dada ni mus.....(tusi)"

duuuh tukamalize wana tukawa tunaingia ndani!! basi kufika tu tunaingia kuna mwana nakumbuka akamdaka belle fasta na kumkazia eti amvulie culture fulani hivi belle alivaa mkononi!
belle akamkazia aaf wakaanza kupandishiana pale pale huyu akitukana belle kajibu nayeye...daaah nikasema yeeees mtoto wa moro ninja kweli!!

Basi kuna wana mle ndani wakaanza zile za "oya kausheni kausheni hawa wana mjue, haya ndiyo majembe, oyaa mkatoriki eeee tulia apo chini msijali apa amani tu!!(hao wana wawili waliokuwa na sauti mle ndani ya kuweza kuwatuliza woote aisee sisahau sura zao hadi leo, maana walituelewa sana!!)
basi tukatulia...

Huku nyuma sasa report zimewafikia wana, maana jana yake sikukuu so mwanza kulikuwa na show kama nne hivi sehemu tofauti!!
alikuwa izzo b, linna,tunda, tip top wote... basi fasta pale kituoni akaja madee/barnaba na wana kibao kuja kujua kinachoendelea....


Sasa mle ndani aisee kwa haraka haraka tulikuwa sio chini ya 20 aisee na zaidi nahisi, yani tumebanana sana!!
asa kuna muda nimekaa nimesizi nawaza tuuu tunafanyaje hapa...
basi nasikia wana wanaambiana

"apo riroma rinatunga sheria apo rikitoka nheeee utasikia ritatoa kama ireee dokta anakunywa varuuu...aisee ire ni kariiii"

aaf ananiinamia ananambia "ivi pare uriwazaga nini jembe"?
sasa mm si unajua nina mastress yangu naona kama anazingua ivi ananirushia...ila ili niende nao sawa inabidi nimjibu...hhhahahahhahahah!!

Jamaa mwingine mara achungulie nje anamuona barnaba kaunta akiongea na maaskari...anamwambia

" wee banaba wee njoo uwatoe wana apa, watarara hapa hawa ohooo!! aisee ira kabanaba ni kafupi jamani..."
yaani ikawa mwana anamix sana stori daah!! kucheka nataka huku nawaza mengi!!
aaaf unajua kuna zile mnakaa aaaf mnagonganisha macho mimi na mwanangu belle aaaf kama mnaongea kwa ishara ivi....daah!!!

Kuna mwana nakumbuka akanitazamaaaaa aaaf akasema
"ira riroma rinaonekana rijembe"

aliposema ivo belle kama naye akamtazama kwa kumkazia ivi uso wa mbuzi...basi mwana nikamsikia tena eti "iraa nyinyi nyote majembe tuuu"
hahahahha belle alinicheki aaf aka-smile ivii!!

nakumbuka vitu wlivokuwa wakisema mle ndani.....
"ira bere ire ngoma sijui masogange iree naikubariiii sana,
aaaf jamaa anaanza kuiimba, sasa akiimba utacheka aisee...

aaaf anaacha kuimba anasema " ira we dayamondi hakuwezi wewe...kisha wanaanza kubishana wao kwa wao"

Aisee mle ndani kuna watu wana majanga nyinyi daaah!! kuna wana yani unakuta sura nzima ana alama za mapanga tu humtazami mara 2, aaaf yeye anakukazia jicho tu kinoma noma!!...

Baadae kdg kuna mwarabu/msomali aliletwa na yeye..basi vile anaingizwa tu na lango kufungwa daah walimnyang'anyia kama mpira wa kona!! jamaa alipigwa ngumi/mateke fasta akavuliwa shati wakalizuia jamaa!! nikasema yeees, wana kweli sisi walituelewa kama hali zenyewe ndiyo hizi!!!
karibu mahabusu hiyo inaitwa!!!

"eti aisee roma nauza frash we ukitoka nitoe buku mbiri tu hii frash ina kirakitu ndani"........ hahaha sasa eti flash inauzwa aaf ina kila kitu sasa badala iwe empty yeye anasema ina kila kitu...

NWAYS yalitokea mengi sana mle ndani hadi tunaletewa msosi mchana, na wana wakatuzunguka wakisema tunawalinda mle kwa amani.. na tukaenjoy nao sana kuwa nao kwa muda ule wa masaa sio chini ya matano!!

Finally tulikuja toka kwa masharti...na kila kitu kikawekwa sawa....sasa baadae usiku tumetulia hotel na belle 9 ndio tunaanza kukumbushiana sasa story za kule..cheka sana...tukagonga macheers nini....ikabaki mumbukumbu tuu!!

Juzi nilikutana na mwana mmoja wapo (GEITA KWENYE SHOW)ni mwana mmoja kati ya wale tuliokuwa ndani siku hiyo!! TULICHEKA NA KUENJOY PAMOJA!!!

(PICHANI NI MASAA KADHAA BAADA YA KUWA HURU)!!

-Nikijaga kuyaimba haya kwenye ngoma zangu naambiwa NAKUSANYA HABARI ZA KITAIFA NA KIMICHEZO...HAHAHHAHAHAHHAHAHH BONGO BANA!!!


"Wakati mwingine tunachukuliana poa ila tuna nguvu sana kwa mtaa/ tunapendwa sana/tuna face a lot of troubles"...bt we still kip t real...ONE!!!"

GAZETI LA MWANANCHI NA MTANZANIA YAFUNGIWA

WAKATI wadau mbalimbali wa sekta ya habari wakifanya harakati za kuitaka serikali kubadilisha Sheria ya Magazeti ya Mwaka 1976, serikali juzi imeyafungia magazeti ya Mwananchi na Mtanzania.
Sheria ya Magazeti ya Mwaka 1976 inampa ruhusa waziri mwenye dhamana ya habari kupiga marufuku uchapaji na matumizi ya gazeti lolote ambalo anafikiri liko kinyume cha masilahi ya umma.
 
Gazeti la Mtanzania limefungiwa kwa siku 90, huku Mwananchi likifungiwa kwa siku 14, yote adhabu zao zimeanza juzi Septemba 27, 2013.
Uamuzi huo wa serikali umekuja mwaka mmoja baada ya kufanya hivyo kwa gazeti la Mwanahalisi ililolifungia kwa muda usiojulikana, kwa kuandika habari na makala ilizodai ni za uchochezi, uhasama na uzushi.
 
Taarifa iliyosambazwa kwa vyombo vya habari jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Assah Mwambene, adhabu hiyo imeanza juzi.
 
Taarifa hiyo imebainisha kuwa magazeti hayo yamepewa adhabu hizo kutokana na mwenendo wa magazeti hayo kuandika habari na makala za uchochezi na uhasama, kwa nia ya kusababisha wananchi wakose imani kwa vyombo vya dola, hivyo kuhatarisha amani na mshikamano uliopo nchini.
 
Mwananchi
Mwambene alisema tangazo la kufungiwa kwa gazeti hilo limetangazwa kwa Tangazo la Serikali namba 333 la Septemba, 27, 2013.
 
Alisema Mwananchi limepewa adhabu hiyo kutokana na hivi karibuni kuchapisha habari zenye mwelekeo wa uchochezi na uvunjifu wa amani.
 
Taarifa hiyo iliongeza kuwa Julai, 17, 2013 katika toleo Namba 4774, lilichapisha habari isemayo: ‘Mishahara mipya serikalini 2013’, kwa kuchapisha waraka uliozuiliwa kwa matumizi ya vyombo vya habari, kwakuwa ulikuwa siri na haukupaswa kuchapishwa magazetini.
 
Alisema katika toleo la Jumamosi, la Agosti, 17, 2013 lilichapisha habari yenye kichwa kisemacho: ‘Waislamu wasali chini ya ulinzi mkali.”
 
Mwambene alisema habari hiyo ilikolezwa na picha ya mbwa mkali mwenye hasira, ambapo picha hiyo ilitoa tafsiri ya kuwa Jeshi la Polisi lilipeleka mbwa katika maeneo ya ibada ya waumini wa dini ya Kiislamu.
 
Alisema jambo hilo halikuwa la ukweli kwa sababu Jeshi la Polisi katika doria siku hiyo halikupeleka mbwa katika maeneo ya misikiti.
 
Alibainisha kuwa serikali na Jeshi la Polisi linaheshimu na kuzingatia maadili ya dini ya Kiislamu na haliwezi kupitisha au kuingiza mbwa katika maeneo ya ibada.
 
Aliongeza kuwa kuchapisha habari hiyo iliyokolezwa na picha ya mbwa ni uchochezi wa kulichonganisha Jeshi la Polisi na waumini wa dini ya Kiislamu. Mbwa ni najisi, hapaswi kuingia katika maeneo ya ibada.
 
Mwananchi wangoja barua
Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili, Mhariri Mtendaji Mkuu wa Mwananchi, Bakari Machumu, alisema mpaka jana jioni hawakuwa wamepata barua hiyo na wanaisubiri ili waangalie hatua za kuchukua.
 
Machumu alisema wataijibu serikali kulingana na hoja walizowaandikia na hawatafanya hivyo kupitia tamko la Mkurugenzi wa Idara ya Habari alilolitoka katika mkutano wake na waandishi wa habari jana.
“Siwezi kukueleza hatua tutakazozichukua dhidi ya uamuzi wa serikali mpaka pale watakapotuandikia barua, mimi nimeona tamko lakini hawajatuletea barua rasmi,” alisema.
 
Kibano cha Mtanzania
Mwambene alisema Mtanzania limefungiwa kutochapishwa kwa kuchapisha habari zenye uchochezi na serikali inadai imeshalionya mara nyingi lirekebishe mtindo wake wa uandishi wa kichochezi na lizingatie maadili, sheria na kanuni za fani ya habari.
 
Alisema pamoja na kuonywa, gazeti hilo halikuonesha kuzingatia maelekezo ya Msajili wa Magazeti.
Mwambene alisema katika toleo Namba 7262 la Machi 20, 2013, liliandika habari yenye kichwa kisemacho: ‘Urais wa damu’.
 
Juni 12, 2013,toleo Namba 7344, lilichapisha makala isemayo: ‘Mapinduzi hayaepukiki.’
Alisema Septemba 18, 2013 katika toleo Namba 73414 ukurasa wa mbele lilichapisha kichwa cha habari kisemacho: ‘Serikali yanuka damu.’
 
Alibainisha kuwa taarifa hiyo ya serikali ilikolezwa na picha zilizounganishwa kwa ustadi mkubwa, kwa kutumia kompyuta kutapakaza rangi nyekundu mithili ya damu nyingi kumwagika.
 
Mwambene alisema katika habari hiyo gazeti hilo limedai bila uthibitisho kuwa Jeshi la Polisi linahusika na wahanga walioumizwa na watu wasiojulikana kwa kumwagiwa tindikali na waliovamiwa na kujeruhiwa vibaya.
 
Aliongeza kuwa gazeti hilo limeishutumu serikali kuwa goigoi katika kushughulikia matukio yenye sura ya kigaidi.
 
Mwambene alisema habari hiyo ni ya kichochezi na ina lengo la kuwafanya wananchi wavichukie vyombo vya ulinzi na usalama, wavione kuwa haviwasaidii.
Alibainisha kuwa kutokana na makosa yaliyotajwa hapo juu, serikali imelifungia gazeti la Mtanzania kutochapishwa kwa muda wa siku tisini (90) kwa Tangazo la Serikali Namba 332 la Septemba 27, 2013.
 
Mtanzania wang’aka
Mtendaji Mkuu wa New Habari 2006, Hussein Bashe, alisema uamuzi huo wa serikali si wa haki na si sahihi.
“Wamelifungia kimya kimya, tarehe 27, hatujaona barua wala hatujaitwa, hii inashangaza sana. Tumeiona katika mitandao, hii imetusikitisha. Hii ni taswira ya aina ya viongozi tulionao katika nchi hii, wizara hiyo hiyo naibu waziri wake alitutaka tuandike barua ya kuomba radhi kutokana na stori yetu, tulifanya hivyo. .. lakini leo mkurugenzi ametuandikia barua ya kutufungia,” alisema Bashe.
Bashe alisema adhabu hiyo inawapa funzo la kufanya kazi na aina ya viongozi na watendaji wa serikali wanaoamua mambo bila kuwahoji watuhumiwa.
“Nawaomba wenzangu tuungane kupambana na sheria hii kandamizi, la sivyo wataendelea kuitumia vibaya,” alisema.
 
Sheria ya Magazeti
Sheria ya Magazeti ya Mwaka 1976 inampa ruhusa waziri mwenye dhamana ya habari mamlaka makubwa ya kuweza kupiga marufuku uchapaji na matumizi ya gazeti lolote ambalo anafikiri liko kinyume cha masilahi ya umma.
 
Kwa vile sheria haitoi orodha halisi ya vigezo vya kutumika ili kupiga marufuku, inampa waziri hiari ambayo anaweza kuitumia bila sababu za msingi, ama hata kuitumia kwa sababu binafsi kunyamazisha magazeti yaliyo makini na uandishi wa habari za kitafiti. Katika sehemu ya pili ya sheria hii, kipengele cha 5(2), waziri anapewa mamlaka kama ya kutoa tangazo kupitia Gazeti la Serikali, kulizuia gazeti lolote kufanya kazi zihusianazo na baadhi ya vipengele ama vipengele vyote vya sehemu hii, aidha moja kwa moja ama kwa kuzingatia masharti ambayo waziri ataona yanafaa.
 
Katika mwelekeo huohuo, kipengele cha 25(1) cha sheria hiyohiyo kinampa waziri uwezo wa kupiga marufuku uchapaji wa gazeti lolote, wakati wowote atakaoona inafaa. Kipengele kinasema:
‘Pale waziri anapoona kwamba ni kwa masilahi ya umma, ama ni kwa masilahi ya amani na utulivu kufanya hivyo, anaweza, kwa kutoa agizo kupitia Gazeti la Serikali kuagiza kwamba gazeti lililotajwa katika agizo hilo liache kuchapwa tangu tarehe ile iliyoelezwa katika agizo.
 
Mamlaka hayo makubwa aliyonayo waziri yanaweza kutumiwa kinyume cha masilahi ya umma, tofauti na ilivyokusudiwa.
 
Wakitoa maoni yao kuhusu kufungiwa kwa magazeti hayo, Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, Zitto Kabwe na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa chama hicho, John Mnyika, wamelaani kitendo cha kufungiwa kwa magazeti ya Mwananchi na Mtanzania, wakisema ni dalili za utawala unaoanguka.
 
Walisema hayo walipokuwa wakihutubia mkutano wa hadhara eneo la Ugindoni, Kata ya Mji Mwema, Jimbo la Kigamboni. Wamewaomba wananchi kutokubali jambo hilo, kwani halikubaliki. Zitto alisema kwamba watawala wanaendelea kupata nguvu ya kuendelea kufungia vyombo vya habari kwa sababu ya ukimya wa wananchi.
 
“Wananchi mkichukua mamlaka yenu kama inavyosema Katiba ya nchi, chukueni mamlaka yenu hata mambo ya hovyo wanayofanya CCM bungeni yatakwisha. Leo nikiwa jukwaani hapa nimesikia magazeti ya Mwananchi na Mtanzania yamefungiwa, yaani watawala walipofungia MwanaHalisi na wananchi mkakubali kuwa kimya, wanaweza kufungia magazeti yote ili yaache kuripoti habari.
 
Via: Tanzania Daima

Monday, September 23, 2013

WARAKA WA SERIKALI WASAMBAZWA, WALIMU WAKUU MARUFUKU KUWA VIONGOZI WA VYAMA VYA WAFANYAKAZI

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni SefueSERIKALI imewakataza watumishi wake waandamizi wakiwemo wanaoongoza mashirika ya umma, wakala na taasisi zake kuwa viongozi ndani ya vyama vya wafanyakazi na kuonya kuwa, atakayekiuka agizo hilo atashushwa cheo au kuchukuliwa hatua nyingine za kinidhamu.
 
Kwa mujibu wa waraka wa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, wa Aprili mosi, mwaka huu, ambao hawapaswi kujiunga na vyama hivyo ni pamoja wakuu wa idara, vitengo,  walimu wakuu (shule za msingi),  wakuu wa shule za sekondari, wakuu wa vyuo na wakaguzi wa shule.
 
Sehemu ya waraka huo inasomeka; “Hairuhusiwi kwa mtu ambaye ameajiriwa katika taasisi za umma akiwa mwenye nyadhifa ya juu wakati huo huo awe kiongozi wa vyama vya wafanyakazi.”
Hata hivyo, wakati Balozi Ombeni akitoa maelezo hayo kupitia waraka huo, Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Ezekiah Oluoch, amezungumzia suala hilo akisema, serikali inapingana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Ibara 20.
 
 
“Ibara ya 20 inatoa Uhuru wa mtu yeyote, kikundi chochote kujiunga ama kuunda na chama chochote kinachotetea imani, masilahi au mawazo yake ambayo ndivyo vitu vya msingi, “Katika huu waraka , nawazungumzia walimu wakuu, wakuu wa shule na wakaguzi wa shule . Hawa hawatungi sera, kuwaweka katika kifungu hiki ni makosa,  sheria ya Bunge haipaswi kupingana na Katiba ambayo ndiyo sheria mama. Kwa hiyo sheria hiyo haiwahusu kwa kuwa wanaotunga sera ni makatibu wakuu na wakurugenzi kwa niaba ya serikali.
 
Kaimu  Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Ezekiah Oluoch“Chini ya Sheria kuna kanuni ambayo haipaswi kupingana na sheria ya Bunge. Chini ya kanuni kuna nyaraka (miongozo). Waraka huu ni batili unapingana na kifungu cha 9 (6) (b) (i) (ii) cha sheria ya ajira na uhusiano kazini ya mwaka 2004.
“Waraka , pia unapingana na kifungu 30 na 31 vya sheria ya majadiliano ya pamoja kwenye utumishi wa umma ya mwaka 2003 kinachowataja wawakilishi wa vyama vya wafanyakazi kushiriki katika mabaraza ya wafanyakazi “Kanuni ya kudumu kifungu F.22 na 23 imezuia baadhi ya watu kuwa viongozi ndani ya vyama vya wafanyakazi  ambacho pia ni batili kwa kuwa kinapingana na sheria ya Bunge.
 
 
Kutokana na kutofautiana huko kati ya Katibu Mkuu Kiongozi kupitia waraka wake huo na CWT, chama hicho cha walimu kimepanga kumuandikia Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kumuarifu kwamba waraka ni batili na hivyo amshauri mtoa waraka aufute baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wanachama wao kudai kuingiliwa uhuru wao.
 
 
“Tumepokea barua kutoka kwa wanachama wanaolalamikia waraka huu kwamba kunaingilia uhuru wao. Baada ya kupata malalamiko hayo, tunayo haki ya kuupeleka mahakamani ikiwa Mwanasheria Mkuu hatamshauri mhusika kuufuta,” anaeleza kiongozi huyo wa CWT.
 
 
Katika hatua nyingine, Septemba 2013, CWT na Serikali vinatarajia kukutana kwa majadiliano ikielezwa kwamba matarajio ya chama hicho cha walimu ni kuwapo kwa ongezeko la mshahara angalau kwa kiwango cha asilimia 65.
 
Katika Afrika Mashariki imewahi kushuhudiwa walimu nchini Kenya wakishiinikiza serikali yao kuongeza mishahara ya walimu na katika kushinikiza mgomo wa siku kadhaa ulifanyika hadi serikali kukubaliana na walimu hao.

via: Raia Mwema

EPUKA UTAPELI HUU

 
Matapeli hayo yamekuwa yakitumia account mbalimbali kama inavyoonekana hapa, wakitumia account ya Airtel Tanzania, huu ni utapeli, wala usikubali, hebu soma utapeli huo na chini yake kuna taarifa ya serikali kukana kuzitambua taasisi hizo, na usisahau kulike au kushare ili na rafiki, ndugu zako na jamaa waione hii wasiingie katika utapeli huu,
 
 
 
TAMKO LA SERIKALI KUHUSU MIKOPO YA AINA HIYO
 
 
SHARE NA LIKE POST HII KWA WENGINE

Friday, September 20, 2013

AGNESS MASOGANGE NA MWENZAKE WAACHIWA KWA DHAMANA

Johannesburg. Watanzania Agness Masogange na Melisa Edward waliokamatwa kwa kutuhumiwa kubeba dawa za kulevya huko Afrika Kusini wameachiwa kwa dhamana.
 
Mkuu wa Kitengo cha Dawa za Kulevya Afrika Kusini, Kamishna Toto Mangaleni aliithibitishia Mwananchi jana kuwa watuhumiwa hao wameachiwa kwa dhamana,lakini wataendelea kubaki Afrika Kusini wakati kesi yao ikiendelea.

 
Mangaleni alisema wanawake hao ambao juzi pia walipanda kizimbani, walipata dhamana hiyo jana kutoka Mahakama Kuu ya Gauteng iliyoko eneo la Kempton Park jijini Johannesburg.
 
Hata hivyo, Kamishna Mangaleni alisema hawezi kuzungumzia zaidi kuhusu kesi hiyo kwa sababu hataki kuharibu uchunguzi ambao unaendelea dhidi ya Watanzania hao, ambao ni wasanii.

Marafiki wa karibu wa Masogange wanaoishi maeneo ya Midland Johannesburg ambao walikataa kunukuliwa majina yao, walithibitisha kuwa wanawake hao wameachiwa kwa dhamana.
 
 
“Ni kweli wameachiwa leo asubuhi. Lakini hatuwezi kuongelea kwa kina habari hizi kwa sababu hatutaki matatizo na polisi. Hii kesi bado inaendelea na wataendelea kubaki hapa hadi kesi yao itakapomalizika,” alisema mmoja wa marafiki zake.

 
Naye Masogange aliandika kwenye mtandao wa ‘Facebook’.
“Namshukuru Mungu nimeamini wewe ulikuwa pamoja na mimi katika maombi yangu na nashukuru kwa wote mliokuwa mkiniombea Mungu kapokea maombi yenu.”

 
Masogange na Melissa walikamatwa Julai 2 mwaka huu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo jijini Johannesburg wakiwa wana mabegi sita makubwa ya dawa zinazoaminika kuwa ni `Crystal Methyl Amphetamine’.
 
Naye Mkuu wa Kitengo cha Polisi cha Kuzuia na Kudhibiti Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa aliiambia Mwananchi jijini Dar es Salaam kuwa alikuwa amepata taarifa za kuachiwa kwa wasichana hao, lakini alikuwa anawasiliana na watu wa Afrika Kusini ili kupata uhakika.
 
Nzowa, hata hivyo alilidokeza gazeti hili juzi kuwa kuna uwezekano wanawake hao wangepata dhamana au kufungwa kifungo chepesi kwani dawa walizokamatwa nazo ni kemikali zinazotumika kutengeneza dawa za aina tofauti kwa matumizi ya binadamu ingawa pia na dawa za kulevya.
 
                              
Mamlaka yapinga uamuzi wa Mahakama
 
Msemaji wa Mamlaka za Huduma za Mapato Afrika Kusini(SARS), Marika Muller alisema wana uhakika asilimia 100 kuwa akina Masogange walikamatwa na dawa za kulevya.
“Timu yetu ilifanya kazi vizuri na ilitambua kuwa mzigo huo ulikuwa wa dawa za kulevya ila tunaiachia mahakama kuendelea na uchunguzi wake,” aliongeza Muller.
 
Chanzo: Mwananchi

Tuesday, September 17, 2013

MCHINA WA NAPE MATATANI

CHADEMA yamshitaki balozi wa China nchini baada ya kushiriki mkutano wa CCM.  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemshtaki Balozi wa China nchini, Dk. Lu Youging kwa Umoja wa Mataifa (UN) kwa kujihusisha na siasa katika majukwaa nchini kitendo ambacho ni hatari katika uhusiano wa diplomasia kati ya Tanzania na China. Pia kimemshtaki kwa Serikali ya China na ya Tanzania kikidai kitendo cha balozi huyo ni kukiuka Mkataba wa Kidiplomasia wa Vienna (Vienna Convention of Diplomatic Reletions of 1964 ibara ya 41 (1-3) ambao unasimamia sheria za nchi wanachama w Umoja wa Mataifa. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Chadema, Ezekiel Wenje alisema kitendo cha Balozi wa China, Dk. Youging kujihusisha na siasa za uenezi katika Chama cha Mapinduzi (CCM) ni kosa kubwa kimataifa na amepoteza sifa za kushikilia nafasi hiyo. Wenje ambaye pia ni Mbunge wa Nyamagana (CHADEMA) na Waziri Kivuli wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa alisema balozi huyo amevunja sheria za Mkataba wa Vienna ambao unasimamia sheria za nchi wanachama wa UN. Alisema kifungu alichovunja kinakataza Balozi yeyote kujihusisha na shughuli nyingine ambazo haziendani na majukumu ya uwakilishi wa nchi na nchi. Wenje alisema balozi huyo anapaswa kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kama inavyoelekezwa katika mkataba wa Vienna kwamba ikiwa balozi atakiuka mkataba huo atakosa sifa na ataondolewa kinga aliyonayo na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Alisema: “Jambo hili katika macho ya diplomasia, limevunja misingi na taratibu za ushirikiano wa kimataifa, wenye nia njema kwa wananchi wa pande mbili, baina ya nchi na nchi na katika ngazi ya serikali. “Kwanza ni taswira ya dharau ya hali ya juu ambayo Balozi wa China ameamua kuwaonyesha Watanzania, hatuamini kwamba amepungukiwa na uwezo kiasi gani lakini anapaswa kukumbushwa aweze kuheshimu mipaka ya majukumu na wajibu wa diplomasia kwa nafsi ya balozi anapokuwa nchi ya ugenini. “Balozi huyu anapaswa kukumbushwa kuwa uhusiano wa vyama, kwa maana ya Chama cha Kikomunisti cha China na CCM hata kama ungekuwa mzuri kiasi gani hauna mwingiliano na uhusiano wa Serikali ya Tanznaia na China. “Hatutaki kuamini kuwa serikali ya China imemtuma Balozi Youquing kuja nchini kufanya kazi za ukatibu mwenezi wa CCM, tumesikitishwa heshima aliyopewa na Watu wa China ameidharau na amevuka mstari ambao hakuna mwanadiplomasia yeyote makini anayeheshimu uhusiano baina ya nchi na nchi angejaribu kufanya hivyo. “Mstari aliouvuka balozi huyu umefafanuliwa wazi katika Mkataba wa Vienna Convention wa 1961 hasa katika kifungu cha 41(1) na 3, katika masuala yanayohusu uhusiano na kinga za mabalozi, kwamba ni marufuku kwa mwanadiplomasia yeyote kuingilia siasa za ndani za nchi mwenyeji wake. “Chadema tunachukua hatua dhidi ya balozi huyo kujihusisha na chama cha siasa kwa kuvaa kofia ya CCM na kuelezea mambo ambayo hayakupaswa kusemwa kwenye majukwaa ya siasa. “Kwanza tunaandika barua tatu, moja itakwenda Serikali ya China, ya pili itakwenda UN na nyingine itakwenda Serikali ya CCM ambayo ndiyo imempeleka huko mikoani. “Barua hizo zitakuwa zinataka kueleza msimamo wa tukio hilo la balozi wa China nchini kujihusisha na siasa za majukwaani na kuvaa nguo za CCM, tunataka kujua hatua gani zitakazochukuliwa haraka kabla ya Chadema hatujapendekeza hatua za kuchukua. “Hii ni hatari kwa balozi huyo kujiingiza kwenye siasa kitendo kinachosababisha kuhatarisha uhusiano uliopo kati ya wawekezaji wa China nchini kwa sababu wananchi wanaweza kutafsiri vibaya. “Kwa mfano kuna maeneo ni ngome za Chadema na pale kuna wawekezaji wa China wanaweza kukataa kutoa ushirikiano wakidai ni wapo mlengwa wa CCM, pia ni hatari chama kingine kitapokuja kushika dola hakutakuwa na uhusiano mzuri. “Tutaambatanisha ushahidi wa kutosha katika barua hizo ikiwa ni pamoja na picha za mnato na video, maneno aliyotamka kwenye mkutano, picha inayoonyesha akiwa amveaa sare za CCM na jinsi anavyocheza”. Picha zilizonyeshwa kwa waandishi wa habari zilionyesha Balozi Youging akiwa katika mikutano mbalimbali ya CCM maeneo ya Kishapu, Shinyanga na Kahama. Katika picha hizo balozi huyo alionekana amevaa sare za CCM, akihutubia na kuendesha baiskeli akiwa na viongozi wa chama hicho akiwamo Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye. Kwa mara ya kwanza balozi huyo aliibukia katika mkutano waCCM uliofanyika Shinyanga huku akishangiliwa na wananchi alipojaribu kuzungumza kisukuma. CCM yazungumza Wakati huohuo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kimesikitishwa na hatua ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kumshutumu Balozi wa China, Dk. . Lu Youqing kwa kuhudhuria mikutano ya CCM. Kimewataka watanzania kupuuza madai ya Chadema kikisema hayana msingi kwa maendeleo ya taifa na watu wake. Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alikuwa akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Mwandoya wilayani Meatu. Alisema ni wazi Chadema kinataka kutumia matatizo ya wananchi kuyageuza agenda ya siasa. Chadema haina budi itambue kuwa chama tawala cha China (CPC) kimekuwa na urafiki wa muda mrefu na CCM ikizingatia Balozi Dk. Lu pia ni kiongozi wa chama hicho. Nape alisema hatua ya Balozi huyo kuhudhuria mkutano huo ni mafanikio ya ziara ya iliyofanywa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana China mapema mwaka huu. “Balozi Dk. Lu amekuja kuleta ukombozi kwa watanzania hasa wa Kanda ya Ziwa kwa kuleta wawekezaji katika Mkoa wa Shinyanga kwa kujenga viwanda wa nyuzi, pamba, nyama, maji na ngozi ambako ajira zaidi ya 1000 zitapatikana. “Watanzania wapuuze madai haya kwani si dhambi kwa Balozi wa China kuhudhuria mkutano wa CCM… urafiki wetu hakuanza leo ni wa muda mrefu katika historia ya nchi hizi mbili tangu na baada ya Uhuru,” alisema Nape. Nape alisema CCM imepitaka kila eneo la yakiwamo majimbo yanayoongozwa na wapinzani na kubaini kuwapo changamoto nyingi. Aliitaka Chadema kwenda kutatua haraka matatizo hayo badala ya kufanya mikutano Dar es Salaam pekee. Wiki iliyopita akiwa mjini Shinyanga Balozi Dk. Lu Youqing, alihudhuria mikutano ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kusema kuwa hakuna chama imara kama hicho. -MtanzaniaCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kuwa Balozi wa China nchini, Lu Youqing, amekiuka mkataba wa kimataifa wa Vienna kwa kuanza kushiriki kazi ya uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kama alivyoonekana akiwa mkoani Shinyanga.
 
Wakati CHADEMA ikitoa madai hayo, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa imekiri balozi huyo kuvunja mkataba huo unaoongoza uhusiano wa kidiplomasia na kuahidi kuchukua hatua.
 
Septemba 12 mwaka huu, balozi huyo alihudhuria mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika uwanja wa Shycom mkoani Shinyanga na baadaye katika eneo la mnada wa Mhunze Jimbo la Kishapu.
Balozi Youquing alitambulishwa kwa wananchi na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, na kisha kuwahutubia akisema China imevutiwa na sera za CCM na hivyo itawekeza katika soko la pamba katika mkoa huo.
 
Ni katika mkutano huo, balozi huyo alicheza nyimbo za CCM za kubeza vyama vya upinzani huku akiwa amevalia kofia ya chama hicho.
 
Akizunguza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa CHADEMA, Ezekia Wenje, alisema balozi huyo amekiuka mkataba wa kimataifa wa Vienna kuhusu mambo ya kidiplomasia kifungu cha 41 (i).
 
Alisema kifungu hicho kinakataza mabalozi wa nchi kujiingiza katika masuala ya ndani ya nchi nyingine.
 
Wenje alibainisha kuwa mkataba huo unataka kazi za balozi kuwa ni kuwakilisha nchi na si chama.
“Balozi wa China yuko hapa kuwakilisha China nchini Tanzania, si Chama cha Kikomunisti kwa CCM,” alisema.
Wenje aliongeza kuwa haamini kama huo ndio msimamo wa serikali ya China na pia CCM kwani Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe, alinukuliwa akiwaonya mabalozi kuingilia mambo ya ndani ya nchi kwa nyakati tofauti wanapokuwa wameongea na vyama vya upinzani.
 
Alisema kuwa CHADEMA imeazimia kuiandikia barua serikali ya China ili kuweza kupata msimamo wake kwa tabia ya balozi huyu kuandamana na chama kimoja na kutumia vifaa vyake vya uenezi katika mikutano ya hadhara.
 
Aliongeza kuwa wataiandikia pia serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuomba ufafanuzi wa jambo hili na pia kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye ndiye msimamizi halali wa mkataba wa Vienna.
 
Naye Mkurugenzi wa Bunge na Hamashauri wa CHADEMA, John Mrema, alisema tabia hiyo inahatarisha uhusiano wa China na Tanzania endapo CHADEMA au chama kingine kitaingia madarakani.
 
Mrema Aliongeza kuwa kitendo hicho kinaongeza mazingira hatari kwa wawekezaji wa Kichina waliopo nchini hasa kwenye maeneo ambayo CCM haikubaliki.
 
Mkurugenzi wa Mafunzo na Oganaizesheni, Benson Kigaila naye alisema kuwa wanawashangaa CCM kwa kuwa wanafanya mzaha na kila kitu.
 
“Wametumia wafanyakazi wa serikali katika siasa kwa muda mrefu bila mafanikio hadi wameanza kutumia mabalozi ili waweze kukubalika kwa wananchi,” alisema.
 
 
CCM wajitetea
 
 

Alipotafutwa Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema kuwa ziara ya balozi huyo mkoani Shinyanga haikuwa ya kisiasa bali ilitokana na mazungumzo kati ya chama hicho na Chama cha Kikomunisti cha China.
 
Alisema kuwa lengo lilikuwa ni China kuweza kuwekeza katika kilimo cha pamba na mifugo kuongeza ajira.
 
“Katika suala hilo CCM ilikuwa nyuma ya kuhamasisha wawekezaji, Katibu wetu alipokwenda China aliomba wawekezaj na watawekeza katika viwanda kumi na sasa wameanza na vitatu, ndio sababu Balozi wa China alienda kumwonyesha Kinana.
 
Nape aliongeza kuwa balozi huyo alipita katika mkutano wa hadhara na kuomba kusalimia wananchi kuelezea uwekezaji utakaofanywa na China.
 
“CHADEMA kulalamika ni kwamba wameweweseka kwa kuwa wamezoea kutumia matatizo ya wananchi kama mtaji wa kisiasa, tatizo la bei ya pamba likiendelea ni mtaji kwao na likiisha watakosa mtaji wa kisiasa,” alisema.
 
Wizara yacharuka
Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe, hakupokea simu yake kufafanua suala hilo lakini alipoandikiwa ujumbe na kupigiwa tena simu ilipokelewa na msaidizi wake ambaye aliahidi kutuma taarifa.
 
Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa na Togolani Mavura kwa niaba ya Waziri Membe ilisema kuwa imefuatilia suala hilo kwenye vyombo vya habari kuhusu kushiriki kwa Balozi wa China nchini kwenye mkutano wa hadhara wa CCM.
 
“Taarifa hizo zimeambatana na picha zinazomuonyesha balozi huyo akiwa amevaa kofia yenye nembo ya CCM. Habari zinaeleza kuwa alikwenda Shinyanga kuhudhuria uzinduzi wa mradi wa viwanda vya kuchambulia pamba vinavyojengwa na mwekezaji wa Kichina anayeitwa Tahong.”
“Viwanda hivyo vitakuwa na uwezo wa kuchambua tani 120,000 za pamba kwa mwaka, vitakapokamilika mwakani,” alisema.
 
Aliongeza kuwa wizara inapenda kutamka kwamba kitendo cha balozi yeyote kuhudhuria mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa na kuvaa sare zenye nembo ya vyama sio sahihi.
 
Ni kukiuka kifungu cha 41(1) cha mkataba wa Vienna wa mwaka 1961, unaoongoza uhusiano wa kidiplomasia.
 
“Katika kipindi cha mwaka 2010 hadi 2012 wizara ilikumbana na vitendo vinavyofanana na kitendo hiki na ikachukua hatua stahiki.
 
“Kadhalika kwa tukio hili, waziri anakusudia kuchukua hatua za kidiplomasia zinazostahili ili kuzuia jambo hili lisitokee tena,” alisema.
 
Via - Tanzania Daima

Saturday, September 14, 2013

NAPE AMTAKA MBOWE AACHIE NGAZI, AMESHINDWA KAZI

Shinyanga.Katibu wa Itikadi na Uendezi wa Chama Cha mapinduzi (CCM),Nape Nnauye amemtaka Kiongozi wa Upinzani Bungeni,Freeman Mbowe kujiuzulu nafasi hiyo mara moja kwa sababu ameshindwa kuiongoza kambi hiyo.
 
Wito huo uliutoa mjini hapa Ijumaa jioni alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara wa kuhitimisha ziara ya siku Nne ya Katibu Mkuu wa Chama hicho, Abdulrahman Kinana katika mkoa huo.

 
Nape alisema vurugu zilizotokea hivi karibuni Bungeni ni uthibitisho wa wazi kuwa,Mbowe ameshindwa kuiongoza kambi hiyo kwa kuwa kabla yake hakukuwahi kuonekana fujo na vurugu kama hizo katika chombo hicho kinachoheshimika.
 
Alisema udhaifu wa Mbowe katika kuiongoza kambi hiyo ndiyo unaosababisha ishindwe kufanya kile ambacho Watanzania wanakitarajia kutoka kwa wapinzani.
 
Alisema wanasiasa ambao wanasababisha na kushabikia fujo na vurugu hawafai kwa madai kuwa wanaipeleka nchi mahali pabaya.

 
Hata hivyo, alisema hilo halitafanikiwa kwa sababu Serikali, CCM na Watanzania wapo makini dhidi ya mtu yeyote anayepanga kuwachonganisha. Aliishangaa Chadema kwa kushinikiza wabunge waongezwe kwenye Bunge la Katiba huku ikitaka wengi wa hao watokane na wanasiasa.
 
“Chadema inataka wawakilishi wa wakulima wawe kumi tu wakati wakulima ni asilimia 80 ya Watanzania wote. Hivi kweli wana lengo la kuwatetea Watanzania au maslahi binafsi tu,?”alihoji Nape.N

 
nape waliwataka wananchi kufanya uamuzi wa busara wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwakani na Uchaguzi Mkuu .

Via-Mwananchi

SUGU AMPONZA AFISA UPELELEZI MKUU WA DODOMA, AHAMISHISHIWA IRAMBA KWA MWIGULU NCHEMBA

Katika hatua nyingine, Mkuu wa Upelelezi wa Dodoma mjini, Jumanne Amasi, ameingia matatani na kulazimishwa kuhamia Iramba ili yule wa Kiomboi aende Dodoma kuisaidia CCM kukabiliana na wapinzani.
 
Taarifa kutoka chanzo chetu zimethibitisha kuwa mkuu huyo wa upelelezi amehamishwa kwa dharura kwenda Iramba kutokana na shinikizo la kigogo mmoja wa CCM.
 
Hatua hiyo inadaiwa kuwa ni kutokana na mkuu huyo kukataa maelekezo ya kigogo huyo yaliyomtaka amweke mahabusu mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (CHADEMA), baada ya fujo zilizotokea bungeni.
 
Inadaiwa kuwa awali mkuu huyo pia alikataa kumkatama Mbilinyi maarufu kama Sugu alipokuwa Desert Hotel ya mjini Dodoma, akitoa sababu kwa wakuu wake kwamba kosa la mbunge huyo lilitendekea bungeni na alipaswa kuwajibishwa kwa kanuni za Bunge.
 
Alipotafutwa msemaji wa polisi kwa simu kufafanua madai hayo, simu yake iliita bila kupokelewa.
Chanzo chetu kimethibitishiwa na Mkuu wa Upelelezi wa Iramba kuwa tayari amepokea taarifa za kuhamia Dodoma kikazi lakini akadai ni masuala ya kawaida.
Naye mkuu wa upelelezi wa Dodoma, hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo kwani alidai kuwa hana taarifa na kwamba kama atahamishiwa Iramba atachukulia kama sehemu ya kazi.
 
Via-Tanzania Daima

Thursday, September 12, 2013

KAMA ULIKUWA HUJUI, HII NDO SABABU ILIYOMWONDOA MCH. PETER MSIGWA, TLP

Mbunge wa Iringa mjini Mchungaji Piter Msigwa amefunguka kupitia ukurasa wake wa facebook na kueleza kile kilichomfanya kuachana na Mrema na TLP yake, hiki ndicho alichoandika, na kufuatia na picha chini ya maelezo haya:
 
Enzi za TLP NA BWANA Lyatonga ,IRINGA MJINI 2005,nikinadiwa nilipogombea ubunge kwa Mara ya kwanza, KWA SASA AMEAMUA KUWA MPAMBE WA CCM,NILIACHANA NAYE 2006 ,baada ya kuona mbele Giza
 
 

HILI SASA BALAA! MWANAMKE AJIFANYA MJAMZITO ABEBA COCAINE KWENYE TUMBO LAKE BANDIA AKAMATWA KIAINA

 
Mwanamke wa Kikanada amekamatwa huko Kolombia akiwa na madawa ya kulevya aina ya cocaine kilo mbili, mzigo huo aliubeba katika tumbo lake bandia akijifanya mama kijacho, Maofisa usalama walimshtukia mkanada huyo, mara baada ya kumuuliza ana mimba ya miezi mingapi? mdada alionekana kama hakulifurahia swali hilo, baada ya muda kidogo akajikuta akijibu kuwa, ana mimba ya miezi saba, jambo ambalo liliwatia wasi wasi vijana 'Saidi Mwema' wa Kolombia, si ndo wakaanza kuichunguza hiyo mimba bwana! Kugusa tumbo, tumbo gumu kama mpira wa miguu! duuh! tumbo lenyewe bwana, likawa la baridi kama limetolewa kwa friji, hapo ndipo msala ukaanza, tazama picha za tukio Zima hapa chini:


Mdada akiwa chini ya ulinzi na katumbo kake bandia
 
Unaliona tumbo lenyewa la miezi saba!
 

Ona tumbo hilo!
 
Latex belly and cocaine that was hidden under it
Tumbo lenyewe hilo kushoto na kulia ndiyo mzigo wenyewe
 
Tumbo lenyewe hilo kushoto na kulia ndiyo mzigo wenyewe
 
 

MZEE MAJUTO ATELEKEZA MKE WA MIAKA 20 HUKO MBAGALA, MWEYEWE ADAI BINTI HAJATULIA


MWANAMKE anayedaiwa kufunga ndoa ya siri na mchekeshaji mahiri Bongo, Amr  Athuman maarufu kama Mzee Majuto au King Majuto, Rahma Abdallah (20), ameibuka na kudai kutelekezwa na mumewe huyo.
Ndoa hiyo ambayo ilifungwa kwa siri jijini Dar Julai 28, mwaka huu na kudumu siku 44, inaonekana imevunjika rasmi baada ya Mzee Majuto kutoa talaka kupitia kwa msanii wa filamu aitwaye Rehema Omary.

Akizungumza na mwandishi wetu, Septemba 9, mwaka huu, Rahma alidai kuwa alikutana na Mzee Majuto jijini Tanga na kuanzisha uhusiano wa kimapenzi kwa miezi sita kabla ya kufunga ndoa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani uliopita.
 
“Tulifahamiana Tanga, mimi ni mwenyeji wa huko kama ilivyo kwa Mzee Majuto, wakati tukiwa kwenye uhusiano, ulipofika Mwezi wa Ramadhani akaona bora tufunge ndoa ili tusiendelee kutenda dhambi, akaniambia dhamira yake hiyo nami sikukataa,” alisema Rahma.
Mke huyo ambaye ni kibinti cha umri wa miaka 20 aliyepishana na Mzee Majuto kwa umri wa miaka 40 alisema kuwa, mwigizaji huyo alifuata taratibu zote za kufunga ndoa kwa kupeleka barua ya posa nyumbani kwao.

 
“Alitoa mahari ndipo ilipopangwa siku ya ndoa iliyofungwa nyumbani kwa mama yangu, Mbagala-Zakhem, Dar,” alifafanua Rahma.

Katika ndoa hiyo iliyofungwa katika Mtaa wa Kibonde-Maji Julai 28, mwaka huu na Shehe Abdurahman Kisoma na kufuatiwa na sherehe nyumbani kwa bibi harusi, ulinzi mkali uliwekwa ili siri ya Mzee Majuto kuoa isivuje.
Mashahidi wa ndoa hiyo walikuwa ni Suleiman Said ‘Barafu’ ambaye ni mwigizaji aliyekuwa mpambe wa bwana harusi pamoja na Mohammed Malila.
Cheti cha ndoa hiyo, kinaonesha kwamba Mzee Majuto alimuoa mwanamke huyo kwa mahari ya shilingi 20,000 aliyolipa yote.
 
“Baada ya ndoa, Mzee Majuto aliwaomba wazazi wangu nikae nyumbani hadi Mwezi wa Ramadhani utakapoisha ndipo atakapokuja kunichukua, akaniachia shilingi elfu sitini tu, mpaka leo hii sijamuona,” alisikitika mke huyo ambaye alikuwa akijua kama Mzee Majuto alikuwa na mke mwingine.
Mke huyo wa Mzee Majuto alisema kuwa kabla ya kufunga ndoa na gwiji huyo wa uchekeshaji alikuwa akifanya kazi katika saluni ya mwanamuziki Joseph Haule ‘Profesa Jay’ iliyopo Msasani, Dar.
 
“Nilikuwa nafanya kazi na kupata kipato huku nikiwa nimepanga chumba lakini Majuto aliniambia niache kazi na nirudishe chumba, nami nikafanya hivyo nikijua naenda kuishi kwa mume wangu, kumbe!...” alijuta Rahma.
  Baada ya Majuto kuondoka mke huyo alikuwa akimpigia simu kutaka fedha za matumizi lakini alikuwa akiambiwa awasiliane na Bi. Rehema, mwanamke ambaye Mzee Majuto huwa anaigiza naye katika filamu zake.
 Rahma alilalamika kutumiwa ujumbe wa matusi kwenye simu yake na mke mkubwa wa Mzee Majuto.
 “Kitendo hicho kinaniuma sana kwani wakati mwingine huwa ananitukana na kunitishia maisha, akidai eti atanifanyia kitu kibaya, nikimpigia Majuto na kumweleza naye ananijibu mbovu,” aliongeza.
 
Mke huyo mdogo wa Mzee Majuto alisema kuwa anaumia kutokana na kuharibiwa maisha kwa kuolewa na kuachishwa kazi huku akiendelea kutukanwa na mke mkubwa.
  
Rahma ambaye aliliachia Amani nakala ya cheti cha ndoa alisema msanii huyo amemdhalilisha kwani kila akidai talaka yake anamwambia ameshaituma kwa Bi. Rehema na kumtaka aende akaichukue kitu ambacho ni kinyume na makubaliano yao.
Rahma alisema kuwa amejipanga kwenda kumshitaki Mzee Majuto katika Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) ili amlipe fidia na kumtafutia kazi.
 
“Yeye ndiye aliyenioa lakini nikimdai talaka ananimbia alimpa Bi.Rehema, wakati mwanamke huyo siye aliyenioa, sasa nampeleka Bakwata ili anikabidhi talaka na kunilipa fidia,” alisema kwa hasira mke huyo.
  
Akijibu tuhuma hizo akiwa jijini Tanga, Mzee Majuto alikiri kufunga ndoa na Rahma na kusema kuwa alishamuacha kwa sababu aligundua hajatulia.

“Huyo mwanamke nimeshaachana naye ila kwa sasa anataka kunichafua, kama anahisi ana haki kwa nini asiende mahakamani? Nimemtuma mshenga ampe talaka hataki kuipokea, anataka nije Dar. Kama huo siyo uhuni ni nini? huyo mwanamke hajatulia,” alisema.


Chanzo: Gazeti la Amani


KIJIJI CHA SASAJILA-MANYONI HAKINA ZAHANATI KWA MIAKA 37 SASA

KIJIJI cha Sasajila, kilichopo Wilaya ya Manyoni, Singida, hakina zahanati wala duka la dawa tangu kuanzishwa kwake miaka 37 iliyopita.
 
Diwani wa Viti Maalumu, Christina Ndahani, alibainisha hayo alipozungumza na Tanzania Daima katika kijiji hicho kilichopo Jimbo la Manyoni Mashariki.
 
Alisema wananchi wa eneo hilo hutumia zahanati ya Makasuku na Chibumwaga ambako hulazimika kutembea zaidi ya saa mbili ili kufika ama kutumia nyingine ya Mpandagani ambayo hutumia saa tatu.
Diwani huyo alieleza kuwa wananchi wanapolazimika kwenda hospitali kubwa ya Kilimatinde hutembea saa tano kwa mguu ili kufika na kupata huduma.
 
Alisema wanaoteseka zaidi ni wanawake wajawazito na watoto, kwani baadhi yao hufariki dunia njiani.
“Mwezi huu wanawake wawili walijifungua njiani, vifo vingi ni kutokana na hali hiyo. Kama wahisani watapatikana tukanyanyua saizi ya lenta katika jengo la zahanati itakuwa mkombozi mkubwa kwa kijiji, kwani serikali itaona na kuimalizia,” alisema diwani huyo.
 
Alieleza kuwa kutokana na kutokuwapo kwa zahanati katika kijiji hicho, baadhi ya wananchi hukimbilia kwa waganga wa jadi kupata matibabu, matokeo yake vifo vinaongezeka.
 
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone alisema kutokana na agizo la Rais Jakaya Kikwete kuwa kila kijiji kiwe na zahanati, wamehamasisha wananchi kuanza michango kwa ajili hiyo, ili serikali nayo iunge mkono.
 
Chanzo: Tanzana Daima

KINANA AMWANGUKIA TUNDU LISSU, AJISALIMISHA KWAKE

WAKATI rufaa ya kupinga ubunge wa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA) ikitarajiwa kuanza kusikilizwa katika Mahakama ya Rufaa Dodoma, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Wakili wake, Godfrey Wasonga, kimeiomba mahakama hiyo kuifuta kesi hiyo.
 
Kwa mujibu wa wakili huyo, sababu ya kuomba kufutwa kwa kesi hiyo ni kutokana na walalamikaji wote kujitoa na kuapa mahakamani kuwa hawapo tayari kuendelea na kesi hiyo.
 
Hata hivyo wakazi wawili wa Kijiji cha Makiungu mkoani Singida, Shabani Selema na Paskali Hallu, ambao walifungua kesi ya msingi kupinga ubunge wa Lissu, tayari walikwisha kuweka bayana kukubaliana na hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma Aprili, mwaka huu.
 
Mara kadhaa wananchi hao wamenukuliwa wakimlalamikia Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, kuwa anawashinikiza kuendelea na rufaa hiyo licha ya kwamba walikwisha kujitoa.
 
Akizungumza na gazeti hili jana, Wasonga ambaye alikuwa akiwatetea wanachama hao katika kesi hiyo, alisema kuwa baada ya kuwasiliana na wateja wake walimwambia hawapo tayari kuendelea na kesi hiyo.
“Ni kweli walalamikaji wote wamejitoa na mimi kama wakili sioni haja ya kuendelea, nitakuwa namwakilisha nani? Nimeongea nao jana, hakuna mwenye nia ya kuendelea na kesi,” alisema.
 
Wasonga alipoulizwa kama bado anadai malipo kutoka kwa walalamikaji hao, alisema japokuwa wateja wake ni wanakijiji wasio na uwezo mkubwa wa fedha walijitahidi kulipa madai yote.
 
Gazeti hili pia liliwatafuta Selema na Paskali wakiwa Muyanji kijijini, ambapo walisema kuwa: “Sisi tulishatoa msimamo tangu mapema hatuna mpango wa kuendelea na kesi.
 
“Tuliapa mahakamani lakini tulishangaa kuona kesi hiyo inapangiwa majaji, sisi pia tumepata taarifa kuwa huyo wakili aliyekata rufaa bila ridhaa yetu amepeleka ombi mahakamani ili kesi iondolewe, hayo ni matakwa yake binafsi kama yeye alikuwa anafuata maneno ya Kinana,” walidai.
 
Naye Lissu alilithibitishia gazeti hili kuwa tayari anao wito wa mahakama kesho kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo.
 
Alisema kuwa jana jioni alipata barua kutoka kwa wakili wa walalakaji kwenda Mahakama ya Rufaa, wakiomba kuifuta rufaa hiyo.
 
“Nimepokea samansi niende kusikiliza kesi hiyo siku ya Ijumaa na tayari nilishaweka pingamizi kupinga rufaa hiyo. Hii taarifa ya kuondolewa au kufutwa kesi wakati tayari nimeshaweka pingamizi nitatoa msimamo siku hiyo palepale mahakamani kwa kutumia vigezo vya kisheria,” alisema.
 
Rufaa hiyo imepangiwa kusikilizwa katika Mahakama ya Rufaa na jopo la majaji watatu, Salumu Massati, Engela Kileo na Natalia Kimaro.
 
Kabla ya kuanza kusikilizwa kwa rufaa hiyo, mahakama ilitarajiwa kusikiliza pingamizi zilizotolewa na upande wa walalamikiwa, ambao ni Lissu na Jamhuri za kupinga rufaa hiyo na jopo hilo la majaji litatoa uamuzi.
 
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana, Lissu alitoa hoja saba za kupinga rufaa hiyo, muda mfupi kabla hajapokea maombi hayo ya kuiondoa kesi hiyo.
 
Lissu alisema hoja hizo ni mkata rufaa Selema ambaye ndiye mlalamikaji namba moja kupinga kwamba hajakata rufaa kwa hati ya kiapo ya Mei 24, mwaka huu.
 
Alisema hoja nyingine ni notisi ya kiapo kutopelekwa kwa mjibu rufaa, ambaye ni yeye, kinyume cha masharti ya kanuni ya 84 (1) ya Kanuni za Adhabu za Mahakama ya Rufaa Tanzania za mwaka 2009.
“Vilevile nakala zote rekodi ya rufaa hazijathibitishwa usahihi wao, na wakata au wakili kinyume cha masharti ya Kanuni ya 96 (5) ya Kanuni za Mahakama ya Rufaa Tanzania za mwaka 2009.
 
“Rufaa hii pia imepitwa na muda wake, kwa sababu hati ya ucheleweshaji iliyotolewa na Msajili wa Mahakama Kuu haijasainiwa, haina tarehe wala muhuri, kinyume cha Kanuni ya 90 (1) ya Kanuni za Mahakama ya Rufaa ya Tanzania za mwaka 2009,” alisema.
 
Lissu aliongeza kuwa walalamikaji walitakiwa kukata rufaa siku sitini baada ya notisi ya rufaa kutolewa na kwamba tarehe ya mwisho ya kukata rufaa ilikuwa Julai 3, mwaka jana, lakini rufaa hiyo ilikatwa Mei 7 mwaka huu.
 
“Hoja nyingine ni kwamba rufaa hiyo si halali kwa kuwa imeacha nyaraka muhimu, ikiwamo maombi ya mwenendo wa shauri wa kusamehewa gharama za dhamana,” alisema.
 
Lissu alisema pia katika rufaa hiyo, amri iliyomshindisha kesi si halali, kwa kuwa haionyeshi tarehe ambayo amri hiyo ilitolewa, kinyume cha kanuni ya 9 ya Kanuni za Masijala za Mahakama Kuu za mwaka 2005.
 
Alisema pia wakata rufaa wamesindwa kuwasilisha mahakamani hoja za maandishi za kuunga mkono hoja za rufaa yao ndani ya siku 60 au kuomba muda wa kuziwasilisha.
 
Pia hoja nyingine ni kushindwa kuwasilisha hoja hizo za maandishi kinyume cha Kanuni ya 106 (1), (2) na (9) ya Kanuni za Mahakama ya Rufaa ya Tanzania za mwaka 2009.
 
Kesi ya kupinga ubunge wa Lissu ilianza kusikilizwa Machi 12, 2012 na Jaji wa Mahakama Kuu, Moses Mzuna, aliyetoa hukumu Aprili 27, mwaka huu na kumtangaza Lissu kuwa mbunge halali wa Singida Mashariki, kwa kigezo kuwa hoja zote zilizotolewa na wanachama hao wa CCM hazitoshi kutengua au kubatilisha ubunge wake.
 
Kufuatia hukumu hiyo, wanachama hao wa CCM waliridhia hukumu ya Mahakama Kuu, hivyo kuandika barua kwa Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Kati kuomba wapewe fedha walizokuwa wameweka kama dhamana yao sh milioni 15.
 
Lakini Ofisi ya Msajili wa Mahakama Kuu imekuwa ikisuasua kutoa majibu kurejesha fedha hizo kwa Selema na Halu.
 
Chanzo: Tanzania Daima

Sunday, September 8, 2013

HII SASA NI HATARIII, Meli ya Tanzania yanaswa Italia na tani 30 za madawa ya kulevya

JITIHADA za Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, kuimarisha mitambo ya ukaguzi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) ili kuwanasa wabeba dawa za kulevya (unga), zimeanza kufifishwa baada ya mtandao kubuni mbinu mpya.
 
Wakati hali ikiwa hivyo, meli ya mizigo yenye usajili wa Tanzania imekamatwa nchini Italia ikiwa na tani 30 za mihadarati aina ya bangi yenye thamani ya sh bilioni 123.
 
Kwa mujibu wa chanzo chetu, wafanyabiashara hao wa dawa za kulevya tayari wameanza kuupa kisogo uwanja wa JNIA na badala yake kuelekeza mikakati hiyo katika uwanja wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
 
“Hatua ya Mwakyembe kufunga mtambo JNIA imewashtua watu wengi na hivi sasa tayari kuna watu watatu ninaowafahamu wameshaweka kambi hapa Moshi kwa ajili ya kusuka mipango ya kusafirisha dawa hizo kwa kutumia uwanja wa KIA,” kilisema chanzo chetu.
 
Mmoja kati ya watu wanaotajwa kufanya biashara hiyo ni raia wa Kenya, Hussein Mombasa, ambaye ameomba uraia wa Tanzania kisha kufanikiwa kufunga ndoa na Halima Mosha.
Kwa kujibu wa chanzo hicho Halima ni ndugu wa karibu na mhasibu mkuu hazina ndogo mkoa wa Iringa, Twaha Mtalika, ambaye ni kaka wa mama yake.
 
Mkenya huyo mbali na kufanikiwa kupata uraia wa Tanzania anadaiwa pia kushirikiana na mkewe huyo kufanya biashara hiyo haramu.
 
Mombasa anadaiwa kumeza dawa aina ya cocaine kisha kusafiri nazo katika nchi mbalimbali na kwamba karibu safari zote alizokuwa akizifanya alikuwa akipitia katika uwanja wa JNIA bila tatizo kutokana na kuwa na mtandao uliokuwa ukimkingia kifua pale uwanjani.
 
“Huyu Mkenya ameshafunga ndoa na huyu mwanamke tangu Julai 5, mwaka huu, na wanaishi katika nyumba ya mjomba wa mkewe iliyoko Ilala Mtaa wa Kilwa.
 
“Shughuli nyingi za kuingiza hizo dawa huzifanyia hapo na mjomba mtu ameamua kuwaachia nyumba hiyo kwa sababu yeye anafanya kazi mkoani,” kilisisitiza chanzo hicho.
 
Nchi ambazo Mkenya huyo anatajwa kusafiri kwa ajili ya kupeleka mzigo akitokea jijini Dar es Salaam ni Hispania ambako alikwenda akipitia uwanja wa JNIA na kurejea Mei mwaka huu, wakati mwaka jana alipeleka dawa hizo Afrika Kusini na kurejea Machi.
 
Inadaiwa kuwa pamoja na ndoa ya Halima kufungwa kihalali lakini bado mwanamke huyo anang’ang’ania kuendelea kuwa sehemu ya umiliki wa nyumba iliyoko Moshi, aliyochuma na Dominick Ngowi ambaye aliishi naye awali na kupata watoto wawili: Oliver Dominick (19) na Frank (18).
 
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Moshi, Stella Mugasha, alishatoa hukumu Agosti 19, 2011 na kuamuru watoto hao watakapotimiza umri wa miaka 18 wamilikishwe nyumba hiyo baada ya baba yao kufungua kesi ya madai (gazeti hili lina nakala zote zikiwemo za hukumu).
 
Hata hivyo, tayari mtoto mkubwa, Oliver ameshakabidhiwa umiliki huo siku chache zilizopita kwa niaba ya mwenzake mbele ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Sabasaba Kata ya Soweto, Pamela Shuma na ofisa mtendaji katia hiyo, Gudila Kimboka.
 
Wakati Mkenya huyo akidaiwa kusafirisha unga kwenda nje ya nchi, Halima anatajwa kuzisafirisha kwa ustadi mkubwa kwa njia ya mabasi na kuzipeleka mkoani Tanga eneo la barabara ya 11, Namanga na Arusha, na kwamba ameshafanya hivyo mara nyingi.
 
“Wakati mwingine Ilala kukikosekana mzigo, huenda kuzichukua katika eneo la Magomeni Mapipa ambako kuna jumba moja la kifahari wakati kwa mkoani huficha mzigo wao Moshi nyumbani kwa mwanamke mmoja maarufu ambaye pia ni ndugu wa karibu wa Mombasa,” kilieleza chanzo kingine cha habari.
 
Habari zaidi zinadai kuwa Halima amekuwa mstari wa mbele kukisaidia chama kimoja maarufu cha siasa nchini ambako ni mmoja wa viongozi wa wanawake mkoani Kilimanjaro.
Tanzania Daima, ilipomtafuta mjomba wa mwanamke huyo Twaha Mtalika ili kutaka kupata ukweli wa madai ya nyumba yake kutumiwa kufanyia biashara hiyo haramu, aling’aka na kueleza kutojua masuala hayo.
 
Twaha ambaye anadaiwa kuwepo jijini Dar es Salaam kimasomo alijibu kwa mkato: “Mwambie huyo kijana aliyekutuma uniulize hayo azungumze na mwanamke wake na asiniingize mimi katika masuala yao.”
 
Naye Halima alipoulizwa kuhusu madai hayo, alijielekeza zaidi kwenye madai ya kuwahusu watoto wasimilikishwe nyumba wakati mahakama ilishaamuru hilo.
 
Huku akikanusha madai ya kughushi cheti cha kuzaliwa cha mtoto wake wa pili Frank kwa lengo la kumpunguza umri ili kuharibu mchakato wa umiliki huo kwa kushirikiana na mjomba wake, pia alisema tuhuma za kusafirisha unga si za kweli.
 
Meli yabambwa Italia
Taarifa za kukamatwa kwa meli hiyo ya MV Gold Star, zilichapishwa hivi karibuni kwenye gazeti la Daily Mail la nchini Uingereza.
 
Meli hiyo ambayo imesajiliwa Tanzania kwa upande wa Zanzibar ilikamatwa baada ya vyombo vya usalama vya nchi hiyo kupata taarifa kuwako kwa meli hiyo iliyokuwa na shehena hiyo.
Baada ya taarifa hizo Kikosi cha Coastgurd cha Italia, kilifuatilia meli hiyo kwa kutumia helikopta na hatimaye kufanikiwa kuinasa.
 
Meli hiyo inadaiwa kuwa wakati inakamatwa ilikuwa na watu tisa baadaye walijaribu kujitosa baharini, miongoni mwao wakiwemo mabaharia wawili, mmoja akiwa raia wa Misri na mwingine wa Syria.
 
Hata hivyo, watu saba waliobakia uraia wao ulikuwa haujafahamika.
Chanzo hicho kilieleza kuwa shehena hiyo ya bangi imepakuliwa pwani ya Uturuki karibu na Italia.
Alipotafutwa Mkuu wa Interpol, Gustavs Babile ili kutoa ufafanuzi, alisema ni kweli meli hiyo iliyosajiliwa Zanzibar ilikamatwa ikiwa na bendera ya Tanzania.
 
“Hata hivyo siwezi kuzungumzia mengi kama unavyojua leo ni Jumapili niko nje ya ofisi lakini hizo ndizo taarifa ambazo ziko kwenye nyaraka ambazo tunazo,” alisema.
 
Baadhi ya Watanzania katika siku za hivi karibuni walinaswa na mihadarati kwenye nchi mbalimbali za Afrika Kusini, Hong Kong na China.
 
Chanzo: Tanzania Daima